Oman yasema inafanya mazungumzo na Iran kuidhinisha meli kutumia mlango wa Bahari wa Hormuz.
Meli ya mzigo imepigwa picha ikipitia kwa mlango wa Hormuz, ambao ulifungwa na Iran tangu vita vilipoanza.
Hatua ya Iran kufunga mlango wa Hormuz – ambayo ni njia muhimu sana katika uchukuzi wa baharini kimataifa – imesababisha bei ya bidha mbali mbali za mafuta na nishati kupanda kote duniani na kuweka shinikizo kubwa kwa uchumi wa dunia.
Wizara ya mambo ya kigeni ya Omana imesema kwamba Maafisa wakuu wa serikali za Omana na Irana wamekutana kwa ajili ya kutafuta Suluhu kwa mzozo unaoendelea na kufunguliwa kwa mlango wa Hormuz. Katika ujumbe uliochapishwa kwenye mtandao wa kijamii wa X wizara hiyo ya mambo ya kigeni ya Oman imesema kwamba viongozi hao wa pande hizo mbili walijadiliana kuhusu mbinu za kupitisha meli kwenye mlango huo wa Bahari kwa njia salama bila matatizo.
Mkutano huo uliofanyika Jumamosi, uliwajumusha wataalamu kutoka pande zote mbili, huku mapendekezo kadhaa ya kitaalamu yakitolewa.
Rais wa Marekani Donald Trump amesema kwamba Teharan nisharti ifunguwe mlango wa Hormuz amba oni njia muhimu ya uchukuzi wa baharini siku ya Jumatatu au kujiandaa kukabiliwa vikali zaidi.
Katika ujumbe wa hivi punde aliouchapisha kwenye mtandao wake wa kijamii wa Truth Social, Rais Trump ametumia maneno makali kuitishia Iran na hata matusi akisisitiza kwamba, ‘'Ni sharti mlango huo wa Bahari wa Hormuz ni sharti ufunguliwe la sivyo basi Iran itashuhudia jahanamu hapa duniani.'‘ Alisema Trump akiendelea kwa kuandika kwamba anamsifu Allah.