Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Mazingira: Bendi ya Fulu yatunza mazingira kwa kubadilisha takataka kuwa vifaa vya muziki
Je! Umewahi kufikiria kusikiliza bendi iliyo na vyombo vinavyotengenezwa kutoka na takataka? Mjini Kinshasa kuna bendi ya muziki ambayo huitwa fulu muziki au muziki wa takataka.
Bendi hiyo hainunui vyombo vya muziki lakini inatengeneza yenyewe vyombo vyake
Wao hutumia vitu mbali mbali walivyookota kutoka kwenye taka, sio tu kwa nia ya kuburudisha, watumbuizaji hao wamekua wakichangia katika kutunza mazingira.
Mwandishi wa BBC Kinshasa Mbelechi Msoshi alikutana nao.
Kwanza huchakura taka na kuchukua vipande vya,chupa,mabomba yaliyoharibika,na vitu vingine ambavyo vinaweza kuzalisha sauti nzuri ya muziki,bendi hio ya mziki inafahamika kama fulu, ikiamanisha mziki wa taka taka. Baada ya kuvicheza vipande vilivyopatikana kwenye taka, sauti nzuri hupatikana.
Pisco Crane ni jina lake la usanii na jina lake rasmi ni Ewango Mabende, yeye ni Kiongozi wa bendi hiyo iliyoanza mwaka 2016.
Lengo kuu ni kupambana na uchafuzi ya mazingira, kupitia mziki wake ,vile vile alitaka kuhamasisha serikali na raia kuhusu kuondokana na takataka nyingi ambazo zimejaa ndani ya mji mkuu wa Kinshasa na zinazoweza kusababisha mangojwa.
"Watu ambao wanatupa taka kando ya makazi ya raia wanashindwa kuondoa uchafu huo, na katika pita pita zangu,nikaona ya kwamba kuna namna ya kuchangia ili kujaribu kupunguza uchafu mjini,wakati naona kitu Fulani ambacho naweza kuchukua na kukipa thamani tena; mfano mzuri ni sisi watu ambao tunaishi karibu na taka hizo tunapata magonjwa yanyotokana na mrundikano wa takataka .Taka ni kitu kibaya sana katika mazingira''.
Aisha ni msichana pekee kati bendi hio .Anasema ''Tuna leta mziki mpya wa mitaa, sisi ni waasanii, hatuwezi baki katika muziki ambao unazungumzia tu masuala ya ngono inabidi kuleta mabadiliko,kuelimisha watu pia kuhusu mazingira,hususani watoto wajue kulinda mazingira. Mimi nilijiunga na bendi hii wakati niliposikia mziki wao unaweza kubadilisha ulimwengu na wala sio tu Kinshasa.''
Kuna vitu havikuwa ndani ya muziki wao, lakini fulu music imeleta mambo mapya.
Watu walifikiri mzaha, hawakuamni kuwa bendi hii imepata umaarufu mkubwa leo.
Matumaini ya piscro crane ni kuona mziki wake unakubalika duniani kote.