Kwa nini Marekani inatuma vikosi maalum vya kijeshi Mashariki ya Kati?

Chanzo cha picha, Anadolu via Getty Images

Muda wa kusoma: Dakika 4

Marekani imekuwa ikiongeza nguvu zake za kijeshi katika ghuba ya uajemi. Kikosi cha The 31st Marine Expeditionary tayari kipo eneo hilo, huku kikosi cha 11th Marine Expeditionary na 82nd Airbone Division, pia wapo njiani kuelekekea eneo hilo.

Kulingana na shirika la habari la CBS, vikosi maalum vya Navy SEAL na Army Rangers wametumwa eneo hilo.

Tofauti na vikosi ambavyo tayari viko eneo hilo, vikosi hivi vipya vinatarajiwa kufanya oparesheni ya ardhini Mashariki ya Kati.

Kufikia sasa, Israel na Marekani wamejizuia kuanzisha oparesheni ya ardhini ndani ya Iran.

Kwa jumla zaidi ya wanajeshi elfu nane wamewasili eneo la Ghuba ya uajemi, 2500 kati yao wakiwa wanajeshi wa majini na takriban 4000 wakiwa wanajeshi wa anga.

Kulingana na wachambuzi, vikosi hivi vinaweza kutumika kwa njia tatu; kufungua mlango wa bahari wa Hormuz, kukiteka kisiwa cha Kharg au kuondoa madini ya urani kutoka nchini humo ambayo yanawekza kutumika kutengeneza silaha za nyuklia.

Kuwatuma wanajeshi zaidi eneo hilo kunaashiria kuwa Marekani iko tayari kutanua matumizi yake ya jeshi, na huenda vita hivi visiende kama ilivyotarajiwa awali.

Kufunga mlango wa bahari wa Hormuz

Iran ilifunga Mlango wa Bahari wa Hormuz baada ya mashambulizi ya anga kuanza mwishoni mwa mwezi Februari.

Kulingana na mamlaka ya nishati ya marekani (EIA) mwaka wa 2024, takriban 20% ya biashara ya dunia ya gesi asilia iliyoyeyushwa hupitia eneo hilo.

Meli za kibiashara, ikiwemo supertankers, kwa sasa haziwezi kupitia eneo hilo la bahari.

Rais wa Marekani Donald Trump anaitaka Iran ifungue Mlango huo wa bahari kufikia Aprili 6, akitishia kuongeza mashambulizi ya anga, ikiwa ni pamoja na kulenga vituo vya nishati.

Hata hivyo, ikiwa Iran itakataa kutii, hata baada ya mashambulizi ya anga kuongezeka, Marekani inaweza kutumia majeshi yake kufungua Mlango wa Bahari wa Hormuz.

Ulinzi wa baharini

Chanzo cha picha, US Marine Corps via Getty Images

Kufungwa kwa eneo hili kunategemea visiwa vilivyo katika Mlango Bahari wa Hormuz

Visiwa hivi ni vya Abu Musa, Greater na Lesser Tunb vilivyo magharibi mwa Mlango Bahari wa Hormuz, na vinaweza kufunga mlango wa kutoka Ghuba ya Uajemi.

Visiwa hivi vinazozaniwa kijiografia kati ya Iran na UAE.

Visiwa hivi vina uwanja wa ndege na miundo mbalimbali ya kijeshi, ikiwemo nafasi za ulinzi wa anga na mifumo ya makombora inayoweza kushambulia malengo yaliyo ardhini na majini.

Kisiwa muhimu zaidi kilicho ndani ya mlango huo ni Qeshm, kisiwa kikubwa zaidi katika Ghuba ya Uajemi. Kinaenea kando ya pwani ya Iran kwa zaidi ya kilomita mia moja na kinatumika kama ngome inayodhibiti mlango huo wa bahari.

Kuna visiwa vingine kadhaa karibu nacho vinavyotumika kudhibiti mlango huo na ni Larak, Hormuz, na Hengam.

Iran iliona kufunga Mlango wa Bahari wa Hormuz ni njia moja ya kujilinda kwa kuzihami visiwa hivi na silaha za vita.

Bandari kuu ya mafuta

Kisiwa cha Kharg pia kinaweza kutekwa.

Takriban 90% ya biashara ya mafuta ya Iran, chanzo kikuu cha mapato kwa utawala wa nchi hiyo, hupitia kisiwa hiki.

Kukiteka kisiwa hiki kutapunguza mapato ya mafuta ya Iran na, kwa hivyo, kupunguza uwezo wake wa kufadhili harakati zake za kijeshi na kutengeneza makombora na silaha za nyuklia.

Lakini iwapo hilo litatokea huenda ikachochea mashambulizi ya kulipiza kisasi dhidi ya malengo muhimu eneo la Ghuba na inaaminika kuwa hadi sasa Iran imeepuka kushambulia malengo mengi yenye umuhimu mkubwa kiuchumi katika eneo la Ghuba.

Chanzo cha picha, Gallo Images/Orbital Horizon/Copernicus Sentinel Data 2024

Marekani tayari imefanya mashambulizi kadhaa kwenye kisiwa hicho cha Kharg, lakini inaaminika kuwa malengo yao yalikuwa ni miundo ya kijeshi tu.

Visiwa

Marekani kudhibiti visiwa vidogo vilivyo karibu na pwani ya Iran, ni muhimu iwapo wanataka kuanzisha oparesheni za kijeshi eneo la bara.

Visiwa, hivyo vinaweza, kutoa ulinzi wa anga kwa hivyo, ni muhimu kuvidhibiti kabla ya kuingia kwenye taifa lenyewe.

Hata hivyo, majeshi yaliyoko kwenye visiwa yanaweza kulengwa kwa mashambulizi kutoka bara.

Kunyakua madini ya urani

Wanaeshi wa Marekani iwapo watatosheleza, wanaweza kufanya operesheni ya kuondoa akiba ya urani iliyoyeyushwa ya Iran iliyohifadhiwa katika vituo vya Isfahan na Natanz. Vituo hivi vilishambuliwa wakati wa vita vya siku 12 na Israel.

Hapo awali, Channel 12 ya Israel iliripoti kuwa ili kuondolewa kwa vikwazo, Washington inaitaka Tehran, miongoni mwa mambo mengine, iharibu uwezo wake wa kinyuklia ikiwemo kuharibu vituo vya kutengeneza silaha hizo, na kisha kuipa madini ya urani iliyoyeyushwa shirika la kudhibiti matumizi ya nyuklia IAEA.