'Siwezi kuondoka Afrika Kusini, nina mtoto hapa'

G

Chanzo cha picha, STANFORD MOGOTSI

Maelezo ya picha, Stanford Mogotsi (kushoto) na Kabelo Mashisi wametengeneza mifumo ya programu za kpmpyuta (software systems) kama zile za  Heineken na Fifa

Mkuu wa kampuni ya programu za kompyuta Stanford Mogotsi anasema bado ataishi Afrika Kusini, licha ya changamoto za kuendesha kampuni ndogo ya teknolojia ya mawasiliano nchini humo. 

 "Ni nyumbani kwangu, nina mtoto hapa, nina familia hapa," anasema  mkuu huyo mwenye umri wa miaka 46.

 Bw Mogotsi  ni mmiliki mwenza wa kampuni ya kutengeneza programu za kompyuta yenye makao yake mjini  Johannesburg  -Nane Solutions  na rafiki yake na mshirika wa kibiashara Kabelo Mashisi, 45.

 Wote wameanzisa mbali tangu walipokuwa wakikua pamoja katika miji ya Afrika Kusini wakatui wa ubaguzi wa rangi. 

 Kila mmoja wao alisomea masomo ya sayansi ya kopmpyuta, na walifanya kazi katika makampuni ya IT, kabla ya kuanzisha kampuni yao , Nane  mwaka  2006.

G

Chanzo cha picha, TRISTEN TAYLOR

Maelezo ya picha, Stanford Mogotsi, hapa akionyesha programu ya kompyuta ambayo kampuni yao iliibuni kwa ajili ya  Heineken, anasema ni vigumu kwa kampuni ndogo ya IT kushinda kandarasi ya  kazi   

Kazi yao ya awali ilikuwa ni ya kutoa ushauri – kuyashauri makampuni kama vile MTN, kampuni kubwa zaidi ya mtandao wa mawasiliano ya simu za mkononi , na kampuni inayomilikiwa na taifa ya umeme-Eskom.

 Lakini walibaini kuwa kazi ya ushauri ilikuwa inasumbua kwasababu walitaka kutengeneza programu za kumpyuta kuanzia mwanzo, kuliko kushauri tu. 

 Mafanikio yao ya kwanza makubwa yalikuwa ni kubuni mfumo wa Shirikisho la mpira wa miguu duniani FIFA wa kuweza kuwamudumia  wafanyakazi wa kujitolea katika Kombe l Dunia la 2010 , lililofanyika nchini Afrika Kusini.

Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

 Halafu katika mwaka 2017 walibuni programu ambayo ilisaidia kampuni ya kutengeneza pombe ya Heineken kuboresha mfumo wake wa usafirishaji  nchini humo. Mradi mwingine mkubwa ulikuwa ni wa kutengeneza programu (App) kwa ajili ya huduma ya  video ya simu unaojulikana kama  Talk360.

Lakini mafanikio hayo hayakupatikana kirahisi. Nane  ambalo ni neneo la Kiswahili, linalomaanisha namabari nane lilichaguliwa kwasababu kampuni hiyo ilikuwa na waasisi wanane. 

Hatahivyo, kuhama kutoka kazi ya ushauri na kuanza biashara ya kutengeneza programu ya kompyuta , na halafu athari za sheria kali za ‘’lockdown’’ za Covid-19 zilizowekwa na Afrika Kusini viliwafanya wote isipokuwa Bw Mogotsi na Bw Mashisi kujiondoa kwenye biashara hiyo.

"Ni vigumu sana kupata kazi wakati una kampuni ndogo," anasema Bw Mogotsi. "Ni lazima tushindane na makampuni ya kimataifa, na watu wanaoweza kuwa wateja  huwa wanataka kwenda kwenye makampuni haya ambayo yalifanyiwa majaribio na makubwa ya teknolojia ya mawasiliano -IT2, hususan wakati uchumi wa Afrika Kusini ni wa mashaka."

G

Chanzo cha picha, TRISTEN TAYLOR

Maelezo ya picha, Profesa  Duncan Coulter anasema kwamba matokeo yake watu wanahamia ng’ambo baadhi ya makampuni ya IT yanahangaika kuajiri.   

Huku Bw Mogotsi na Bw Mashisi wanabaki Afrika Kusini, Profesa Coulter anasema kwamba tatizo kubwa linaloendelea nchini Afrika Kusini ni kuondoka kwa watu wenye ujuzi wa IT – watu wanatafuta kazi katika nchi za kigeni. 

 "Wanafunzi wetu wengi sana sasa wanaondoka kwenda Ulaya, Marekani, Asia, na wanafanya vyema sana maishani mwao, tunajivunia sana maisha yao," anasema.

 "Na kama sehemu ya watu wenye ujuzi wanaokwenda mbali na Afrika Kusini  wanapata fursa ya haraka ya kupata ajira sawa na mawakili na madaktari ."

 Matokeo yake hawa vijana wte wenye taaluma ya teknolojia ya Mawasiliano- IT wanapata kazi ng’ambo, Profesa  anasema kwamba makampuni katika sekta hii nchini Afrika Kusini sasa yanahangaika  kujaza nafasi zao. 

Bw Mashisi anasema kuwa  "kimshahara hatuwezi kushindana" na ule unaotolewa na  makampuni makubwa ya ng' ambo.

Licha ya kuondoka kwa wasomi wengi wa IT nchini Afrika Kusini bado kuna makampuni yenye mafanikio yanayoanza ambayo yanatengeneza bidhaa maarufu.

 Mfano ni programu hii ya kompyuta inayofahamika kama  EskomSePush, ambayo iliwatahadharisha watumiaji kote nchini Afrika Kusini ni lini watarajie kukatwa kwa umeme. 

 EskomSePush ni kampuni iliyoanzishwa na  Dan Wells (35) pamoja na  Herman Maritz, waliozindua programu hiyo mwaka   2015 na kuiendesha kutoka katika nyumba zao mjini Cape Town.  

Getty

Chanzo cha picha, DAN WELLS

Maelezo ya picha, Dan Wells anasema programu nzuri ya kompyuta ni ile inayotatua tatizo 

Inakusanya na kupangilia mipangilio migumu kutoka kwa  Eskom  na serikali za mitaa kote nchini Afrika Kusini.

Halafu taarifa hutumwa kwa watumiaji kuwafahamisha ni lini umeme utapatikana katika maeneo yao na kwa muda gani.

Bw Wells anasema kwamba katika kipindi cha miezi sita ya kuanzishwa kwa programu hiyo, watu 250,000 wamekwisha ipakua, "jambo ambalo lilikuwa ni la kushangaza wakati huo".

Anaongeza kuwa leo programu iki  "katika siku milioni saba, na takriban watu milioni hubofya kupata taarifa  mara moja".

 Kama kuna kitu kinachowaunganisha Waafrika Kusini ni mapenzi ya mchezo, huku Kriketi ukiwa ni mchezo wa tatu unaopendwa zaidi nchini humo.

Getty

Chanzo cha picha, TRISTEN TAYLOR

Maelezo ya picha, Tevin Moodley anasema anataka kusaidia kizazi kijacho cha Afrika Kusini cha wachezaji wa kriketi  

Programu yake inaweza kutambua mara moja ni magongo mangapi yamepigwa na kila mchezaji kutokana na kurekodi mechi ya majaribio au mechi nyingine.   

 Hii inamaanisha kwamba mkufunzi wa kriketi anaweza kucheza video kadhaa za picha fulani, bila kulazimika kutazama picha zote kufahamu uwezo wa mchezaji.   

 Hii itasaidia timu na mkufunzi kutathmini mchezo na ni wapi marekebisho yanaweza kufanyika.

 Wakati programu yake bado iko katika awamu ya utafiti, Bw Moodley anasema kwamba kutokana na kwamba kuna wawekezaji wanaofaa na washikadau ataangalia jinsi yay a kujenga programy hiyo ya kibiashara 

 Lakini wakati huo huo lengo lake ni kusaidia kizazi kijacho cha Afrika Kusini cha wachezaji wa kriketi . "Ninataka kuifanya iwe ya hapa  na kujaribu kuisaidia timu yetu ," anasema.