Maelfu wajitolea kupiga picha za utupu ili kuongeza ufahamu wa saratani 

g

Chanzo cha picha, Getty Images

Watu wapatao 2,500 wamejitolea kupiga picha za utupu wakati jua lilipochomoza mapema asubuhi kwenye ufukwe wa  Bond mjini Sydney Australia kwa ajili ya  kazi ya Sanaa iliyoandaliwa ili kuongeza ufahamu wa  saratani ya ngozi .

Shughuli hiyo imeandaliwa na  ya hivi karibuni ya mradi wa mpigapicha Mmarekani  Spencer, inayolenga kuwatia moyo Waastralia kupimwa mara kwa mara saratani ya ngozi.   

 Sheria ilibadilishwa ili kuruhusu watu kuwa watupu mahala pa umma kwenye fukwe kwa mara ya kwanza.

 Australia ni nchi inayoathiriwa na saratani ya ngozi zaidi duniani, Mfuko wa utafiti wa dunia wa saratani unasema.

g

Chanzo cha picha, EPA

g

Chanzo cha picha, EPA

Kuanzia saa tis ana nusu alfajiri, maelfu ya watu waliojitolea kuandaa kazi hiyo ya Sanaa walikusanyika kwenye ufukwe kushiriki  shughuli hiyo, iliyofanyika kwa ushirikiano na shirika la msaada linalopipa saratani ya Ngozi -Skin Check Champions katika  wiki ya saratani ya ngozi.

 "Tuna fursa ya kutoa uelewa zaidi kuhusu uchunguzi wa ngozi na nimepewa heshima…kuja hapa, nitengeneze Sanaa yang una kusherehekea tu mwili na ulinzi wake ," alisema msanii maarufu Tunick katika nukuu ya  Reuters.

 Bruce Fisher, mwenye umri wa miaka 77, ambaye alishiriki katika tukio hilo , aliliambia shirika la habari la  AFP: "Nusu  ya maisha yangu  nimeishi katika  jua na uvimbe kadhaa wa saratani  ya ngozi uliondolewa mgongoni mwangu.   

 "Nilidhani ilikuwa ni sababu nzuri na ninapenda kuvua nguo zangu kwenye ufukwe wa Bondi ."

Tunick anafahamika vyema kwa kutengeneza picha za watu wengi  watupu katika baadhi ya maeneo  asili maarufu zaidi  duniani.