Tetesi za soka Jumapili:Bayern Munich wanavutiwa na Rogers wa Aston Villa

Chanzo cha picha, Getty Images

Muda wa kusoma: Dakika 2

Morgan Rogers wa Aston Villa analengwa na Bayern Munich, ambao wamejiunga na Chelsea na Manchester United katika kumtaka mshambuliaji huyo wa Uingereza mwenye umri wa miaka 23. (Football Insider)

Kiungo wa kati wa Uingereza Curtis Jones, 25, anajiandaa kuondoka Liverpool msimu huu wa joto, huku Aston Villa ikiwa tayari mbioni kumnyakua. (Teamtalk)

Manchester City inaendelea kuweka kipaumbele katika uhamisho wa mlinzi wa Newcastle United wa Uingereza Tino Livramento, 23, lakini pia wanatafuta mbadala. (Teamtalk)

Chanzo cha picha, Getty Images

Real Madrid wanafikiria kumteua meneja wa zamani Jose Mourinho, ambaye yuko Benfica. (Record)

Real Madrid itafanya uamuzi kuhusu mustakabali wa meneja Alvaro Arbeloa mwishoni mwa msimu. (Marca)

Real Madrid wanapanga kufanya marekebisho makubwa ya kikosi chao msimu huu wa joto, huku kiungo wa kati wa Ufaransa, Eduardo Camavinga, 23, akiondoka. (Sport )

Chanzo cha picha, Getty Images

Kupandishwa kwa Coventry City hadi Ligi Kuu kunamaanisha uhamisho wa mkopo wa kiungo wa Nigeria Frank Onyeka, 28, kutoka Brentford utakuwa wa kudumu. (Talksport)

Lorient wanamfikiria aliyekuwa kocha wa Lens na Southampton Will Still kama chaguo la nafasi ya meneja. (L'Equipe)