Kyiv yashambuliwa huku viongozi wa dunia wakikutana kwa mkutano wa G20

Urusi imefanya shambulizi katika mji mkuu wa Ukraine  Kyiv,  huku milipuko ikisikika na moshi ukionekana kupaa angani

Majengo mawili ya makazi  katika wilaya ya kati ya mji huo ni miongoni mwa maeneo yaliyopigwa, kulingana na meya  Vitali Klitschko.

 Viongozi wa dunia kwa sasa wanakutana katika mkutano wa  G20  nchini Indonesia ambako wamelaani vita dhidi ya Ukraine.

Makombora kadhaa ya Urusi yameweza kudunguliwa na wahudumu wa uokozi wamefika eneo la tukio, amesema Bw Klitschko.

 Tahadhari ya uvamizi huo wa anga pia ilikuwa imetolewa na Ukraine.

Vitaly Kimm, Meya wa Mykolayiv, amedai kuwa makombora ya Urusi yalikuwa yameshambulia katika makundi matatu.

Katika  Chernihiv, Gavana Vyacheslav Chaus  aliwatahadharisha watu kutafuta hifadhi, akisema kuwa  "mashambulio ya makombora yanaendelea ".

Katika kipindi cha wiki iliyopita Urusi iliondoa vikosi vyake katika mji wa kusini mwa Ukraine wa Kherson -  ikiwa ni hasara kubwa kwa urusi tangu ilipoivamia Ukraine. 

Katika miezi iliyopita Urusi ilipoteza vibaya maeneo iliyokuwa imeyateka katika mashambulio ya ulipizaji yaliyofanywa na vikosi vya Ukraine. 

Takriban  makombora 70 yamepigwa nchini Ukraine, anasema mshauri wa masuala ya ulinzi wa Ukraine

“Hivi sasa tunavyoongea nimeona ripoti kwamba makombora ya Ballistic yamepigwa Ukraine ," Yuriy Sak anasema.

Baadhi ya maeneo ya mji wa kyiv hayana umeme, anasema meya wa mji, Andriy Sadovy.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Viongozi wa G2o , katika mkutano unaoendelea Indonesia

Milipuko imesikika pia kaskazini – mashariki mwa Kharkiv

Tumeanza kupikea picha za wimbi la mashambulizi ya makombora ya Urusi kote nchini Ukraine.

Milipuko pia imesikika katika mji wa kaskazini -mashariki wa  Kharkiv, kulingana na taarifa ya Interfax Ukraine , shirika la habari la Ukraine.

Meya wa Kharkiv, Igor Terekhov, alisema kuwa kumekuwa na "shambulio la kombora" katika mji huo na hakuna taarifa kuhusu vifo na majeruhi kwa sasa

Alisema kuwa kutokana na uharibifu, kuna matatizo ya umeme katika mji huo ambao umesitisha usafiri wa treni zinazotumia umeme- metro."Wahandishi wa umeme na wafanyakazi wa umma wa maeneo hayo wanafanya kila liwezekanalo kurejesha maisha ya kawaida katika mji wa   Kharkiv haraka iwezekanavyo," alisema kwenye Telegram.

 Milipuko pia imeripotiwa katika mji wa   Zhytomyr, kulingana na shirika la utangazaji la Ukraine, Suspilne.