Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Sarafi ya kurejea tena kwenye Mwezi ina umuhimu gani?
- Author, Rebecca Morelle
- Nafasi, Science editor
- Author, Alison Francis
- Nafasi, Senior science journalist
- Muda wa kusoma: Dakika 6
NASA kupitia mpango wake wa Artemis II imetuma wanaanga wanne kuelekea Mwezini.
Safari yao kuuzunguka Mwezi jirani yetu wa karibu angani itaandaa njia ya kutua Mwezini na hatimaye kujenga kituo cha kudumu huko.
Mpango wa Artemis umechukua miaka mingi ya maandalizi, umehusisha maelfu ya watu, na inakadiriwa kugharimu dola bilioni 93 hadi sasa.
Hata hivyo, kwa baadhi ya watu, kuna hisia ya kwamba "tayari tulishafanya hili."
Zaidi ya miaka 50 iliyopita, misheni za Apollo missions za Marekani ziliweka historia wakati binadamu wa kwanza walipotua juu ya uso wa Mwezi. Kwa jumla ya safari sita za kutua, ilionekana kana kwamba suala la Mwezi lilikuwa limekamilika kabisa.
Hivyo basi, kwa nini Marekani inatumia muda, juhudi na fedha nyingi kurejea tena?
Rasilimali zenye thamani
Uso wa Mwezi unaweza kuonekana mkavu, wenye vumbi na tupu—lakini sivyo ulivyo kwa kweli.
"Mwezi una mambo sawa na tuliyo nayo hapa Duniani," anasema Prof Sara Russell, mwanasayansi wa sayari katika Jumba la Makumbusho la Historia ya Asili.
"Mfano ni vitu asili adimu za dunia, ambazo ni chache sana duniani, na kunaweza kuwa na sehemu za Mwezi ambapo hizi zimejilimbikizia vya kutosha kuweza kuzichimba."
Kuna metali pia, kama chuma na titani, na pia heliamu, ambayo hutumiwa katika kila kitu kutoka kwa vifaa vinavyoweza kupitisha umeme usio na sufuri hadi vifaa vya matibabu.
- Harufu za ajabu za anga za juu zinazowashangaza wanasayansi
- Mlipuko wa jua ni nini na kwa nini unaweza kusababisha kukatika kwa umeme duniani?
- Unajua taarifa zako sasa kuhifadhiwa mwezini? Wanasayansi wanajenga Vituo maalumu huko
- Fahamu miamba ya angani iliyo karibu na dunia, na tishio linalowasumbua Wanasayansi
Rasilimali inayovutia zaidi ni ya kushangaza: maji.
Maji yamehifadhiwa ndani ya baadhi ya madini ya Mwezi, na pia yapo kwa wingi katika maeneo ya ncha zake. Kuna mashimo (craters) ambayo hayapati mwanga wa jua kabisa, na humo barafu hujikusanya.
Upatikanaji wa maji ni muhimu kwa maisha ya binadamu Mwezini. Mbali na kunywa, maji yanaweza kugawanywa kuwa hidrojeni na oksijeni hewa ya kupumua na hata mafuta ya vyombo vya angani.
Ushindani wa kutawala anga
Katika miaka ya 1960 na 1970, misheni za Apollo zilichochewa na ushindani wa anga kati ya Marekani na Umoja wa Kisovieti. Sasa, mshindani mkuu ni China.
China imekuwa ikifanya maendeleo ya haraka na mpango wake wa anga. Imefanikiwa kutua roboti na mashine kwenye Mwezi, na inasema itawafikisha wanadamu hapo ifikapo 2030.
Bado kuna ufahari wa kuwa wa kwanza kupandisha bendera yako kwenye vumbi la mwezi. Lakini sasa ni muhimu sana mahali unapoipanda.
Marekani na China zote zinataka kufikia maeneo yenye rasilimali nyingi, ambayo ina maana ya kupata mali isiyohamishika bora zaidi ya mwezi.
Mkataba wa Umoja wa Mataifa wa mwaka 1967 unasema hakuna nchi inayoweza kumiliki Mwezi. Hata hivyo, ''mtu anaweza kutumia eneo fulani bila kuingiliwa,'' anasema Dkt. Helen Sharman, mwanaanga wa kwanza wa Uingereza.
Hii ndiyo sababu mataifa yanajaribu kupata maeneo bora yenye rasilimali nyingi hata kama hayawezi kuyamiliki rasmi.
Njia kuelekea Mirihi
NASA inalenga kuwapeleka binadamu kwenye sayari ya Mars ifikapo miaka ya 2030.
Hili ni lengo kubwa na lenye changamoto nyingi za kiteknolojia. Ndiyo maana Mwezi unatumika kama sehemu ya majaribio.
China pia inapiga hatua kwa kasi katika programu yake ya anga, ikiwa tayari imetua roboti Mwezini na inalenga kupeleka binadamu huko kufikia mwaka 2030.
Leo hii, si tu kufika Mwezini kunakohesabika bali ni wapi hasa unatua.
Marekani na China zote zinataka maeneo yenye rasilimali nyingi zaidi.
"Kwenda Mwezini na kukaa huko kwa muda mrefu ni salama zaidi, nafuu zaidi na rahisi zaidi kuwa eneo la majaribio la kujifunza jinsi ya kuishi na kufanya kazi kwenye sayari nyingine," anasema Libby Jackson, mkuu wa anga katika Jumba la Makumbusho la Sayansi.
Kwa msingi wa Mwezi, Nasa inaweza kuboresha teknolojia ili kutoa mahitaji ya wanaanga wa hewa na maji. Watalazimika kufikiria jinsi ya kuzalisha nishati na kujenga makazi ili kulinda watu kutokana na halijoto kali na pia mionzi hatari ya angani.
"Hizi zote ni teknolojia ambazo ukizijaribu kwa mara ya kwanza kwenye Mirihi na zikakosea, kuna uwezekano wa janga. Ni salama zaidi na ni rahisi zaidi kuzijaribu kwenye Mwezi," Jackson anasema.
Mafumbo ambayo hayajang'amuliwa
Wanasayansi wana hamu yaa kupata na kushika nyenzo kutoka kwa Mwezi.
Miamba iliyoletwa nyumbani na wanaanga wa Apollo ilibadilisha uelewa wetu wa jirani yetu wa anga.
"Walituambia kuwa Mwezi uliundwa na tukio hili la kushangaza, ambapo mwili wa ukubwa wa Mars ulivunja Dunia na vipande vilivyotoka viliunda Mwezi. Tunajua kuhusu hilo kwa sababu ya miamba ya Apollo," anasema Prof Sara Russell.
Lakini anasema bado kuna mengi ya kugundua.
Kwa sababu Mwezi hapo awali ulikuwa sehemu ya Dunia, unashikilia rekodi ya miaka 4.5bn ya historia ya sayari yetu wenyewe. Na bila tektoniki za sahani, au upepo na mvua kufuta rekodi hii, Mwezi ni kibonge cha wakati mwafaka.
"Mwezi ni kumbukumbu nzuri ya Dunia," anasema Russell. "Usafirishaji mpya wa miamba kutoka eneo tofauti la Mwezi itakuwa ya kushangaza."
Kuhamasisha kizazi kipya
Misheni za zamani zilihamasisha watu wengi kuingia katika taaluma za sayansi, teknolojia na uhandisi.
Sasa, misheni za Artemis zinazorushwa moja kwa moja mitandaoni kwa ubora wa juu zinatarajiwa kuhamasisha kizazi kipya.
Katika dunia ya teknolojia, kuna haja kubwa ya wanasayansi, wahandisi na wataalamu wa hisabati, na anga lina uwezo mkubwa wa kuwavutia watu katika nyanja hizi.
Misheni ya Artemi iliyopeperushwa moja kwa moja kwa mitandao na katika ubora wa 4k inaaminka kuwa itahamasisha kizazi kipya.
"Tunaishi katika ulimwengu wa teknolojia. Tunahitaji wanasayansi, wahandisi na wanahisabati - na anga ina uwezo mzuri wa kuwasisimua watu kuhusu masomo hayo," anasema Libby Jackson.
Ajira mpya na uchumi wa anga unaostawi utaipa Marekani faida ya mabilioni ya dola ambayo yamemwagwa kwa Artemi. Kama vile mabadiliko yoyote kutoka kwa teknolojia iliyotengenezwa kwa misheni ambayo ina matumizi Duniani.
Lakini Helen Sharman anasema kurejea kwa Mwezi pia kutaipa dunia nguvu inayohitajika sana.
Zaidi ya yote, kurejea Mwezini kunaweza kuwa ishara ya uwezo wa binadamu kushirikiana na kufanikisha mambo makubwa.
Inaonyesha wazi kile ambacho wanadamu wanaweza kufanya wakishirikiana.
Imetafsiriwa na Mariam Mjahid