Watu 25 wafariki katika mlipuko katika kiwanda nchini India

Watu wasiopungua 25 wamefariki katika mlipuko katika kiwanda cha fataki katika jimbo la kusini mwa India la Tamil Nadu, huku wengine wanne wakijeruhiwa vibaya.
Mlipuko huo ulitokea Jumapili jioni. Kiwanda hicho kilitakiwa kufungwa lakini kulikuwa na takriban wafanyakazi 50 wakati huo, wanasema maafisa.
Mlipuko wa pili ulitokea wakati shughuli za uokoaji zikiendelea, na kuwajeruhi watu wengine 13, ingawa hakuna aliyepata majeraha makubwa ya moto, Afisa wa Wilaya, NO Sukhaputra aliliambia shirika la habari la ANI.
Chanzo cha mlipuko huo bado hakijajulikana na uchunguzi unaendelea.
Shughuli za uokoaji - ambazo sasa zimekamilika - zilipunguzwa kasi kwa kiasi kikubwa wakati fataki zikiendelea kulipuka ndani ya jengo hilo.
Polisi wamesema malalamiko yaliwasilishwa dhidi ya mmiliki wa kiwanda na msimamizi, ambao wote wamekimbia, na kuongeza kuwa timu nne maalum zimeanzishwa kuwafuatilia na kuwakamata.
Wakati huo huo, juhudi za kuwatambua waathiriwa zinaendelea. Maafisa wa wilaya wamesema 22 kati ya 25 waliokufa wametambuliwa hadi sasa - wengi wao ni wanawake.
Wiwanda vya fataki ni kwa ajili ya kuzalisha fataki za harusi na sherehe zingine.










