Tetesi za soka Ulaya: Gordon kuuzwa Bayern kwa £75m

Anthony Gordon

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Anthony Gordon
Muda wa kusoma: Dakika 2

Newcastle United wako tayari kumuuza nyota wake Anthony Gordon (25) kwenda Bayern Munich ikiwa mabingwa hao wa Ujerumani watakubali kutoa pauni milioni 75 kwa kiungo huyo mshambuliaji wa England (Times).

Manchester United wanaendelea kufuatilia kwa karibu hali ya Aurelien Tchouameni (26) ndani Real Madrid huku wakipanga kusajili angalau viungo wawili msimu huu wa joto (Telegraph).

Liverpool wamemuweka Yan Diomande (19) kama chaguo lao kuu kuchukua nafasi ya Mohamed Salah (33), uamuzi uliopitishwa na viongozi wa klabu (Florian Plettenberg - Sky Germany).

Cristian Romero (27) anawindwa na Atletico Madrid huku mustakabali wake Tottenham Hotspur ukiwa na mashaka (Caught Offside).

Curtis Jones

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Curtis Jones

Curtis Jones (25) haridhishwi na nafasi yake ndogo katika kikosi cha kwanza cha Liverpool na anaweza kuondoka majira ya joto (Football Insider).

Klabu za Manchester City na Liverpool huenda zikamkosa Alessandro Bastoni (27) kwani yuko tayari kuondoka Inter Milan kwa ajili ya Barcelona pekee (Mundo Deportivo).

Liverpool ni miongoni mwa vilabu vinavyomuwania Enzo Le Fee (26) kutoka Sunderland (Teamtalk).

Chelsea wamewasiliana na wakala wa Karim Adeyemi (24) wa Borussia Dortmund kuhusu uwezekano wa kumsajili (Fussballdaten).

Everton wanaongoza katika mbio za kumsajili Hayden Hackney (23) kutoka Middlesbrough (Teamtalk).

John Stones (31) anatarajiwa kuondoka Manchester City kama mchezaji huru majira ya joto (Fabrizio Romano).