Moja kwa moja, Iran yasema iko mbali na makubaliano ya amani na Marekani, huku mlango bahari wa Hormuz ukifungwa tena

Spika wa bunge la Iran, Mohammad Bagher Ghalibaf, anasema pande hizo mbili "hazijakaribia kufikia makubaliano ya mwisho" ya mazungumzo ya kukomesha vita na Marekani.

Muhtasari

Moja kwa moja

Na Lizzy Masinga

  1. Marekani imesema nini kuhusu kuzuia bandari za Iran?

    Meli

    Kizuizi cha majini cha Marekani dhidi ya meli zinazoingia na kutoka bandari za Iran kimekuwa kikiendelea wikendi hii.

    Donald Trump alitangaza kizuizi hicho wiki moja iliyopita, chini ya siku moja baada ya mazungumzo marefu kati ya Marekani na Iran nchini Pakistan kushindwa kufikia makubaliano.

    Vikosi vya Marekani vilisema vitazuia au kuzirudisha meli zinazosafiri kwenda au kutoka pwani ya Iran, bila kujali utaifa.

    Marekani inatarajia kuweka shinikizo kwa Iran kwa kupunguza uwezo wake wa kufaidika na mauzo ya mafuta nje ya nchi.

    Kamanda Mkuu wa Marekani alisema wikendi hii kwamba amelazimisha meli 23 kugeuka karibu na Mlango Bahari wa Hormuz tangu kizuizi hicho kilipoanza.

    Katika chapisho la mitandao ya kijamii lililochapishwa saa moja tu iliyopita, Centcom inasema "kizuizi hicho kimesimamisha kabisa biashara ya kiuchumi inayoingia na kutoka Iran kwa njia ya bahari".

    Hata hivyo, BBC Verify ilifuatilia takribani meli nne kutoka bandari za Iran ambazo zilionekana kuvuka mstari wa kizuizi cha Marekani.

    Unaweza kusoma;

  2. Iran yasema iko mbali na makubaliano ya amani na Marekani, huku mlango bahari wa Hormuz ukifungwa tena

    Mohammad Bagher Ghalibaf

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Spika wa bunge la Iran, Mohammad Bagher Ghalibaf, anasema kwamba ingawa "maendeleo yamepatikana" katika mazungumzo ya kukomesha vita na Marekani, pande hizo mbili "hazijakaribia kufikia makubaliano ya mwisho".

    Ghalibaf alikuwa Pakistani wiki iliyopita kwa mazungumzo ya amani na wajumbe wa Marekani, akiwemo Makamu wa Rais JD Vance.

    Hakuna tarehe iliyowekwa kwa ajili ya duru inayofuata ya mazungumzo.

    Unaweza kusoma;

  3. Habari za asubuhi, karibu katika taarifa zetu hii leo