Tetesi za Soka Ulaya Alhamisi: PSG inamfuatilia Fernandes West Ham

Chanzo cha picha, Getty Images

Muda wa kusoma: Dakika 3

Paris St-Germain imeanza kuwasiliana na wawakilishi wa kiungo wa Ureno na klabu ya West Ham Mateus Fernandes, 21. (Foot Mercato - kwa Kifaransa)

Chelsea inaandaa orodha fupi ya wagombea watakaochukua nafasi ya Liam Rosenior, huku mkufunzi anayeondoka Bournemouth Andoni Iraola akiwa miongoni mwa wale wanaotajwa. (RMC Sport - kwa Kifaransa)

Chelsea pia inamfuatilia kiungo wa zamani Cesc Fabregas, ambaye kwa sasa anainoa klabu ya Como ya nchini Italia. (Football Insider)

Barcelona inamtaka Marcus Rashford, 28, kusalia nao kwa mkopo msimu ujao badala ya kuilipa Manchester United pauni milioni 26 iliokubaliwa hapo awali ili kumsajili mshambuliaji huyo wa Uingerezakwa mkataba wa kudumu. (Mirror)

Klabu za Liverpool, Chelsea, Tottenham, Aston Villa na Newcastle zimeonyesha nia ya kutaka kumsajili kipa wa Manchester City na England James Trafford, 23. (Goal)

Manchester United imemuomba kiungo wa kati wa Ureno Bruno Fernandes, 31, kusalia Old Trafford. (Sun)

Sunderland huenda ikamfuta kazi meneja Mfaransa Regis Le Bris mwishoni mwa msimu huu kalbu hiyo isipofuzu kwa soka la Ulaya . (Sportsport)

Chanzo cha picha, Getty Images

Bayern Munich haina mpango wa kuongeza mkataba wa mkopo wa mshambuliaji wa Senegal Nicolas Jackson, 24 kutoka Chelsea mwishoni mwa msimu huu. (Florian Plettenberg)

Barcelona inawanyatia washambuliaji kadhaa msimu huu wa joto akiwemo mshambuliaji wa Manchester City na Ureno Bernardo Silva, 31, na mshambuliaji wa Chelsea wa Ureno Pedro Neto, 26. (Mundo Deportivo - kwa Kihispania)

Juventus inamsaka mlinda lango mpya msimu huu wa joto na mlinda mlango wa Liverpool na Brazil Alisson, 33, anaongoza katika orodha yao ya usajili. (Fabrizio Romano)

Manchester United inamfuatilia kiungo wa kati wa Bournemouth Muingereza Alex Scott, 22. (Mirror)

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Alisson alikosa mechi mapema msimu huu kwa sababu ya jeraha la misuli ya paja

United pia inamtaka Richard Rios wa Benfica, huku mchezaji huyo wa kimataifa wa Colombia mwenye umri wa miaka 25 akipewa nafasi ya kiungo. (Caught Offside)

Bournemouth wamejiunga kwenye kinyang'anyiro cha kumnunua kiungo wa kati wa Bayer Leverkusen wa Marekani Malik Tillman, 23. (Team Talk)

Fulham inajianda kwa mpango wa dharura ikiwa meneja Marco Silva ataamua kuondoka mkataba wake utakapokamilika mwishoni mwa msimu. (The I)

Arsenal inamfuatilia kiungo wa kati wa Uturuki Arda Guler, 21, ambaye huenda akaamua kuhamia Real Madrid kutokana sintofahamu kuhusu mustakabali wa meneja Alvaro Arbeloa. (Caught offside)