Jinsi tiba mpya ya kuongeza kinga mwilini inavyoondoa saratani

Chanzo cha picha, Emmanuel Lafont/ BBC
- Author, Jamie Ducharme
- Nafasi, BBC
- Muda wa kusoma: Dakika 6
Baada ya karibu miaka 100 ya maendeleo, sasa matibabu yanayoimarisha mfumo wa kinga ya mwili ili kupambana na saratani ili kuokoa maisha ya wagonjwa yamepatikana.
Maureen Sideris mwenye umri wa miaka 71 alipotibiwa saratani ya utumbo mpana mwaka 2008, ilibidi afanyiwe operesheni. Matibabu yake yalifanikiwa, lakini mchakato wa kupona baada ya upasuaji ulikuwa mgumu.
Miaka kumi na minne baadaye, Sideris, anayeishi New York, aligunduliwa na saratani ya umio - na wakati huu, matibabu yake, yaliyotolewa kupitia jaribio la kimatibabu, ambalo ni tofauti kabisa.
Kila baada ya wiki tatu, kwenda Kituo cha Saratani cha Memorial Sloan Kettering huko New York City kwa ajili ya kuingizwa dawa kupitia dripu inayoitwa dostarlimab kwa muda wa dakika 45.
Baada ya miezi minne tu ya matibabu, uvimbe wa Sideris ulitoweka - bila upasuaji, mionzi au dawa, na athari yake pekee ni upungufu wa adrenal unaosababisha uchovu.
Sideris ni mmoja wa wagonjwa wanaoongezeka ambao wannufaika na tiba hii ya kuongeza kinga mwilini ili kupambana na saratani. Pamoja nayo inakuja na ahadi ya tiba ya kibinafsi, msamaha wa saratani wa muda mrefu na madhara machache kuliko matibabu mengine kama vile chemotherapy na radiotherapy.
Mwili una uwezo wa asili wa "kugundua na kuondoa seli za saratani," anaelezea Karen Knudsen, mtendaji mkuu wa Taasisi ya Parker iliopo Marekani, inakuza tiba ya kwa kinga mwilini.
Ikiwa tiba hiyo itakwenda vizuri, huondoa seli zote za saratani. Lakini wakati mwingine, seli za saratani hukwepa au huuzidi maarifa mfumo huo, na kusababisha saratani. Hujificha, bila ya kuweza kuzitofautisha na seli zenye afya.
Lengo la tiba ya kinga mwilini ni kufichua seli hizo za saratani ili mfumo wa kinga uweze kuziona jinsi zilivyo. Tiba hii iznaimarisha ulinzi wa mfumo wa kinga ili uweze kuzizpata na kuziharibu seli za saratani.
Tiba kutumia kinga ya mwili

Chanzo cha picha, Emmanuel Lafont/ BBC
Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.
Bonyeza hapa kujiunga
Mwisho wa Whatsapp
Kuna aina mbili za tiba kwa kutumia kinga mwilini, ni tiba ya seli T za CAR na vizuizi vya ukaguzi wa kinga mwilini. Tiba kwa seli T za CAR huhusisha kutoa seli T (seli maalum za kinga mwilini zinazowinda na kuua seli vamizi) kutoka kwenye damu ya mgonjwa, kuzibadilisha katika maabara ili ziweze kuzitafuta na kuzishambulia seli za saratani na kisha seli hizo za T zibaki mwilini. Tiba hii kwa sasa zinatumika kutibu saratani ya damu.
Vizuizi vya ukaguzi wa kinga mwilini, ni dawa ambazo huzuia kinga za mwili kutoa majibu makali ambayo huathiri seli zenye afya, ikimaanisha kwamba seli T hutambua seli za saratani kama tishio na kuanzisha shambulio.
Vizuizi vya kinga mwilini ni aina ya tiba kwa kutumia kinga ya mwili dhidi ya saratani, inayowezesha mfumo wa kinga kutambua na kushambulia seli za saratani kwa kuzuia seli ambazo huzuia seli T kuharibu saratani.
Wanasayansi walioanzisha uvumbuzi huu walishinda Tuzo ya Nobel mnamo 2018, na dawa hizo zinatumika kutibu saratani.
Mapungufu ya tiba
Hata hivyo, njia zote mbili zina mapungufu. Ingawa utafiti unaendelea, wanasayansi wameshindwa kufanya tiba kwa kutumia seli T za CAR zifanye kazi dhidi ya uvimbe (tofauti na saratani ya damu).
Saratani ya uvimbe huchangia zaidi ya 90% ya saratani mpya. Matibabu haya pia ni ghali na yanahitaji nguvu kazi ya kutosha.
Tiba kwa kutumia vizuizi vya kinga mwilini, vinaweza kuja na madhara," anasema Samra Turajlic, mtaalamu wa saratani ya katika Taasisi ya Francis Crick huko London.
Kwa sababu tiba hii inakusudiwa kuzuia mwili usishambulie tishu zake na kuzuia kinga hiyo kunaweza kuhatarisha seli zisizo za saratani pamoja na uvimbe.
Kulingana na Taasisi ya Kitaifa ya Saratani ya Marekani, madhara ya kawaida ni pamoja na vipele vya ngozi, kuhara na uchovu, huku katika hali nadra inaweza kusababisha uvimbe wa ini, moyo na figo.
Tiba hii inaweza kuwa ya maana ikiwa itadhibiti saratani kali. Lakini haifanyi kazi hivyo kila wakati. Tatizo kubwa linalokabili uwanja mzima wa tiba hii ya saratani, Turajlic anasema, ni kwamba hakuna tiba ya kinga inayofanya kazi kwa 100%.
Kuna sababu nyingi, kuanzia muundo wa uvimbe, ambao unaweza kupunguza seli za kinga zisifike, na sifa za seli za kinga zenyewe.
Kwa ujumla, kati ya 20% na 40% ya wagonjwa hupona kwa tiba ya kinga mwilini. Hiyo ina maana kwamba asilimia iliobaki ya wagonjwa, ambao ni wengi - hupoteza muda bila faida.
Tiba mchanganyiko

Chanzo cha picha, Emmanuel Lafont/ BBC
Je, wagonjwa wanaweza kutumia kinga ya mwili kupambana na saratani? Maktari wanataja mambo mengi kujibu swali hili.
Utafiti wa Wargo, unaonyesha kwamba wagonjwa wanaokula lishe zenye nyuzinyuzi nyingi wanaweza kuona matokeo bora kupitia mabadiliko kwenye vijidudu vya utumbo ambavyo vinaweza kusaidia mfumo wa kinga na kuzuia uvimbe.
Utafiti mwingine wa kushangaza unaonyesha kwamba statins, dawa za bei nafuu na zinazopatikana kwa urahisi za kupunguza kolesteroli, zinaweza kuongeza kinga mwilini.
Hata muda wa matibabu ni muhimu, utafiti wa hivi karibuni unadokeza kwamba wagonjwa waliopewa dozi mapema wanakuwa bora zaidi kupambana na saratani kuliko wale waliotibiwa kwa kuchelewa.
Kuchanganya tiba kwa kutumia kinga mwilini na matibabu mengine ya saratani, kama vile mionzi au ultrasound, inaweza kuwa njia nyingine ya kuongeza mapambano dhidi ya saratani.
"Mionzi inaweza kuufanya uvimbe uonekane na mfumo wa kinga," anaelezea Sandra Demaria, katika Kituo cha Matibabu cha Weill Cornell ambaye ametafiti mbinu hii tiba mchanganyiko.
Tiba ya ultrasound, hutumia mawimbi ya sauti ya masafa ya juu kushambulia uvimbe, inaweza kuufanya uvimbe pia uonekane na kinga za mwili.
Watafiti wengine wanatumia fursa ya uwezo wa tiba ya kinga mwilini kwa ajili kupata njia bora ya matibabu kutokana na magonjwa yao.
"Saratani si ugonjwa mmoja," Knudsen anasema. "Ni magonjwa 200 tofauti, na yote hutokana na sababu tofauti na yanapaswa kutibiwa tofauti." Hata wagonjwa wawili wenye aina na hatua sawa ya saratani wanaweza kuwa na magonjwa tofauti katika kiwango cha seli.
Wanasayansi katika Kituo cha Saratani cha Memorial Sloan Kettering tayari wamejaribu mbinu ya tiba mchanganyiko, ikiwa mgonjwa atatibiwa kwa kinga ya mwili kisha ikafuatiwa na operesheni, majibu yanakuwa bora zaidi.
Luis Diaz, mkuu wa saratani ya uvimbe katika Kituo cha Saratani cha Memorial Sloan Kettering anasema, "Tunapaswa kuhama kutoka nyakati za Zama za Kati hadi nyakati za kisasa," anasema. "Ili kuondokana na tiba za kukata tumbo au kibofu chako - tunapaswa kufanya vizuri zaidi kuliko hilo."
Chanjo za saratani
Watafiti wanaendelea kutafuta mbinu mpya za tiba ya kinga mwilini na kujaribu kuboresha mbinu za zamani - kama vile chanjo za saratani.
Watafiti kutoka Taasisi ya Saratani ya Dana-Farber nchini Marekani hivi karibuni waliunda chanjo za binafsi kwa watu tisa wenye aina ya saratani ya figo. Baada ya uvimbe wao kuondolewa kwa upasuaji, wagonjwa walichanjwa ili kuondoa seli zozote za uvimbe zilizokuwa zikiendelea mwilini mwao.
Katika utafiti uliochapishwa mwaka 2025, timu hiyo iliripoti kwamba wagonjwa wote tisa walianzisha mfumo maalum wa kinga dhidi ya saratani na walibaki bila saratani miaka kadhaa baada ya upasuaji. Chanjo binafsi pia zimeonyesha matumaini ya kutibu saratani.
Tafiti zaidi zinahitajika ili kuunga mkono baadhi ya mbinu zinazotia moyo za kupambana na saratani, na kufikia mustakabali ambapo madaktari wanaweza kuwatibu wagonjwa kwa usahihi na kwa uhakika na matibabu ambayo yatafanya kazi dhidi ya saratani zao.
"Mmoja wa madaktari [aliniambia] kwamba ndani ya miaka 10 ijayo, kutumia dawa kali na mionzi zitahesabiwa kuwa ni mbinu za kizamani," anahitimisha Sideris.















