Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Jinsi wanyama wanavyogundua majanga hata kabla yatokee
Kwa miaka mingi watu kote ulimwenguni wameripoti tabia za kutisha za wanyama wakati wa majanga ya asili. Je, ishara hizi zinaweza kutumiwa kutuonya juu ya majanga yanayokuja?
Mnamo mwaka wa 2004, tsunami iliyosababishwa na tetemeko la ardhi lenye ukubwa wa 9.1 katika vipimo vya Richter karibu na Indonesia iliangamiza jamii za pwani karibu na Bahari ya Hindi, na kuua watu wasiopungua 225,000 katika nchi kadhaa.
Idadi kubwa ya vifo ilisababishwa na kile kwamba jamii nyingi hazikupokea onyo.
Mifumo ya tahadhari ya mapema iliyotengenezwa na mwanadamu, kama vile vitambuzi vya mawimbi na tetemeko la ardhi, ilishindwa kutoa tahadhari yoyote iliyo wazi. Maeneo mengi ya pwani yalikosa mifumo ya onyo ya ving'ora vya tsunami.
Mawasiliano yasiyo ya kawaida pia yalishindwa kutoa maonyo, huku ujumbe mwingi ukishindwa kufika kwenye simu za rununu katika maeneo hatarishi au kutosomwa.
Hata hivyo katika dakika na saa chache kabla ya kuta za maji yenye urefu wa mita 9 (futi 30) kubomoa maeneo ya ufuo, baadhi ya wanyama walionekana kuhisi hatari iliyokuwa karibu na kufanya jitihada za kukimbia. Kulingana na masimulizi ya watu waliojionea, tembo walikimbilia maeneo ya juu, flamingo waliacha maeneo ya viota vya chini, na mbwa walikataa kwenda nje.
Katika kijiji cha pwani cha Bang Koey nchini Thailand, wenyeji waliripoti kundi la nyati kando ya ufuo huo wakitazama baharini, kisha wakakanyagana wakipanda hadi kilele cha mlima uliokuwa karibu dakika chache kabla ya tsunami kupiga.
"Walionusurika pia waliripoti kuona wanyama, kama vile ng'ombe, mbuzi, paka na ndege, wakihama ndani zaidi ardhini muda mfupi baada ya tetemeko la ardhi na kabla ya tsunami kuja," anasema Irina Rafliana, ambaye awali alikuwa sehemu ya kikundi cha ushauri cha Umoja wa Mataifa kuhusu majanga (UNISDR) ambaye sasa ni mtafiti katika Taasisi ya Maendeleo ya Ujerumani huko Bonn. "Wengi wa wale walionusurika walikimbia pamoja na wanyama hawa au baada ya muda mfupi."
Rafliana anasimulia hadithi kama hizo zinazohusiana na kazi yake kuhusu majanga mengine, kama vile tsunami ya mwaka 2010 iliyosababishwa na tetemeko la ardhi chini ya bahari karibu na Sumatra, ambayo iliua karibu watu 500 kwenye visiwa vya Mentawai.
Hapa pia, baadhi ya wanyama, kama vile tembo, waliripotiwa kuonyesha tabia kana kwamba walikuwa na aina fulani ya ufahamu wa mapema wa tukio hilo. Siku chache zilizotanguliwa, kasa aliyekuwa ameachiliwa aligeuka na kurudi ghafla siku mbili kabla ya mlipuko wa volkeno ya Januari huko Tonga.
Mifumo ya tahadhari ya mapema haipo katika maeneo mengi yanayokumbwa na majanga ya asili mara kwa mara. Mnamo mwaka wa 2017, Shirika la Hali ya Hewa Ulimwenguni liligundua kuwa serikali za karibu nchi 100 bado hazina mifumo ya tahadhari ya mapema ya majanga ya asili ambayo yalikuwa yanawakabili.
Lakini masimulizi haya kuhusu tabia za wanyama kabla ya majanga yamewachochea watafiti wengine kuzingatia nadharia ya kwamba wanyama wanaweza kuwa na mifumo ya ndani ambayo inawatahadharisha kuhusu majanga ya asili yanayokuja. Inazua swali, je, wanyama wanaweza kutoa mifumo ya asili ya maonyo ya mapema kwa wanadamu?
Moja ya uchunguzi muhimu zaidi kuhusu jinsi wanyama wanageweza kutabiri majanga ulifanywa miaka mitano iliyopita na timu inayoongozwa na Martin Wikelski kutoka Taasisi ya Max Planck ya Tabia ya Wanyama nchini Ujerumani.
Utafiti huo ulihusisha kurekodi mienendo ya wanyama tofauti kama (ng'ombe, kondoo na mbwa) - mchakato unaojulikana kama biologging - kwenye shamba katika eneo linalokumbwa na mitetemeko ya ardhi la Marches katikati mwa Italia. Vifaa viliunganishwa kwa kila mnyama, ambavyov ilituma data ya harakati kwa kompyuta kuu kila dakika chache kati ya Oktoba 2016 na Aprili 2017.
Katika kipindi hiki, takwimu rasmi zilirekodi zaidi ya matetemeko 18,000 katika eneo hilo, kutoka kwa mitetemeko midogo ya ukubwa wa 0.4 katika vipimo vya Ritcher hadi zaidi ya mitetemeko 10 ya 4 au zaidi - ikijumuisha tetemeko kubwa la ardhi la Norcia lenye ukubwa wa 6.6.
Watafiti walipata ushahidi kwamba wanyama hao walianza kubadili tabia zao hadi saa 20 kabla ya tetemeko la ardhi. Wakati wowote wanyama waliofuatiliwa walipokuwa na shughuli kwa asilimia 50 zaidi kwa zaidi ya dakika 45, watafiti walitabiri tetemeko la ardhi lenye ukubwa wa juu ya 4.0. Mitetemeko saba kati ya nane ya nguvu ilitabiriwa kwa njia hii.
Huko Amerika Kusini, mwanaikolojia wa tabia Rachel Grant amepata matokeo sawa. Alifanya utafiti wa biologging ya wanyama wanaotembea kwa kutumia kamera zinazoendeshwa na mienendo ya wanyama ndani ya Hifadhi ya Kitaifa ya Yanachaga katika milimo ya Andes nchini Peru kwa muda uliojumuisha tetemeko la ardhi la 7.0la Contamana mnamo 2011.
"Idadi ya wanyama waliorekodiwa kwenye mitego ya kamera ilianza kupungua takriban siku 23 kabla ya tetemeko la ardhi - na kupungua kwa kasi siku nane kabla ya tetemeko la ardhi," Grant alisema katika nakala yake ya mwaka 2015 kuhusu utafiti. "Siku ya 10, sita, tano, tatu na mbili kabla ya tetemeko la ardhi - na siku ya tetemeko la ardhi - hakuna harakati za wanyama zilizorekodiwa, ambayo si ya kawaida sana."
Matetemeko ya ardhi mara kwa mara hutanguliwa na kipindi ambapo mifadhaiko mikali hutokea kwenye mwamba mzito - mikazo inayojulikana kuunda chaji za kielektroniki inayoitwa "positive holes". Vibeba chaji hizi za kielektroniki zinazohamishika sana zinaweza kutiririka haraka kutoka kwenye ukoko hadi kwenye uso wa dunia, ambapo huweka molekuli za hewa juu ya mahali zinapoonekana. Ionization kama hiyo imebainika kabla ya matetemeko kote ulimwenguni. Mashimo haya chanya yanapotiririka, pia hutoa mawimbi ya sumakuumeme ya masafa ya chini sana, na kutoa ishara ya ziada ambayo baadhi ya wanyama wanaweza kuichukua.
"Vitangulizi vya tetemeko la ardhi havijarekodiwa vyema kisayansi," anasema Matthew Blackett, profesa katika jiografia na majanga ya asili katika Chuo Kikuu cha Coventry. Lakini wanasayansi wengine wana nadharia kwamba wanyama huenda wameweza kubuni utaratibu wa kutoroka kwa mshtuko, anasema. "Labda wanatambua mawimbi ya shinikizo kabla ya matetemeko ya ardhi kufika, labda wanaona mabadiliko kwenyewa umeme wakati mwamba unapoanza kubana. Wanyama pia wana madini mengi ya chuma, ambayo hutambua sumaku na umeme."
Siku chache kabla ya tetemeko la ardhi la Gujarat nchini India la vipimo vya 7.7 mwaka 2001, kuongezeka kwa viwango vya kaboni monoksidi kulichukuliwa na satelaiti katika eneo la kilomita 100 mraba katika kile kilichotokea kuwa kitovu cha tetemeko hilo.
Wanasayansi wamependekeza kuwa gesi ya kaboni monoksidi inaweza kulazimishwa kutoka duniani kutokana na msongamano wa miamba wakati shinikizo la tetemeko linaongezeka.
Wanyama wengi, bila shaka, wana vifaa vya hali ya juu ambavyo vinaweza kusoma ishara za asili ambazo maisha yao yanaweza kutegemea - kwa hivyo inaonekana kuwa inawezekana kabisa kwamba wanyama wengine wanaweza kuchukua vitangulizi vyovyote vya tetemeko la ardhi.
Kemikali zisizopendeza zinaweza kunuswa, mawimbi ya chini kutambuliwa, na hewa iliyotiwa chuma kutambuliwa na manyoya.
Kwa kuwa matetemeko ya ardhi ni magumu sana kutabiri, matokeo haya yanaibua swali: je, wanadamu wanaweza kutabiri matetemeko ya ardhi kwa msaada wa wanyama, na hivyo kuweza kuwaonya watu yanakuja?
Katika nakala ya 2020, Wikelski na wenzake waliweka mfano wa mfumo wa tahadhari ya mapema ya tetemeko la ardhi kwa kutumia maeneo ya ufuatiliaji wa shughuli za wanyama, kulingana na data kutoka kwa utafiti wake nchini Italia.
Alikadiria kuwa wanyama wa kufugwa walio juu ya eneo la asili ya tetemeko la ardhi ambalo waliweza kuliona kwa njia fulani wangeonyesha shughuli saa 18 kabla ya kutokea. Wanyama walioko umbali wa kilomita 10 kutoka kwenye kitovu wanapaswa kuonyesha ishara saa nane baadaye, wakifuatwa na wanyama kwenye maeneo yaliyo umbali wa kilomita 20 saa nane zaidi baadaye. "Kama ni sahihi, hii itaashiria tetemeko la ardhi liko karibu ndani ya saa mbili zijazo," anasema.
Watafiti watahitaji kuchunguza idadi kubwa ya wanyama kwa muda mrefu katika maeneo tofauti ya tetemeko la ardhi duniani kote kabla ya kutumika kutabiri mitetemeko ya ardhi.
Kwa hili, Wikelski na wengine wanageukia mfumo wa kimataifa wa uchunguzi wa wanyama Icarus kwenye Kituo cha Kimataifa cha Anga cha Juu ili kukusanya data ya shughuli za wanyama duniani kote.
Wakati huo huo China, imeunda mfumo wa kutambua mitetemeko katika ofisi yake ya tetemeko la ardhi huko Nanning, kufuatilia tabia ya wanyama walio karibu zaidi na ardhi - haswa, nyoka katika mashamba katika eneo kubwa linalokumbwa na mitetemeko.
Nyoka wana mifumo mikubwa ya hisia inayolenga kugundua mabadiliko madogo katika mazingira yao, na ilikuwa ni mabadiliko ya ghafla ya tabia ya nyoka na wanyama wengine ambayo yalisababisha mamlaka kuuhama mji wa Haicheng nchini Uchina mnamo mwaka 1975, kabla ya tetemeko kubwa kupiga, hatua iliyookoa maisha ya watu wengi.
"Kati ya viumbe vyote duniani, labda nyoka ndio walio na uwezo zaidi wa kutambua mitetemeko ya ardhi," Jiang Weisong, ambaye wakati huo alikuwa mkurugenzi wa ofisi ya Nanning, aliiambia China Daily mwaka wa 2006. "Tetemeko la ardhi linapokaribia kutokea, nyoka watatoka kwenye viota vyao hata wakati wa baridi kali."
Mnamo mwaka wa 2014, wanasayansi waliokuwa wakifuatilia ndege wanaojulikana kama winged warblers nchini Marekani walirekodi mfano wa kushangaza wa kile kinachojulikana kama uhamaji wa kuhamishwa. Ndege hao walipaa ghafla kutoka katika eneo lao la kuzaliana katika Milima ya Cumberland mashariki mwa Tennessee na kuruka umbali wa kilomita 700 (maili 435) - licha ya kuwa walikuwa wameruka kilomita 5,000 kutoka Amerika Kusini.
Muda mfupi baada ya ndege hao kuondoka, kundi la kutisha la vimbunga zaidi ya 80 lilipiga eneo hilo, na kuua watu 35 na kusababisha uharibifu wa zaidi ya dola biloni 1.
Pendekezo hilo lilionekana kuwa wazi - kwa namna fulani ndege walikuwa wamehisi vijiti vikitoka umbali wa zaidi ya kilomita 400 (maili 250). Pia masafa ya chini ya sauti isiyoweza kusikika kwa wanadamu, lakini inapatikana katika mazingira asilia.
Kugundua tofauti katika sauti pia inafikiriwa kuwa njia ambayo ndege wanaohama wanaonekana kuwa na uwezo wa kukwepa dhoruba wanavuka bahari - wazo ambalo sasa linajaribiwa na utafiti unaoendelea unaojulikana kama Kivi Kuaka katika Bahari ya Pasifiki.
Mradi huo ulioanzishwa Januari 2021, unahusisha timu kutoka Makavasi ya Kitaifa ya Historia ya Asili ya Ufaransa inayojumuisha ndege 56 wa aina tano tofauti na vifuatiliaji vya GPS kufuata njia wanazopitia baharini. Kituo cha Kimataifa cha Anga za mbali hutoa uangalizi, kupokea mawimbi kutoka kwa ndege wanaporuka - na kuangalia jinsi wanavyokabili hatari za asili wakiwa njiani. Lebo zao pia hukusanya data ya hali ya hewa ili kusaidia kuboresha utabiri wa hali ya hewa kote eneo la Pasifiki.