"Trump agundua Israel ilimdanganya " - The Independent

.

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Rais wa Marekani Donald Trump wakati wa mkutano wake na Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu katika Ikulu ya White House mjini Washington Septemba 29, 2025.
Muda wa kusoma: Dakika 4

Mapitio ya magazeti ya Uingereza, ambayo yanajumuisha uchambuzi wa mwenendo wa vita katika Mashariki ya Kati, uwili wa Marekani na Israel katika kukabiliana na Iran, athari za kupungua kwa matumizi ya fedha katika ulinzi wa Uingereza, na mizozo ya kisheria kuhusiana na athari za kutumia mitandao ya kijamii.

Katika gazeti la The Independent, makala ya Robert Fox inaangazia mwenendo wa vita vya Marekani na Israel dhidi ya Iran, yenye kichwa "Hatimaye, Donald Trump ametambua kwamba Israel imemfanyia hila."

Makala hiyo inazungumzia "kutoelewana hadharani" kati ya Rais wa Marekani Donald Trump na Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu kuhusu usimamizi wa vita na Iran.

Mwandishi anaamini kwamba wote wawili sasa wanahusika katika "kupanua wigo wa vita.

Kifungu hicho kinarejelea kile Idhaa ya 12 ya Israel iliripoti kuhusu hasira ya Trump kwa wito wa Netanyahu wa uasi nchini Iran kufuatia mauaji ya afisa mkuu wa Iran Ali Larijani na kamanda wa Basij Gholam Reza Soleimani.

Mwandishi huyo anasema kuwa, Trump alimkosoa vikali Waziri Mkuu wa Israel kwa kuielekeza Marekani kuwataka Wairani wote kuingia barabarani kuupindua utawala huo, na Trump alinukuliwa akimwambia Netanyahu katika mazungumzo ya simu: "Kwa nini tunatoa wito kwa watu kuingia mitaani wakati watauawa?"

Kulingana na mwandishi, kwa Trump hii ni upanuzi usio na msingi wa wigo wa misheni yao.

Kwa kuhofia hamu ya Trump ya kufikia makubaliano ya kumaliza uhasama mwishoni mwa wiki hii, Netanyahu aliripotiwa kuwataka majenerali wake kutekeleza "shambulio kali zaidi nchini Iran ndani ya saa 48 zijazo, kulingana na nakala hiyo.

Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Mwandishi anaamini kwamba kupeleka vikosi vya komando na askari wa miamvuli bila makubaliano yoyote rasmi ya kusitisha mapigano, na kujaribu kulazimisha kupita kwenye mlangobari huo, ni "kamari kubwa," kwani operesheni za ardhini sio sehemu ya mpango wa asili.

Mwandishi anajaribu kukagua masharti ya kijeshi ambayo yanaelezea hali ya sasa na ya baadaye ya vita.

Makala hayo yanaeleza kuwa ni Waisraeli wachache wanaotarajia suluhu la haraka la mzozo kati ya Iran, na neno la kimkakati la "kukata nyasi" limeibuka baada ya baadhi ya viongozi na wataalamu wa mikakati wa Israel kulitumia.

Hii ina maana haja ya kupigana ili kuwashinda wapinzani kama vile Hamas, Hezbollah, Walinzi wa Mapinduzi ya Iran, na hata taifa la Iran, mara kwa mara na kwa vizazi.

Kuna maneno "mkakati wa kuondoka" na "kutoka barabara kuu" ili kuelezea hamu ya kuondoka haraka kutoka kwa mgogoro wa Iran na mtego wa Mlango bahari wa Hormuz.

Mtazamo wa msemo "usikubali kushindwa" unajiri, kulingana na mwandishi, ambaye anaogopa kwamba majeshi ya Marekani na Israel yanakaribia kufanya hivyo: "kwenda katika vita na kukuza kushindwa."

Matumizi ya ulinzi wa Uingereza yamepungua

.

Chanzo cha picha, EPA

Maelezo ya picha, Mwanajeshi wa Uingereza anashiriki katika mazoezi ya uwanjani katika kituo cha kijeshi cha Tapa nchini Estonia

Mwandishi wa The Telegraph, David Blair anajadili katika makala yake "Uingereza iko chini katika orodha ya NATO ya 2025" kuhusu matumizi ya ulinzi wa Uingereza ikilinganishwa na nchi za NATO.

Inaaminika kwamba wakati nchi katika muungano huo zinazidisha juhudi zao za ulinzi, "bajeti iliyokwama ya Uingereza inahatarisha usalama na ushawishi wa nchi."

Blair anasema, "Habari njema ni kwamba wanachama wote wa NATO sasa wamejitolea kufikia lengo lililowekwa katika Mkutano wa Wales mwaka 2014, ambao ni kutumia angalau asilimia 2 ya Pato la Taifa kwa ulinzi," lakini aliongeza, "Kuna tofauti kubwa katika utendaji wa washirika."

Wanachama wa NATO wanaweza kugawanywa katika makundi manne, kuanzia "watendaji bora" hadi "wale wanaohitaji kuboreshwa," kulingana na mwandishi.

Uingereza inajikuta katika kundi la mwisho, baada ya Waziri Mkuu wa Uingereza Keir Starmer kutenga asilimia 2.3 tu ya Pato la Taifa kwa ulinzi mwaka jana, na kuiweka Uingereza katika nafasi ya 14 kati ya washirika 32.

Blair anakumbuka viashirio vya 2023, wakati bajeti ya ulinzi ya Uingereza ilikuwa kubwa zaidi barani Ulaya ilipopimwa kama asilimia ya Pato la Taifa, kabla ya kupungua katika mwaka uliopita.

Mwandishi anaonyesha kuwa washirika wengine wameongeza matumizi yao ya ulinzi maradufu, wakati Uingereza ikipiga hatua chache.

"Hii inaweza kuwa na madhara makubwa kwa ushawishi wa Uingereza ndani ya NATO," mwandishi alisema.

Blair anahitimisha: "Kwa kuwa Uingereza haina tena bajeti kubwa zaidi ya ulinzi barani Ulaya, na matumizi yake ya kijeshi kama asilimia ya Pato la Taifa yakiongezeka kidogo katika muongo mmoja uliopita, nafasi ya ushawishi wa Uingereza ndani ya muungano huo inaweza kutiliwa shaka."