Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Tetesi za soka Ulaya Alhamisi: Real Madrid yawasiliana na kiungo wa Newcastle Sandro Tonali
Wawakilishi wa Sandro Tonali wamewasiliana na Real Madrid kama sehemu ya harakati za kutafuta klabu ijayo ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25, huku Manchester City pia wakiwa na nia ya kumsajili kiungo huyo wa kati wa Newcastle na Italia. (TeamTalks)
Kiungo wa kati wa Uingereza John Stones hatarajiwi kupewa ofa mpya na Manchester City, huku klabu ya zamani ya Everton ikiwa miongoni mwa wanaofuatilia hali yake. (Sportsport),
Barcelona wanaongoza katika kinyang'anyiro cha kumsajili kiungo wa kati wa Manchester City na Ureno Bernardo Silva, 31, kwa uhamisho wa bure msimu huu wa joto. (Sun)
Arsenal inamfuatilia mshambuliaji wa Bayer Leverkusen na Cameroon Christian Kofane, 19, huku klabu hiyo ya Ujerumani ikitaka hadi £60m kwa uhamisho wa majira ya joto. (Florian Plettenberg)
Chaguo la Barcelona la pauni milioni 26 kumnunua kwa mkopo mshambuliaji wa Uingereza Marcus Rashford, 28, lilimalizika mwezi Machi, kumaanisha kwamba klabu hiyo ya Uhispania lazima sasa ifanye mazungumzo na Manchester United kuhusu ada ya uhamisho. (Cadena SER - In Spanish)
Manchester City, Liverpool na Chelsea wanamfuatilia beki wa Barcelona na Ufaransa Jules Kounde, 27. (Mundo Deportivo - In Spanish)
Beki wa kulia wa Inter Milan na Uholanzi Denzel Dumfries, 29, amepewa ofa kwa vilabu vya Premier League vikiwemo Liverpool, Manchester City, Manchester United, Chelsea, Tottenham na Newcastle United. (TeamTalks)
Manchester United wanavutiwa na beki wa Benfica na Uswidi Samuel Dahl, 23, na wametuma maskauti kumtazama zaidi ya mara 10 msimu huu. (Record via SportWitness)
Celta Vigo wanataka kiungo wa kati Mhispania Fer Lopez, 21, kusalia katika klabu hiyo baada ya mkopo wake kutoka Wolves kukamilika mwishoni mwa msimu. (Faro de Vigo via SportWitness)
Roberto de Zerbi anataka kumsajili kiungo wa kati wa Juventus na Italia Manuel Locatelli, 28, kwa Tottenham msimu wa joto. (Calciomercato - Italy)
Manchester United na Liverpool wanahaha kumnunua winga wa Ivory Coast mwenye umri wa miaka 19 na RB Leipzig Yan Diomande. (Sportsboom)