Kombe la Dunia 2018 Croatia 1-2 England: Mashabiki walivyosherehekea kuwashinda England nusufainali, London 'walivyoomboleza'

Chanzo cha picha, AFP/Getty Images

Maelezo ya picha, Mashabiki wakisherehekea Zagreb

Mashabiki wa Croatia walisherehekea usiku kucha baada ya taifa lao kuwaondoa England kutoka kwa michuano ya Kombe la Dunia Urusi na kufuzu kwa fainali kwa mara yao ya kwanza kabisa, England waliomboleza.

Croatia walipata ushindi wa 2-1 baada ya mechi kumalizika sare ya 1-1 muda wa ziada.

Mashabiki walijaza uwanja ulio katikati mwa mji mkuu wa Croatia wa Zagreb wakiimba na kupeperusha bendera za taifa hilo. Baadhi walijitumbukiza hadi kwenye chemchemi za maji zinazopamba uwanja huo.

Mabao yalivyofungwa

Kieran Trippier dakika ya 5 Croatia 0-1 England

Ivan Perisic dakika ya 68 Croatia 1-1 England

Mario Mandzukic dakika ya 109 Croatia 2-1 England

Croatia ni taifa la watu milioni nne hivi na ni moja ya mataifa yenye idadi ndogo sana ya watu kuwahi kufika fainali Kombe la Dunia.

Watakutana na Ufaransa katika uwanja wa Luzhniki mjini Moscow Jumapili kwa fainali saa tatu usiku saa za Afrika Mashariki.

England watakutana na Ubelgiji mechi ya kuamua atakayemaliza nafasi ya tatu, mechi ambayo itachezewa mjini St Petersburg.

Kwa Croatia kukiwa kicheko na shangwe, kwa raia wa England kulienda masikitiko, huzuni na majonzi.

Chanzo cha picha, AFP/Getty Images

Maelezo ya picha, Mashabiki wakisherehekea Zagreb

Chanzo cha picha, AFP/Getty Images

Maelezo ya picha, Mashabiki wengi walijitokeza Zagreb

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Mashabiki wakicheza kwenye maji kusherehekea katikati mwa mji wao mkuu Zagreb

Chanzo cha picha, AFP/Getty Images

Maelezo ya picha, Rais wa Croatia Kolinda Grabar-Kitarovic (kushoto) alimpa waziri Mkuu wa Uingereza Theresa May jezi ya taifa hilo wakati wa mkutano mkuu wa Nato mjini Brussels, Ubelgiji

Chanzo cha picha, AFP/Getty Images

Maelezo ya picha, Kiongo wa kati wa Croatia Luka Modric (kati) akiwa na Mario Mandzukic (kulia) wakisherehekea Luzhiniki, Moscow
Maelezo ya picha, Shabiki huyu kwa jina Daniel alisherehekea kwa kinywaji, na aliambia BBC kwamba "ushindi huo ni mkubwa mno" kwa taifa hilo ndogo

Hali ilivyokuwa kwa England:

Walianza kwa matumaini baada ya bao kufungwa dakika za kwanza lakini baadaye wakavunjwa moyo.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Ndoto kwisha: Mashabiki wakifarijiana katika bustani maarufu ya Hyde Park jijini London

Chanzo cha picha, PA

Maelezo ya picha, Shabiki mdogo wa England akiliwazwa Castlefield Bowl, Manchester

Katika bustani ya Hyde Park, London, takriban mashabiki 30,000 walifika kutazama England wakicheza nusufainali, mkusanyiko mkubwa wa watu London kutazama mchezo wa kandanda tangu Euro 96.

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha, Shabiki huyu labda alizidi katika kusherehekea kabla ya mechi Urusi

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Shabiki wa England akisherehekea karibu na shabiki wa Croatia kabla ya mechi Urusi

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Maelfu ya mashabiki Hyde Park kabla ya mechi kumalizika

Chanzo cha picha, EPA

Maelezo ya picha, Wakati wa muda wa ziada Hyde Park

Chanzo cha picha, PA

Maelezo ya picha, Mashabiki wa England wakitokwa na machozi Manchester
Maelezo ya picha, Manchester wakisherehekea baada ya England kufunga bao la kwanza

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Mashabiki wakitokwa na machozi Brighton Beach

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Mashabiki waliovalia barakoa za Harry Brighton Beach

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Shabiki wa England, Hyde Park

Chanzo cha picha, PA

Maelezo ya picha, Mashabiki walivyokuwa wakisherehekea awali Nottingham Castle
Maelezo ya picha, Lily Harkin mwenye miaka minane alikuwa ameandika mgongoni mwa Cole Bryceland, Nottingham kwa matumaini, 'Kombe linarejea nyumbani', lakini baadaye 'England walirejea nyumbani' bila kombe

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Roho mkononi Millennium Square, Leeds

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Masikitiko Hyde Park