Moja kwa moja, Vita vya Iran: Rubani wa pili ameokolewa - Trump

Kulikuwa na ‘‘makabiliano’’ kati ya vikosi vya Marekani na Iran wakati wa uperesheni ya uokoaji wa rubani huyo.

Moja kwa moja

Na Ambia Hirsi & Laillah Mohammed

  1. Habari za hivi punde, Iran ilikuwa 'karibu kumpata' mwanajeshi wa Marekani aliyepotea nchini humo – Trump

    Donald Trump

    Chanzo cha picha, EPA

    Rais wa Marekani Donald Trump amesema kwamba mwanajeshi aliyekuwa akitafutwa na Majeshi ya Marekani na Irani katika eneo la milimani kusini mwa Iran, nusra akamatwe na wanajeshi wa Iran.

    Katika ujumbe aliouchapisha mapema leo katika ukurasa wa mtandao wa kijamii wa TRUTH SOCIAL, Rais Trump alitoa maelezo zaidi kuhusu juhudi za kumuoka mwanajeshi huyo wa pili aliyepotea Iran baada ya ndege aliyokuwa ndani aina ya F-15-E kudunguliwa siku ya Ijumaa.

    “Tumemuokoa mwanajeshi huyo ambaye amejeruhiwa vibaya na aliyestahmili mazingira makali kw aujasiri. Operesheni ya kumuokoa ilitekelezwa katika eneo la ndani la milimani huko Iran. Jeshi la Iran lilikuwa linamkaribia mwanajeshi huyo na lilikuwa limetekeleza operesheni kali ya kumtafuta, kwa kutumia idadi kubwa ya wanajeshi wa ardhini na teknolojia ingawa walikuwa karibu sana kumfikia. Mwanajeshi huyo ni afisa mwenye kiwango cha Kanali anayeheshimika sana.”

    '‘Aina hii ya operesheni haijawahi kutelekezwa wakati mwingine na ni nadra sana kufanyika kwa sababu ya hatari kwa binadamu na mashine ambazo hutumiwa. Operesheni ya pili, ilifanyika muda mfupi baada ya ile ya kwanza, ambapo tulimuokoa Rubani na afisa wa kwanza mchana peupe, jambo ambalo pia si la kawaida, na ilituchukuwa saa saba ndani ya himaya ya Iran.’'

    “Huu ni ujasiri, na uwezo wa kutekeleza kazi ulioonyesha na wahusika wote. Nitaandaa kikao cha wanahabari kwa pamoja an Jeshi la Makerakni katika ofisi ya Rais ya Oval Jumattau saa saba mchana. Mungu aibariki Jeshi letu na Mashujaa wetu. Rais DONALD J.TRUMP”

    Maelezo zaidi:

  2. Mashambulizi ya ndege zisizokuwa na rubani yasababisha hasara kubwa katika vituo vya nishati Kuwait

    .

    Mashambulizi ya ndege zisizokuwa na rubani yasababisha hasara kubwa katika vituo vya nishati Kuwait.

    Shirika la mafuta ya Petroli la Iran limesema kwamba baadhi ya vituo vyake vimelengwa katika mashambulizi ya ndege zisizokuwa na rubani za Iran, hali iliyosababisha moto mkubwa kutokea na uharibifu mkubwa kushuhudiwa.

    Kwa mujibu wa taarifa ya serikali ya Kuwait, makundi ya wahudumu wa dharura yanakabiliana na moto mkubwa kuudhibiti na kuzuia kusambaa, ila eneo ambalo moto huo unakabiliwa haukutajwa katika ujumbe huo uliochapishwa kwenye mtandao wa kijamii wa X.

    Hakuna majeruhi walioripotiwa katika shambulizi hilo, ambalo linefuatwa mashambulizi mengine yaliyotekelezwa katika maeneo mengine ya Ghuba, ikiwemo kituo cha mafuta na nishati huko Bahrain.

    Maelezo zaidi:

  3. Habari za hivi punde, Mtoto mmoja ni miongoni mwa waliouawa kwenye shambulizi la Israel, kusini mwa Lebanon

    .

    Chanzo cha picha, Reuters

    Wizara ya afya ya Lebanon, imesema kwamba watu saba, akiwemo mtoto mwenye umri wa miaka minne . Watu hao waliathirika katika shambulizi lililotekelezwa katika mji wa Lebanon, Kfar Hatta.

    Taarifa ya wizara ya afya ya Lebanon, ilichapishwa katika shirika la habari linalomilikiwa na serikali la NNA baada ya vyombo vya kibinafsi kuripoti kuwa mashambulizi yalitekelezwa usiku kucha.

  4. Giza la intaneti lazidi kushuhudiwa Iran

    .

    Chanzo cha picha, NetBlocks

    Kwa mujibu wa shirika la kutathmini shughuli za mitandao giza la mawasiliano ya intaneti inayoendelea huku hali hiyo kuingia siku yake ya 37 Jumapili hii.

    Kampuni ya Netblocks imesema kwamba ukosefu wa huduma za intaneti nchini Iran ndiyo iliyochukuwa muda mrefu zaidi duniani. Wakati huo huo BBC imefahamu kwamba baadhi ya maafisa wa serikali na wanaounga mkono serikali kwa pamoja na waandishiw a habari wana idhini ya kutumia intaneti kwa kiwango kidogo, huku wengine wengi wakitozwa ada ya juu zaidi kwa ajili ya kupata huduma hiyo.

    Wengine wanatumia huduma za satelaiti ili kupata mtandao wa intaneti kama vile starlink.

  5. Vita vya Iran vyasababisha bei ya maji na pombe kupanda India

    .

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Raia nchini India wanajiandaa kwa msimu wa joto kali, huku ikiropitiwa kwamba nyuzi joto zinatarajiwa kupanda 45 katika baadhi ya maeneo ya nchi hiyo.

    Lakini vita vya Iran tayari vimepandisha bei ya maji ya kunywa ya chupa kwa kiwango kikubwa.

    Sekta ya maji ya chupa ambayo inakadiriwa kuwa ya thamani ya dola bilioni sita za Kimarekani nchini India, imeripotiwa kuathirika pakubwa kutokana na vita hivyo vya Iran.

    Mwezi Machi, kampuni kubwa ya maji ya chupa nchini India ya Bisleri iliongeza bei ya bidhaa hiyo kwa asilimia 11 na kuuza dazani moja ya chupa za maji za lita moja kwa dola senti 26 za Kimarekani.

    Kampuni kama vile Bailley na Clear Premium Water pia zimeongeza bei ya maji hayo ya kunywa kulingana na ripoti ya shirika la habari la Reuters.

    Huku kampuni za maji ya chupa zikilalamikia athari ya vita kwa biashara zao, kampuni za kutengeneza pombe aina, pia zimeripoti kuongeza bei ya bidhaa hiyo.

    Muungano wa wafanyabishara wanaotengeza pombe nchini India umesema kwamba wateja wao wanapaswa kujiandaa kulipa bei ya juu zaidi ili kujiburudisha kwa 'bia baridi wanayoipenda.'

    Hii ni kwa sababu kampuni za kutengeza chupa za glasi ambazo huhifadhi bia na pombe ya aina nyingine, yamekosa kupata bidhaa muhimu zinazohitajika katika kutengeneza chupa hizo.

    Kwa mfano kampuni kama vile Vitrum Glass zimeamua kutumia mafuta kuchomea glasi zao ila bei ya juu ya bidhaa hiyo imepandisha gharama ya uzalishaji wa bidhaa hiyo.

    Serikali ya India imesema kwamba ina mafuta ya kutosha nchini ila katika baadhi ya hoteli na migahawa nchini humo, wafanyibiashara wameyafunga kutokana na uhaba wa bidhaa muhimu kama gesi ya kupikia. Uhaba wa mafuta pia umeathiri sekta ya kutengeneza vyombo vya udongo na mbolea, huku sekta ya usafiri wa ndege ikikumbwa na uhaba wa mafuta na bei ya juu ya bidhaa hiyo.

    Maelezo zaidi:

  6. Askofu Mkuu wa Kanisa la Kianglikana Duniani aombea amani Mashariki ya Kati

    Dame Sarah Mullaly

    Chanzo cha picha, PA Media

    Dame Sarah Mullaly anaongoza ibada yake ya kwanza ya Pasaka kama Askofu Mkuu wa Cantebury.

    Mfalme Charles, Mke wake Malkia Camilla, Mwanamfalme William na Mke wake Catherine Binti Mfalme wa Wales wanahudhuria ibada hiyo.

    Kiongozi huyo mpya, anaongoza ibada hiyo kwa mara ya kwanza tangu kuapishwa kama kiongozi wa kanisa la Kainglikana kufuatia kuondoka kwa mtangulizi wake.

    Katika ibada ya leo, Mullaly anatarajiwa kuiombea taifa la Uingereza lakini pia kuombea amani Mashariki ya Kati ambapo vita kati ya Marekani na Israel dhidi ya Iran vinaendelea na kusambaa katika mataifa jirani katika eneo hilo.

    Kiongozi huyo amezitaka mataifa za Ghuba na MAshariki ya Kati kupokea amani, kushuhudia haki ikitendeka kwao na uhuru ambao wameuhitaji kwa muda mrefu.

    '‘Ninaomba mfahamu kwamba Mungu atasimama nanyi wakati huu mgumu, ‘ amesema.

    Ibada hii ya Jumapili ya Pasaka, inafanyika wiki mbili baada ya Dame Mullaly kutawaza rasmi kama kiongozi wa kwanza wa kike kuiongoza kanisa la kianglikana. Kiongozi huyo ametaja uteuzi wake kama jambo la kihistoria ambalo hakulitegemea kufanyika hasa alipokuwa kijana mdogo.

    Maelfu ya watu wameripotiwa kuuawa kwenye mzozo unaoendelea tangu Februari 28, huku mashambulizi yakitekelezwa na Marekani na Israel huku Iran ikijibu mashambulizi hayo kwa kulenga kambi za kijeshi za Marekani na miundo mbinu kadhaa katika mataifa jirani ya Ghuba.

    Israel pia imetekeleza mashambulizi kadhaa kote Lebanon baada ya Kundi linaloungwa mkono na Iran – kutoka Lebanon la Hezbollah.

    Soma pia:

  7. DR Congo inajiandaa kuwapokea wahamiaji wa Marekani

    .

    Chanzo cha picha, AFP via Getty Images

    Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo imekiri kujadiliana na Marekani kuhusu mpango wa kuanza kuwapokea wahamiaji wa nchi ya tatu mwezi huu, huku ukandamizaji wa utawala wa Trump dhidi ya wahamiaji ukiendelea.

    Taarifa iliyotolewa na Wizara ya Mawasiliano inasema mfumo wa muda wa kuwapokea wahamiaji umeanzishwa, na maeneo ya kuwahifadhi wahamiaji tayari yametengwa karibu na mji mkuu Kinshasa.

    Taarifa hiyo hata hivyo haikutaja idadi ya wahamiaji wanaotarajiwa nchini.

    Mamlaka zinasisitiza kwamba uamuzi wa kukubali wahamiaji wa nchi ya tatu waliofurushwa nchini Marekani unalingana na dhamira ya serikali ya utu wa binadamu, mshikamano wa kimataifa na kulinda haki za wahamiaji.

    "Serikali itatoa msaada wa vifaa na wa kiufundi kwa ushirikiano na serikali ya Marekani," taarifa hiyo ilisema na kuongeza kuwa serikali ya DRC haitagharamia mpango huo.

    Hofu imeibuka kwamba wahamiaji hao huenda wakarejeshwa katika nchi zao, ambapo baadhi wanahofia kuteswa, lakini maafisa wa Kongo wanasema hakuna uhamisho kama huo unaopangwa.

    Serikali pia imesema mpango huo sio "utaratibu wa kudumu wa uhamishaji au utumiaji wa sera za uhamiaji."

    Nchi nyingine za Afrika kama vile Cameroon, Eswatini, na Ghana pia zimewapokea watu waliofukuzwa kutoka Marekani.

    Hatua hiyo imekosolewa, kwa sababu mikataba inaonekana kufanywa kisiri.

    DRC tayari inakabiliana na vitisho vya usalama mashariki mwa nchi, na utawala wa Trump umekuwa ukishinikiza kumalizwa kwa mzozo huo ili makubaliano ya amani kati ya maafisa wa Kongo na Rwanda yafikiwe, ingawa utekelezaji bado ni changamoto.

    Huku mzozo ukiwa bado unaendelea, haijafahamika ni vipi DR Congo inanuia kuangazia sera ya uhamiaji ya Marekani huku pia ikikabiliana na tishio la usalama, ambalo limezua mzozo mkubwa wa kibinadamu.

    Maelzo zaidi:

  8. Jeshi la Israel lashambulia mji wa Beirut huku ikikabiliana na Hezbollah

    .

    Chanzo cha picha, Reuters

    Moshi umeonekana ukifuka katika mtaa wa Ghobeiry, ambapo jeshi la Israel liliwaonya wakazi wake kuondoka kwani ni ‘'eneo linalohusishwa na Kundi la Hezbollah.’'

    Jeshi la Israel limesema kwamba limetekeleza mashambulizi mapya dhidi ya miundombinu inayomilikiwa na kundi la Hezbollah, jijini Beirut.

    Haya yanafanyika kufuatia onyo lililotolewa na jeshi hilo kwa raia ambao ni wakaazi wa mitaa kadhaa iliyopo kusini mwa mji huo, wakitakiwa kuondoka mara moja Jumapili asubuhi.

    Wakati huo huo, kundi hilo linaloungwa mkono na Iran, limesema kwamba limerusha makombora yaliyolenga upande wa Israel – japo jeshi la Israel limesema kwamba mfumo wake wa ulinzi wa angani umeyazuia makombora hayo.

    Kwa mujibu wa vyombo vya habari vya Israel, makabiliano hayo yalitokea saa chache baada ya Hezbollah kutangaza kuwa imeshambulia meli ya kijeshi ya Israel iliyopo kwenye Bahari inayopakana na pwani ya Lebanon.

    IDF imeviambia vyombo vya habari vya Israel kwamba haina taarifa zozote kuhusu shambulizi hilo la Hezbollah.

    Soma pia:

  9. Watu kadhaa wauawa katika mashambulizi kusini mwa Iran

    Gavana mmoja wa jimbo la kusini mwa Iran la Kohgiluyeh – Boyerahmad, amesema kwamba raia kadhaa wameuawa katika mashambulizi yaliyotekelezwa katika jimbo hilo.

    Kulingana na vyombo vya habari nchini Iran, Gavan awa Boyerahmad Abbas Basheti amesema kwamba watu watano wameuawa huku wengine wanane wakijeruhiwa kutokana na mashambulizi yaliyotekelezwa katika eneo la Kuh Siah lililopo katika jimbo hilo.

    Basheti ameielezea pia shirika la habari la serikali la IRNA kwamba maeneo mawili ya Kakana na Vezeg yaliyopo katika jimbo hilo pia yalishambuliwa usiku wa kuamkia Jumapili.

    Watu wawili waliuawa katika shambulizi la Kakana na wengine watatu kuuawa katika shambulizi la Vezeg kwa mujibu wa Besheti.

    Mapema Jumapili, Rais wa Marekani Donald Trump alichapisha ujumbe wa ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Truth Social, kwamba MArekani ilifanikiwa kutekeleza operesheni kali ya uokoaji wa kijeshi kwa ujasiri mkubwa na ambayo haijafanywa katika historia ya jeshi la Makerani.

    Lakini kulingana na msemaji wa jeshi la Iran, misheni ya Marekani ameitaja kama iliyofeli na wala haikufanikiwa.

    “Adui katika juhudi zake za kumuokoa mwanajeshi wake aliyepotea, hakufanikiwa na tunamshukuru Allah kwa baraka zake kwa kuisaidia jeshi la Iran ,’ alisema.

    Imeripotiwa kwamba makabiliano yalizuka kati ya wanajeshi wa Iran na Marekani wakati ambapo operesheni ya uokoaji kumtafuta mwanajeshi wa Marekani aliyepotea ilikuwa ikiendeela.

    Katika matangazo yake Jumapili hii, shirika la habari la Iran limefuata mtazamo wa jeshi la Iran ulionekana kudai kwamba Rais Trump alitoa madai tupu kuhusu uokoaji wa mwanajeshi aliyepotea ndani ya Iran, na kwamba ni mbinu ya kuzuia dunia kujuwa ukweli kuhusu Marekani kushindwa vitani.

  10. Uokoaji ulihusisha mamia ya wanajeshi na makumi ya ndege za kivita

    .

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Sasa imebainika uokoaji wa rubani wa Marekani nchini Iran ilikuwa operesheni ngumu sana iliyohusisha rasilimali muhimu za kijeshi, na mamia ya wafanyikazi wa vikosi maalum, ndege kadhaa za kivita na helikopta zilizopewa jukumu la kumtafuta.

    Kituo cha habari cha CBS kiinaeleza jinsi ndege, Afisa wa Mifumo ya Silaha (WSO) ambaye anaketi kwenye kiti cha pili cha ndege ya kivita aina ya F-15E Strike Eagle, alijvyoeruhiwa wakati wa mchakato wa kumtoa kwenye ndege hiyo kusini mwa Iran.

    Ndege iliyoanguka ilikuwa ya kwanza F-15E Strike Eagle kudunguliwa katika mapigano katika zaidi ya miaka 20.

    "Wizzo", Kanali ambaye jina lake halijatajwa, alipata majeraha kadhaa lakini inasemekana aliweza kuondoka na kukwepa kukamatwa kwa zaidi ya siku moja. Alikuwa na bunduki tu.

    Maelezo zaidi:

  11. Rubani wa Marekani aliyetoweka kwenye ndege iliyodunguliwa Iran ameokolewa - Trump

    .

    Chanzo cha picha, US Air Force via Getty Images

    "TUMEMPATA!"

    Hivi ndivyo Donald Trump alivyoanza chapisho lake la mtandao wa kijamii akitangaza kuokolewa kwa rubani wa pili wa nMarekani.

    Trump anadai hatua hiyo kama ushindi mkubwa kwa jeshi la Marekani, na kugeuza ktukio ambalo lilizua hofu kuwa sababu ya kusherehekea.

    Kwa muda wa saa 48, alikuwa amekabiliwa na kibarua kigumu cha kumuokoa rubani wa ndege ya kivita ya Marekani, ambaye sasa tunafahamishwa alikuwa kanali, alikamatwa na Iran na uwezekano mkubwa kuonyeshwa kwenye televisheni ya serikali.

    Majukwaa ya mitandao ya kijamii yanayoiunga mkono Irani hapo awali zilichukua fursa ya tukio hilo kuelezea kinachofanyika Iran.

    Baadhi walichapisha video ya rubani huyo akifukuzwa na wenyeji, huku wengine wakiweka mtandaoni picha za Akili Mnemba za afisa huyo akifurahia ukarimu wa Iran.

    Msemaji wa Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu alikuwa ameiita siku ya "kufedhehesha" kwa Marekani.

    Soma pia:

  12. Karibu katika matangazo ya moja kwa moja leo Jumapili 05.04.2026