Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.

Bofya kuelekea tovuti kuu

Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data

Moja kwa moja, Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kupigia kura azimio la kufikia Mlango - Bahari wa Hormuz

China, ambayo ina kura ya turufu, inapinga mpango wowote wa kutumia nguvu.

Muhtasari

Moja kwa moja

Na Ambia Hirsi

  1. Vita vya Iran: Bei ya mafuta yatarajiwa kupanda Kenya

    Wakenya wametahadharishwa kuwa bei ya mafuta huenda ikapanda, huku athari za vita vinavyoendelea Mashariki ya Kati zikianza kushuhudiwa.

    Bei ya bidhaa hiyo muhimu duniani imekuwa ikipanda, na serikali sasa haina budi kushughulikia hali hiyo alisema Waziri wa Fedha John Mbadi.

    Kuanzia katikati ya mwezi Aprili, bei ya mafuta huenda ikakabiliwa na shinikizo kuongezaka. Hata hivyo, waziri Mbadi anasema mabilioni ya fedha zitatumika kupunguza atharu ya kupanda kwa bei ya mafuta kwa watumiaji, lakini kwa muda mfupi tu.

    "Mzunguko wa sasa wa bei ya mafuta, Machi 15, 2026, hadi Aprili 14, 2026, hauwezi kuathiriwa kwa vile bidhaa husika ilitolewa kabla ya mzozo wa Mashariki ya Kati," alisema Mbadi.

    Serikali, hata hivyo, inasema kuwa takriban Ksh.17 bilioni zinazoshikiliwa kwa sasa katika hazina ya uimarishaji chini ya Ushuru wa Maendeleo ya Petroli zitatumwa ili kudhibiti bei na kuwakinga watumiaji kutokana na ongezeko kubwa kwa muda wa miezi mitatu ijayo.

    Serikali pia inafikiria kusitisha utozaji wa ushuru wa ziada (VAT) wa mafuta, kama hatua ya kudhibiti bei ya ya bidhaa hiyo.

    Pia unaweza kusoma:

  2. Wakenya 16 hawajulikani waliko baada ya kujiunga na jeshi la Urusi

    Wakenya 16 wametoweka nchini Urusi baada ya kujiunga na jeshi la nchi hiyo, na wengine 47 wamerejea nyumbani kutoka vitani nchini Ukraine, Waziri wa Mambo ya Nje wa Kenya Musalia Mudavadi ameimbia kikao cha kamati ya Bunge la Seneti.

    Wengine 38 kwa sasa wako katika hospitali tofauti za Urusi chini ya vizuizi vya ufikiaji Mudavadi aliongeza kusema.

    Idadi ya Wakenya waliotoweka nchini Urusi imeongezeka kutoka 10 hadi 16 ndani ya saa 24 zilizopita.

    Bado haijabainika ikiwa wamefariki au wako hai.

    Waziri huyo pia alikadiria kuwa Wakenya 165 wanashiriki kikamilifu katika operesheni za kijeshi, na kufanya jumla ya walioshiriki katika mzozo wa Ukraine kufikia zaidi ya 250.

    Mudavadi alisema idadi hiyo huenda ikawa kubwa zaidi.

    Aliongeza kuwa Wakenya wawili wanazuiliwa nchini Ukraine kama wafungwa wa kivita.

    Mudavadi pi alisema walioajiriwa wametia saini kandarasi za kuhudumu kama maafisa wa usafirishaji au kufanya majukumu ya kivita.

    "Kinyume na ripoti zilizopo, Wakenya wengi walijiunga na jeshi la Urusi kwa hiari," Mudavadi aliambia kamati ya wabunge.

    Baadhi ya mashirika yenye makao makuu nchini Kenya, Urusi, Qatar na Umoja wa Falme za Kiarabu yalihusika na usajili huo, kwa mujibu wa waziri Mudavadi.

    Kenya imeanzisha uchunguzi kuhusu usajiliwa kwa raia wake kupigana vita nchini Ukraine kinyume cha sheria.

    Soma zaidi:

  3. Waziri wa Ulinzi Pete Hegseth amtaka Mkuu wa Majeshi kuachia ngazi

    Waziri wa Ulinzi wa Marekani Pete Hegseth amemtaka Mkuu wa Majeshi Randy George kuachia wadhifa wake, kulingana na CBS News, mshirika wa habari BBC wa Marekani.

    Msemaji Mkuu wa Pentagon Sean Parnell alisema katika taarifa yake kwenye mitandao ya kijamii kwamba George "atastaafu kutoka wadhifa wake kama Mkuu wa 41 wa Wanajeshi mara moja".

    Mkuu wa Jeshi kawaida huhudumu kwa kipindi cha miaka minne.

    George, afisa wa kijeshi ambaye alihitimu kutoka chuo cha kijeshi cha West Point, aliteuliwa kwa jukumu hilo mnamo 2023 na Rais wa zamani Joe Biden.

    Mabadiliko ya hivi punde yanakuja baada ya Trump kusema katika hotuba yake kwa taifa kwamba vita vya Marekani na Israel dhidi ya Iran vinatarajiwa kumalizika "hivi karibuni".

    George aliwahi kuwa afisa wa jeshi katika Vita vya kwanza vya Ghuba na katika migogoro ya hivi majuzi nchini Iraq na Afghanistan.

    Haijabainika kwa nini alitakiwa kuondoka. "Tunashukuru kwa utumishi wake, lakini ulikuwa wakati wa mabadiliko ya uongozi katika Jeshi," afisa mkuu wa ulinzi ambaye hakutajwa jina aliiambia CBS.

    Msemaji wa Pentagon Parnell alisema: "Idara ya Vita inashukuru kwa miongo kadhaa ya utumishi wa Jenerali George kwa taifa letu. Tunamtakia kila la heri anapostaafu."

    Nafasi yake itachukuliwa na Makamu Mkuu wa Jeshi Jenerali Christopher LaNeve ambaye atakuwa kaimu mkuu wa majeshi, kulingana na vyombo vya habari vya Marekani.

    Soma pia:

  4. Kushambulia miundo mbinu ya raia hakutaifanya Iran kusalimu amri - Araghchi

    Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Abbas Araghchi amesema kulengwa kwa daraja la B1 kwenye barabara kuu ya Tehran-Kaskazini hakutaifanya nchi hiyo kusalimu amri.

    Bwana Araghchi aliandika kwenye Mtandao wa X: "Kulenga miundombinu ya kiraia, ikiwa ni pamoja na madaraja ambayo ujenzi wake bado unaendelea, kamwe hakutawashinikiza Wairani kusalimu amri... Kila daraja na kila jengo litajengwa upya kwa ustadi zaidi; lakini jambo ambalo kamwe halitarekebishwa ni uharibifu unaofanywa kwa na Marekani."

    Saa kadhaa zilizopita, Donald Trump alichapisha video ya shambulio la Marekani dhidi ya daraja hilo kwenye mtandao wake wa kijamii, akiandika: "Ni wakati wa Iran kufikia makubaliano kabla ya muda kuwapa kisogo na kuiacha nchi ikiwa imesambaratika."

    Maelezo zaidi:

  5. Marekani yashambulia daraja kuu la Iran

    Rais wa Marekani Donald Trump ametangaza kushambiliwa kwa daraja la B1 la Iran, iliyojengwa hivi karibuni ambayo ilikuwa inaunganisha mji wa Karaj na mji mkuu Tehran.

    Trump aliongeza: "Tuliripua madaraja yao makuu matatu jana usiku. Yanaharibiwa ..."

    Video inaonyesha moto na moshi ukifuka juu ya daraja hilo, nasehemu ya katikati ikiwa imeachana.

    Watu wanane wameripotiwa kuuawa na wengine 100 kujeruhiwa katika shambulio hilo

    Daraja la B1, ambalo halikuwa halijaanza kutumika linatajwa kuwa mojawapo ya madaraja marefu zaidi katika Mashariki ya Kati. Lina urefu wa mita 1,050 na nguzo zenye urefu wa mita 136, kulingana na ripoti ya vyombo vya habari vya serikali ya Iran.

    Pia unaweza kusoma:

  6. Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kupigia kura rasimu ya azimio kuhusu Mlango- Bahari wa Hormuz

    Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa leo linatarajiwa kupigia kura rasimu ya azimio lililowasilishwa na Bahrain kuhusu kulinda meli za kibiashara ndani na karibu na Mlango-Bahari wa Hormuz.

    China, ambayo ina nguvu ya kura ya turufu, inapinga mpango wowote wa kutumia nguvu.

    Bei ya mafuta imepanda kwa kasi tangu Marekani na Israel zilipoanzisha mashambulizi dhidi ya Iran mwishoni mwa mwezi Februari, na hivyo kuzua mzozo ambao sasa umedumu kwa zaidi ya mwezi mmoja na kusababisha kufungwa kwa Mlango wa Bahari wa Hormuz.

    Wanadiplomasia wanasema Bahrain, ambayo kwa sasa ni mwenyekiti wa Baraza hilo la Usalama lenye nchi wanachama 15, imekamilisha rasimu ya azimio linaloidhinisha matumizi ya "njia zote muhimu za kujihami" kulinda meli za kibiashara kwa mujibu wa shirika la habari la Reuters.

    Waziri wa Mambo ya Nje wa Bahrain Abdullatif bin Rashid Al Zayani aliiambia baraza hilo, "Tunatazamia kupata msimamo mmoja kutoka kwa baraza hili tukufu wakati upigaji kura utakaofanyika kesho Ijumaa, kuhusu rasimu ya azimio hilo" Mungu akipenda.

    Hapo awali Bahrain ilikuwa imeondoa pendekezo la utekelezaji wa sheria katika jaribio la kuzuia pingamizi kutoka kwa nchi zingine, haswa Urusi na China.

    Rasimu ya azimio inaidhinisha kuchukuliwa kwa hatua hizi "kwa muda wa angalau miezi sita ... na hadi Baraza litakapoamua vinginevyo."

    Hata hivyo, Fu Cong, mwakilishi wa China katika Umoja wa Mataifa, aliweka wazi katika hotuba yake kwa Baraza la Usalama kwamba Beijing inapinga kuidhinisha nchi wanachama kutumia nguvu.

    Maelezo zaidi:

  7. Natumai hujambo.