Taliban laitaka Marekani kuondoka Afghanistan

Kiongozi mpya wa kundi la Taliban Haibatullah Akhundzada

Chanzo cha picha, AFGHAN ISLAMIC PRESS VIA AP

Maelezo ya picha, Kiongozi mpya wa kundi la Taliban Haibatullah Akhundzada

Kiongozi wa kundi la wapiganaji la Taliban amezungumza kwa mara ya kwanza tangu kuchaguliwa kwake mwezi mei, ambapo ameitaka Marekani kuondoka Afghanistan.

Maulawi Haibatullah Akhundzada amesema uwepo wa Marekani na washirika wake nchini Afghanistan hautaathiri juhudi za makundi ya kijihadi.

Wapiganaji wa Taliban
Maelezo ya picha, Wapiganaji wa Taliban

Amesema kuwa Taliban haitaki kuwa na ukiritimba wa mamlaka, japo akasisitiza kwamba ni Lazima serikali ya Afghanistan ikatize uhusiano wake na Marekani, kama hatua ya kwanza ya mchakato wa amani katika misingi ya sheria za kiislamu.