Afya: Fahamu kwanini hufai kupuuza saratani ya umio

Ni sababu ya sita kwa vifo vya saratani kote duniani, Lakini watu wengi hawana habari wanaugia ugonjwa huo.

Saratani ya umio - aina hii ya saratani haionyeshi dalili zozote mwanzoni.

Mwanasoka wa zamani wa Uskochi, Andy Goram, ambaye alihudumu kama mlinda lango na mchezaji wa vilabu tofauti huko Scotland na Uingereza, hivi karibuni alifichua kwamba anaugua saratani ya umio.

Taarifa hiyo iliwafadhaisha wafuatiliaji wake kwani Goram, 58, alisema amepewa miezi sita kuishi.

Katika mahojiano na, mchezaji kandanda huyo wa zamani alielezea kwamba mara ya kwanza alijihisi kuwa mgonjwa karibu wiki saba zilizopiya wakati alipokuwa na matatizo ya kula na kunywa.

Lakini alipuuza kiungulia alichoshuhudia baada ya kushindwa kupata miadi na daktari wake.

Sawa wana Goram, wagonjwa wengi waliouguzwa saratani ya umio wameelezea jinsi ugonjwa huo unavyojitokeza bila dalili zozote au alili ambazo zinaweza kpuuzwa kirahisi.

"Nilimpuza kama kila mtu"

Paul Sinclair, kutoka eneo la Fife, Scotland, aliambia BBC kwamba alianza kujihisi kana kwamba "ana gesi kwenye sehemu ya chini ya mbavu" mnamo Septemba 2020. Sinclair pia alijihisi kana kwamba "amekula kupita kiasi". katika mkao mmoja."

"Nilimpuuza kama kila mtu mwingine," anasema. "Nilidhani alikuwa na gesi. Alikuwa akila vizuri, hakuwa na maumivu."

"Ilikuwa ni maumivu chini ya mbavu zangu. Iliendelea kwa takriban wiki moja na nusu ndipo nikaonelea, 'Nitafute ushauri kuhusiana na hali hii.'

"Nilienda kwa daktari na moja kwa moja kwa uchunguzi wa endoskopi. Hiyo ilithibitisha kuwa nilikuwa na uvimbe kwenye tumbo langu la juu.

Sinclair alifanyiwa tiba ya chemotherapy kwa wiki nane kbal ya kusitisha tiba hiyo kwa wiki sita.

Alafu akafanyiwa upasuaji wa saa 11, ambayo pia ilijumuisha kutolewa kwa wengu lake. Baada ya hapo "alirejelea tiba ya chemotherapy" tena.

"Nilikuwa mgonjwa sana baada ya kufanyikwa awamu mbili za chemotherapy," alielezea. "Ya pili ilikuwa mbaya zaidi kwa sababu tayari nilikuwa dhaifu baada ya kufanyiwa upasuaji."

"Kadri unapoendelea kupona, unaanza kujifunza kula tena, kutafuna chakula vizuri, kula chakula kidogo kidogo mara saa tofauti kwa siku."

Sasa, miaka mitatu baadaye, Sinclair anaweza kufanya mazoezi mepesi, lakini mambo hayatakuwa "kawaida kabisa."

"Lazima uwe na mtazamo chanya na kushukuru kila siku unapoamka," anasema.

"Jambo muhimu zaidi ni kwamba sikuwa na dalili mbaya sana, lakini ni muhimu sana usizipuuze na ujiangalie mwenyewe."

Dalili ya saratani ya umio

Umio ni mrija mrefu ambao hubeba chakula kutoka koo hadi tumboni. Dalili kuu za saratani ni:

Kuwa na shida ya kumeza (dysphagia)

Kuwa na ukojihisi kuwa na kichefu chefu

Kupata kiungulia

Dalili za kuvimbiwa, kama vili uteuka sana

Dalili zingine ni pamoja na:

Kikohozi kisichoisha

Sauti ya mkwaruzo

Kupoteza hamu ya kula au uzani wa mwili bila kujaribu kufanya hivyo

Kujihisi kuchoka

Uchungu kwenye koo au sehemu ya kati ya kifua, hasa wakati unapomeza

Chanzoo: NHS (Huduma ya kitaifa ya Afya Uingereza)

"Huwezi kupona kabisa"

Linda Moffat, ambaye pia anaishi Scotland, alijichukulia kuwa mwanamke mwenye nguvu imara akiwa na miaka 48, alikuwa akiendesha farasi kila siku.

Lakini Disemba 2014, alianza kupata shida ya "kumeza chakula, kilikuwa kinakwama," alikumbuka. "Uchungu uliongezeka kadri chakula kilivyonisakama."

" Ilibidi nijitapishe ili kukitoa. Nilidhani nina kidonda cha tumbo. Sikutilia maanani nilidhanini ni tatizo kidogo."

Baada ya muda, anasema "alipata ujasiri wa kuzungumza na daktari" na akaagizwa dawa za kupunguza asidi. Lakini dalili ziliendelea hadi akashauriwa kufanyiwa uchunguzi zaidi.

Uchunguzi ambao ulibaini "ana uvimbe ambao uliokomaa" kwenye umio na ikawa "mwanzo wa safari ndefu ya maumivu," alielezea.

"Ni saratani kali sana na upasuaji wake ni wa kikatili sana: saa nane kwenye chumba cha upasuaji," alisema. "Unapata tiba ya kemikali kabla na baada. Ni lazima ujifunze kula tena."

"Na una matatizo mengi ya kutapika, kuhara na maumivu. Nadhani hutapona kabisa."

"Nina bahati sana. Saratani yangu ilikuwa imeendelea sana na nilikuwa na nafasi ya 20% tu ya kuishi," anasema.

"Lakini imekuwa karibu miaka saba na nina furaha sana kuwa hai na ninashukuru sana kila mtu aliyenisaidia kuwa hapa."

"Ugonjwa huu mara nyingi huitwa ' the silent killer ' kwa sababu dalili hutofautiana sana," anaongeza. "Omba tu kwamba watu waende kwa daktari haraka vya kutosha."