Vita vya Afghan: Marekani na Taliban watia saini kumaliza vita vya miezi 18

Chanzo cha picha, AFP
Marekani na Taliban wamesaini mkataba wa makubaliano unaolenga kufikiwa kwa amani Amani Afghanistan baada ya mapigano ya zaidi ya miaka 18.
Marekani na washirika wake wa Nato wamekubaliana kuondoa wanajeshi wake katika taifa hilo kwa muda wa miezi 14, kama wanajeshi watadumisha mkataba huo.
Waziri wa mambo ya nje Mike Pompeo na kiongozi wa Taliban walihudhuria hafla hiyo katika mji wa Doha, Qatar.
Mazungumzo kati ya serikali ya Afghanistan na Taliban yanatarajiwa kufuata.
Chini ya makubaliano hayo yaliyotiwa saini Doha, wanamgambo pia wamekubaliana kuruhusu kundi la al-Qaeda na makundi mengine yenye msimamo mkali kufanya shughuli zao katika maeneo wanayodhibiti.
Marekani ilivamia Afghanistan wiki kadhaa baada ya shambulio la Septemba 2001 lililotekelezwa na kundi la al-Qaeda lenye makao yake Afghanistan.
Zaidi ya wanajeshi 2400 wa Marekani wameuwawa katika mapigano hayo.
Huku wengine takriban 12,000 bado wakiwa wapo katika taifa hilo. Rais Trump amehaidi kumaliza uhasama huo.
Mazungumzo kati ya Marekani na Taliban yalianzia wapi?
Tangu mwaka 2011, Qatar imekuwa mwenyeji wa viongozi wa Taliban ambao walienda huko kujadiliana suala la amani nchini Afghanistan. Ofisi ya Taliban ilifunguliwa 2013, na kufunga mwaka huo huo baada ya kutokea kwa malumbano juu ya bendera yao.
Aidha majaribio mengine ya kufanyika kwa mazungumzo pia yalikwama.
Mwezi Desemba 2018, jeshi lilitangaza kuwa watakutana na maafisa wa Marekani kujaribu kutafuta njia ya kufikiwa kwa Amani.
Lakini kikundi ya kiislamu cha IS kiliendelea kukataa kuhudhuria mazungumzo yoyote rasmi na serikali ya Afghanstan, na kuwataja kama vibaraka wa Marekani.
Kufuatia kufanyika kwa duru tisa za majadiliano kati ya Marekani na Taliban Qatar, pande hizo mbili zimefia makubaliano.
Mpatanishi wa Marekani alitangaza Septemba mwaka jana kwamba Marekani itaondoa wanajeshi wake 5,400 kutoka Afghanistan ndani ya wiki 20 kama sehemu ya makubaliano yaliyofikiwa na wanamgambo wa Taliban.
Siku chache baadaye, Bwana trump alisema mazungumzo hayo yamekwamba baada ya kundi hilo kumuua mwanajeshi wa Marekani. Lakini ndani ya wiki kadhaa, pande hizo mbili zilianza tena mazungumzo bila kujulikana.
Wiki moja iliyopita Taliban walikubaliana kupunguza ghasia ingawa maafisa wa Afghanistan wanasema karibia wanajeshi 22 na raia 14 wameuawa katika mashambulizi yaliyotekelezwa na Taliban ndani ya kipindi hicho.
Mkataba wa kihistoria uliozongwa na wasiwasi

Makubaliano hayo ya kihistoria yamekua yakiendelea kwa miaka mingi kwasababu pande zote zimekuwa zikitafuta kunufaika.
Mkataba huo umetokana na dhamira ya Marekani ya kurejesha vikosi vyake nyumbani huku baadhi ya Wataliban wakitambua kwamba mazungumzo ndio njia nzuri ya kurejea Kabul.
Ni moja ya hatua muhimu iliyopigwa licha ya uwepo wa hali ya wasiwasi kwa kiasi kikubwa kuhusu hatma ya mkataba huo.
Wakati ambapo kile kinachoonekana kuwa mbadala ni vita visivyokuwa na mwisho, raia wengi wa Afghanistan wako tayari kuchagua amani hata kama bado hali haieleweki.
Viongozi wa Taliban wanasema kwamba wamebadilika ingawa bado utawala wao mbaya miaka ya 90 bado unakumbukwa na wengi hasa wanawake wa Afghanistan.
Mchakato huu utakuwa jaribio kwa Taliban lakini pia kwa viongozi wa nyuma waandamaizi wa Afghanistan, na kizazi kipya ambacho kimepitia mengi katika kipindi cha miaka 20 iliyopita na kinatarajiwa kuwa siku za baadaye zenye mabadiliko.

Chanzo cha picha, AFP/Getty Images
Historia ya vita ya Afghan ni ipi?
Vita hii ilianza wakati ambao Marekani ilianzisha mapigano ya anga mwezi mmoja baada ya shambulizi la Septemba 11, 2001 kutokea na baada ya Taliban kukataa kumsalimisha mwanaume aliyekuwa akiongoza mapigano ya kigaidi, Osama bin Laden.
Ingawa jeshi lake lilikabadilika na kuwa kikosi cha waasi na kuendeleza mashambulizi ya mauaji kila kukicha dhidi ya serikali ya Afghanstan.
Muungano wa kimataifa ulisitisha oparesheni yake mwaka 2014, na kusalia tu ukitoa mafunzo kwa wanajeshi wa rain Afghan.
Lakini Marekani iliendelea na operesheni zake ikiwemo mashambulizi ya anga.
Hata hivyo, kundi la Taliban pia limekuwa likiendeleza uwepo wake na mwaka jana BBC ilibaini kwamba lilikuwa linaendesha shuguli zake katika asilimi 70 ya maeneo ya Afghanstani.
Kwanini vita hivyo vimechukua muda mrefu?
Kuna sababu nyingi sana.Lakini yanajumuisha upinzani mkali kutoka kwa taliban, uwezo wa vikosi vya Afghan na uongozi na nchi zingine kuonyesha kuendelea kuwa na vikosi vya Afghanistan kwa muda mrefu.
Katika kipindi cha miaka 18, kundi la Taliban limekuwa nyuma. Mwishoni wa 2009, rais wa Marekani Barack Obama alitangaza kuongeza wanajeshi wa Marekani nchini Afghanistan na kufikia idadi kubwa zaidi ya 100,000.
Idai hiyo ilisaidia kuondoa Wataliban katika baadhi ya sehemu za kusini mwa Afghanistan, lakini haikuwa imedhamiriwa kwamba hilo litachukua muda mrefu.












