Unachopaswa kujua kuhusu vikosi vitakavyoshiriki mashindano ya kombe la dunia 2026

Muda wa kusoma: Dakika 3

Nchi sita za mwisho zimefuzu kwa Kombe la Dunia 2026, hivyo kukamilisha orodha ya timu 48 zitakazoshiriki katika mashindano hayo.

DR Congo na Iraq zilikuwa timu za mwisho kufuzu, baada ya kujipatia fursa ya kushiriki mashindano ya Kombe la Dunia yatakayofanyika nchini Marekani, Canada na Mexico kuanzia tarehe 11 Juni hadi 19 Julai.

Mchakato mrefu wa kufuzu kushiriki katika kombe hilo ulioanza Septemba mwaka 2023 sasa umekamilika, ukihusisha mashirikisho sita ya soka duniani.

Timu nne za mwisho kutoka Ulaya ziliidhinishwa siku ya Jumanne, huku habari kubwa ikiwa ni kwamba mabingwa wa mara nne Italia walitolewa na BosniaHerzegovina. Jamhuri ya Czech, Uturuki na Uswidi pia zilifuzu.

DR Congo na Iraq zilipata tiketi zao baada ya ushindi dhidi ya Jamaica na Bolivia mtawalia.

Kati ya timu 48 zitakazoshiriki, nchi tatu ambazo ni wenyeji wa kombe hilo walifuzu moja kwa moja, huku nafasi 43 zikijazwa kupitia hatua za kufuzu katika mashirikisho mbalimbali, na nafasi mbili za mwisho huamuliwa kupitia mchujo wa mabara tofauti.

Sasa, baada ya timu zote kuidhinishwa macho yanaelekezwa kwenye Kombe la Dunia.

Mashindano ya Kombe la Dunia 2026 yataendeshwaje?

Mashindano ya mwaka huu 2026 yatakuwa makubwa zaidi kuwahi kufanyika, ikiwa na jumla ya timu 48 , hii ikiwa ongezeko kutoka timu 32 zilizoshiriki Kombe la Dunia 2022. Jumla ya mechi 104 zitachezwa katika nchi tatu kwa mara ya kwanza.

Mashindano haya yatafanyika kati ya tarehe 11 Juni hadi 19 Julai katika miji 16, miji 11 nchini Marekani, mitatu Mexico na miwili Canada.

Pia yatadumu kwa siku 39 , ikilinganishwa na siku 29 mwaka 2022 na siku 32 katika mashindano ya 2014 na 2018. Mfumo mpya wa mashindano utakuwa na makundi 12, kila kundi likiwa na timu nne.

Mechi ya ufunguzi itawakutanisha Mexico dhidi ya South Africa katika Estadio Azteca, jijini Mexico City tarehe 11 Juni siku 18 baada ya kumalizika kwa msimu wa Premier League.

Timu mbili za juu kutoka kila kundi,jumla timu 24 pamoja na timu nane bora zilizoshika nafasi ya tatu zitasonga mbele hadi hatua ya mtoano, ambayo itaanza na timu 32.

Bingwa mpya wa dunia atapatikana tarehe 19 Julai katika MetLife Stadium, iliyoko New Jersey.

Makundi ya timu zitakazoshiriki kombe la dunia

  • Kundi A

Mexico

Afrika Kusini

Korea Kusini

Jamhuri ya Czech

  • Kundi B

Canada

Bosnia-Herzegovina

Qatar

Uswizi

  • Kundi C

Brazil

Morocco

Haiti

Scotland

  • Kundi D

Marekani

Paraguay

Australia

Uturuki

  • Kundi E

Ujerumani

Curaçao

Ivory Coast

Ecuador

  • Kundi F

Uholanzi

Japan

Tunisia

Sweden

  • Kundi G

Ubelgiji

Misri

Iran

New Zealand

  • Kundi H

Uhispania

Cape Verde

Saudi Arabia

Uruguay

  • Kundi I

Ufaransa

Senegal

Iraq

Norway

  • Kundi J

Argentina

Algeria

Austria

Jordan

  • Kundi K

Ureno

DR Congo

Uzbekistan

Colombia

  • Kundi L

Uingereza

Croatia

Ghana

Panama

Mechi za Kombe la Dunia 2026 zitachezwa lini?

Kutokana na mechi kufanyika katika maeneo yenye tofauti ya saa nne na umbali wa hadi maili 2,800 kati ya viwanja,mechi hizo zitaanza katika saa tofauti.

Hii ina maana kwa watazamaji wa Ulaya, baadhi ya mechi zitachezwa kuanzia saa sita usiku.

Kwa mfano, mechi zote tano za hatua ya makundi zitakazochezwa katika uwanja wa Kansas City zitakuwa usiku wa manane kwa saa za Uingereza.

Mechi ya mapema zaidi itaanza saa sita usiku siku ya Ijumaa, tarehe 26 Juni kati ya Tunisia na Uholanzi, huku mechi ya mwisho ikiwa kati ya Algeria na Austria Jumapili, tarehe 28 Juni.

Eneo la San Francisco Bay litakuwa mwenyeji wa mechi mbili Austria dhidi ya Jordan Jumanne, tarehe 16 Juni na Uturuki dhidi ya Paraguay siku ya Ijumaa, tarehe 19 Juni.

Pia kutakuwa na mechi mjini Vancouver Australia dhidi ya Uturuki siku ya Jumamosi, tarehe 13 Juni na katika Guadalupe, Tunisia watakapocheza dhidi ya Japan siku ya Jumamosi, tarehe 20 Juni.

Kwa jumla, kutakuwa na mechi 35 za hatua ya makundi zitakazoanza.