Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Tetesi za soka Ulaya Ijumaa: Rogers, kuondoka Aston Villa huku Chelsea, Liverpool, Arsenal na Man United zikimtaka
Morgan Rogers, 23, atakuwa tayari kuondoka Aston Villa msimu huu - huku Chelsea, Liverpool, Arsenal na Manchester United zikiwa katika mchanganyiko wa kumsajili kiungo huyo wa kati wa Uingereza. (Sun).
RB Leipzig wameweka bei ya pauni milioni 87 kwa winga wa Ivory Coast Yan Diomande, 18, ambaye analengwa na Liverpool na Manchester United. (Sky Sports),
Saudi Pro League inaongeza kasi ya kumsaka mshambuliaji wa Liverpool na Misri Mohamed Salah, 33, na inazidi kuwa na uhakika wa kupata makubaliano kabla ya Kombe la Dunia msimu huu. (TeamTalks)
Everton wanazidi kujiamini kuwa winga wa Manchester City na England aliye kwa mkopo Jack Grealish, 30, atarejea katika klabu hiyo msimu ujao. (Daily Mail),
Manchester City, Paris St-Germain na Arsenal wote wanavutiwa na mchezaji wa kimataifa wa Uhispania Dani Olmo, 27, huku Barcelona wakiwa tayari kumuuza kiungo huyo mshambuliaji. (Fichajes - In Spanish),
Atletico Madrid wanakaribia kumnunua kiungo wa kati wa Brazil na Atalanta Ederson, 26, ambaye pia anavutiwa na Manchester United na Manchester City. (Fabrizio Romano)
Meneja wa Manchester City Pep Guardiola hatofanya uamuzi kuhusu mustakabali wake katika klabu hiyo hadi mwisho wa msimu huu. (Telegraph - Subscription Required)
Manchester United itatafuta kuongeza viungo wawili wapya wa kati kwenye kikosi chao msimu huu, huku Waingereza Elliot Anderson, 23, wa Nottingham Forest na Adam Wharton wa Crystal Palace, 22, pamoja na kiungo wa kati wa Newcastle United na Italia Sandro Tonali, 25, wakizingatiwa. (Givemesport)
Arsenal bado wana nia ya kumsajili beki wa Real Madrid Mhispania mwenye umri wa miaka 19 Victor Valdepenas mwishoni mwa msimu huu lakini watakabiliwa na ushindani kutoka kwa AC Milan. (Caughtoffside)
Kiungo wa kati wa Ureno Bernardo Silva ataondoka Manchester City kama mchezaji huru mkataba wake utakapokamilika mwezi Juni, huku mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 31 tayari akiwa ameshatathmini chaguo lake. (Fabrizio Romano)
Barcelona wana mpango wa kumsajili fowadi wa Borussia Dortmund na Ujerumani Karim Adeyemi, 24, msimu huu. (Fichajes - In Spanish)
Mshambuliaji wa Uholanzi na West Ham Crysencio Summerville, 24, anafuatiliwa na Aston Villa, Everton, Tottenham, Marseille na Napoli. (TeamTalks)
Crystal Palace wanaaminika kuhamia kwenye malengo mengine ya usimamizi, kwani meneja wa Bournemouth Andoni Iraola, 43, hana uwezekano wa kuhama kwenda Selhurst Park. (Sky Sports)