Vita vya Israel, Marekani na Iran: Mafuta na gesi vimekuwa silaha ya vita

l

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha, Kiwanda cha gesi pwani ya South Pars
    • Author, Alexey Kalmykov
    • Nafasi, BBC
  • Muda wa kusoma: Dakika 4

Iran imeshambulia vituo vya mafuta na gesi nchini Saudi Arabia, Qatar na Falme za Kiarabu kujibu shambulio la Israeli dhidi ya vituo vyake vikubwa zaidi vya gesi duniani.

Tangu vita kuanza, Iran imeonyesha kuwa iko tayari kufanya mashambulizi hadi kiwango ambacho kinaweza kusababisha mgogoro mkubwa wa nishati duniani.

Vita na Iran vimekuwa vikiendelea kwa wiki tatu, lakini hakuna upande wowote ambao umetumia mbinu ya kuharibu miundombinu ya mafuta na gesi. Hali hii imeifaa Iran, kwa sababu imeweza kutumia sekta ili kunusurika na hata kusaka ushindi katika mapambano na wapinzani wenye nguvu zaidi.

Hadi sasa, Iran imeipiku Marekani katika vita vya nishati: Kwa kufunga Mlango wa Bahari wa Hormuz, mataifa ya Ghuba yamenyimwa mauzo ya nje ya mafuta na gesi asilia, lakini Iran inaendelea kuuza nje mafuta na kupata pesa kutokana na kuiuzia China, hali ambayo hata meli za Marekani hazijaweza kuizuia.

Bei ya mafuta pia inaongezeka, kwani dunia imepoteza takriban asilimia 20 ya usambazaji wake wa gesi asilia na zaidi ya asilimia 10 ya jumla ya uzalishaji wa mafuta.

Iran imetumia ndege zisizo na rubani mara kwa mara katika wiki za hivi karibuni kushambulia vituo na viwanda vya UAE, Qatar, Kuwait, Iraq na Saudi Arabia, lakini lengo la mashambulizi haya sio kuviangamiza bali ni kuunda hofu na kuvilazimisha kusimamisha uzalishaji na usafirishaji kwa sababu za tahadhari.

Vituo vya mafuta na gesi ni shabaha rahisi ya makombora na ndege zisizo na rubani, na Iran imeonyesha tangu mwaka 2019 kwamba ina uwezo wa kusababisha uharibifu mkubwa katika vituo hivyo.

Marekani pia imejiwekea kikomo kwa kufanya mashambulizi machache na ya tahadhari katika eneo la mafuta la Iran, katika Kisiwa cha Kharg. Asilimia 90 ya mafuta ya Iran yanasafirishwa nje kupitia Kisiwa cha Kharg.

Donald Trump aliamuru vituo vya kijeshi pekee ndio vipigwe mabomu na miundombinu ya mafuta ya kisiwa hicho isishambuliwe, lakini alionya kwamba anaweza kubadilisha mawazo yake wakati wowote.

Richard Nephew, naibu mwakilishi maalum wa zamani wa Iran katika Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani, anaamini kujizuia kwa Iran kunaonyesha imani ya nchi hiyo katika uwezo wake.

Anasema: "Imani ya viongozi wa Iran inaonyesha kwamba wamejiandaa kukabiliana na mgogoro huu kwa wiki, miezi, na hata miaka ijayo, na kwa sababu hii, kwa sasa hawako tayari kuighadhabisha Marekani kwa kuharibu nishati ya mafuta na gesi katika Ghuba ya Uajemi."

"Lakini kuna hatari ya kutoke tukio la janga, au hesabu isiyo sahih na matukio ya Jumatano yanaweza kuangukia katika kundi hili.

Nini kilitokea?

l

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Uharibifu uliosababishwa na ndege isiyo na rubani ya Iran iliyoanguka katika eneo la mafuta la Fujairah katika Falme za Kiarabu, Machi 14
Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Iran ilitangaza kwamba kwa mara ya kwanza tangu kuanza kwa vita, vituo vyake vya mafuta na gesi vilishambuliwa, shambulio ambalo lililipua eneo kubwa zaidi la gesi duniani, South Pars katika Ghuba ya Uajemi.

South Pars inadhibitiwa na Iran, huku sehemu ya kaskazini ikiwa ya Qatar, mzalishaji mkuu wa gesi katika eneo hilo. Qatar hutoa takriban asilimia 20 ya gesi asilia duniani, lakini vita vilipoanza, ilifunga kiwanda chake kikubwa huko Ras Laffan, na kusababisha bei ya gesi kupanda barani Ulaya na Asia.

Kwa Iran, kiwanda cha gesi cha South Pars kwa sasa si muhimu sana kuliko mafuta, kwa sababu mafuta husafirishwa zaidi nje ya nchi, lakini gesi hutumika zaidi ndani ya nchi na kidogo tu husafirishwa kwenda Iraq.

Kufuatia shambulio hilo, Iran ilitishia kulenga kituo cha Ras Laffan cha Qatar, na hilo litasababisha uharibifu mkubwa na usumbufu wa muda mrefu katika soko la gesi duniani. Iran pia imeionya Saudi Arabia kuhamisha mafuta yake katika viwanda vyake vikubwa viwili na kutoa onyo kama hilo kwa UAE kuhusu gesi yake.

Shambulio la kwanza la Israel dhidi ya miundombinu ya mafuta na gesi ya Iran lilikosolewa vikali na Qatar, huku maafisa wakielezea kuwa ni "hatua hatari."

Wizara ya Mambo ya Nje ya Qatar imesema: "Mashambulizi dhidi ya miundombinu ya nishati ni tishio kwa usalama wa nishati duniani na pia yanahatarisha wakazi wa eneo hilo na mazingira.”