Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Tetesi za Soka Ulaya Jumapil: Inter Milan inamfukuzia kipa wa Tottenham
Inter Milan inamtaka mlinda lango wa Tottenham Muitaliano Guglielmo Vicario, 29, kuwa kipa wao mkuu mpya. (CalcioMercato - kwa Kiitaliano)
Chelsea ina nia ya kumsajili beki wa Argentina Valentin Barco, 21, kutoka klabu ya Strasbourg. (Talksports)
Liverpool inapania kumjumuisha beki wa kulia wa Atalanta Mtaliano Marco Palestra mwenye umri wa miaka 21 kwenye kikosi chao msimu huu wa joto. (CaughtOffside)
Manchester United ni mojawapo wa klabu kadhaa za Ligi ya Premia zinazomfuatilia beki wa Blackburn wa Ireland Kaskazini Tom Atcheson, 19. (Teamtalk)
Sunderland huenda ikamsajili kiungo mkabaji wa Almeria, 24, Sergio Arribas ikiwa mkurugenzi wa michezo Florent Ghisolfi atafuatilia nia ya muda mrefu. (Sport Witness)
Arsenal inajiandaa kumenyana na Liverpool katika usajili wa mshambuliaji wa Newcastle Anthony Gordon, 25. (Football Transfers)