Jinsi rubani wa Marekani aliyetoweka Iran alivyookolewa

Chanzo cha picha, Getty Images

    • Author, Gabriela Pomeroy
    • Author, Grace Eliza Goodwin
  • Muda wa kusoma: Dakika 7

Marekani imemuokoa rubani wa pili aliyepotea ndani ya Iran baada ya ndege ya kivita ya nchi hiyo kudunguliwa. Ndege hiyo aina ya F-15 ilidunguliwa Ijumaa kusini mwa Iran.

Rais wa Marekani Donald Trump, amethibitisha kuokolewa kwa rubani huyo kupitia ujumbe aliouchapisha kwenye mtandao wake wa kijamii wa Truth Social mapema Jumapili, baada ya jeshi la Marekani kuendesha operesheni ngumu ya uokoaji katika historia yake. ''Mwanajeshi huyo yupo salama salmini'', aliongezea Trump.

Wanajeshi wawili waliokuwa ndani ya ndege hiyo ya kivita walijiondoa kutoka kwa ndege hiyo punde tu hali ya hatari ilijitokeza. Rubani mmoja aliokolewa Ijumaa na wanajeshi wenzake wa Marekani.

Mamlaka za Iran zimesema kwamba ndege hiyo ya kivita ilidunguliwa na mfumo wake wa makombora ya kutoka ardhini kuelekezwa angani.

Taarifa za ziada kuhusu operesheni ya uokoaji na jinsi ilivyotekelezwa bado zinaendelea kutolewa. Kwa sasa tunayafahamu haya:

Mwanajeshi huyo aliokolewa vipi?

Majeshi ya Iran na Marekani yalikuwa mbioni kumtafuta mwanajeshi wa Marekani aliyoepotea baada ya ndeeg ya kivita ya Marekani kudunguliwa katika eneo la kusini mwa Iran.

Taarifa za undani kuhusu mpango wa uokoaji wa Marekani, bado hazijawekwa wazi, ila mtu mmoja ambaye alikuwa na ufahamu wa ndani wa operesheni hiyo aliielezea kama 'operesheni kali ya kimkakati ya kivita ' ya uokoaji ambayo ilitekelezwa kusini mwa Iran.

BBC inafahamu kwamba kulikuwa na makabiliano kati ya majeshi ya Iran na Marekani wakati wa operesheni hiyo, na kwamba rubani huenda alijeruhiwa punde tu alipojiondoa kwenye ndege hiyo.

Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Operesheni ya kuwaokoa wanajeshi ambao pia ni marubani wa ndege ya kivita iliyodunguliwa ni mojawapo ya masuala magumu ambayo hutegemea wepesi wa kazi kwa ajili ya kutoharibu mud awa kuwapata wakiwa hai- Operesheni hiyo ya uokoaji ya kijeshi inafahamika kama {Combat serarch and rescue – CSAR} na ambayo Jeshi la Marekani hutumia kwa uokoaji wa wanajeshi wake na ambayo pia inatumika na majeshi ya mataifa washirika wa Marekani.

Misheni hizi kwa wakati mwingi hutekelezwa na ndege aina ya helikopta, ambazo hupaa juu ya anga ya 'adui', zikisindikizwa na ndege nyinginezo za kivita ambazo hutekeleza mashambulizi na kushika doria katika shughuli hiyo nzima.

Katika ujumbe wake aliouchapisha kwenye mtandao wake wa kijamii wa Truth Social ,Rais Trump amesema kwamba Mwanajeshi huyo katika Jeshi la Ngani la Marekani ambaye ni Kanali –''alikuwa katika himaya ya maadui wa Marekani, na hususan alikuwa katika eneo la milimani nchini Iran alipokuwa akitafutwa na maadui wa Marekani, ambao walikuwa wanakaribia alipokuwa kwa kila saa alipozidi kuwa ndani ya Iran.'

Rais huyo ameongezea kwamba eneo ambapo mwanajeshi huyo alikuwa – lilikuwa linashikwa doria na jeshi la Marekani kwa 24 kila siku ambapo alikuwa huko. Operesheni ya kumlinda mwanajeshi huyo ilisimamiwa na kutekelezwa na maafisa wakuu wa jeshi ambao walihusika na kupanga operesheni hiyo ya uokoaji.

Rais Trump amesema kwamba jeshi la Marekani lilituma makumi ya ndege za kijeshi nchini Iran na kudai kwamba operesheni hiyo ilitekelezwa bila ya wanajeshi wa Marekani kuuawa au kujeruhiwa.

Shrika la habari la kitaifa la Iran limeripoti kuwa wanajeshi kutoka kitengo cha ulinzi wa mapinduzi {IRGC} kimedungua ndege isiyo na rubani inayomilikiwa na Marekani, ilipokuwa kwenye operesheni ya kumtafuta rubani wa Marekani aliyekuwa amepotea.

Ndege hiyo ya Kimarekani isiyokuwa na rubani, ilianguka katika mkoa wa ISFAHAN, kusini mwa Iran huku afisa wa mawasiliano ya umma wa kitengo cha jeshi la mapinduzi la Iran akinukuliwa kuthibitisha hilo.

Awali, Iran ilisema kwamba ilitaka kuwapata wanajeshi hao wawili wa Marekani waliopotea Iran wakiwa hai, na hata kutoa tangazo la kumzawadia raia yeyote atakayewasaidia kuwapata.

Kulingana na jeshi la Marekani, wanajeshi wanaotekeleza misheni za kijeshi hupata mafunzo maalum ya kuwawezesha kujificha na kustahmili ugumu n ahata kutoroka eneo la adui ikiwa watajipata katika hali kama ile ya Ijumaa.

''Jukumu lao kuu ni kuhakikisha wanasalia kuwa hai na kuhakikisha hawakamatwi na jeshi la nchi ya kiadui,'' alisema Jeniffer Kavanagh ambaye ni Mkurugenzi wa kampuni ya utafiti wa mambo ya kijeshi ya Defense Priorities alipohojiwa na BBC.

''Wanapata mafunzo ya kuwawezesha – kuwa na wazo kuwa wana uwezo wa kujiokoa na ikiwa hawajajeruhiwa – basi anaweza kuondoka kutoka eneo alipotua baada ya kujiondoa kwenye ndege angani, na anapaswa kufanya hivyo mara moja na kujicha asionekane na maadui kwa ajili ya usalama wake.''

Pia wamepata mafunzo ya kustahmili hali ngumu katika mazingira magumu, ili kuweza kukaa muda mrefu bila ya kuwa na maji ya kunywa au chakula au ajitafutie jinsi ya kupata cha kula hapo alipo kwa muda utakaohitajika, Kavanagh alisema.

Ndege ilidunguliwa wapi na lini?

Shirika la habari la kitaifa nchini Iran limedai kwamba ndege hiyo ya kivita ilidunguliwa siku ya Ijumaa wakati jeshi la Iran lilipolenga ndege hiyo iliyokuwa inapaa angani katika eneo la Kusini mwa nchi hiyo.

Eneo halisi ambapo ndege hiyo aina ya F-15 iliripotiwa kuangushwa halikuthibitishwa, ila mikowa miwili iliyosemekana ndege hiyo ilikuwa imeanguka ilitajwa na vyombo vya habari vya Iran. Mikoa iliyotajwa ni Kohgiluyeh na Boyer-Ahmad na vile vile Khuzestan.

Wanajeshi wawili walikuwa ndani ya ndege iliyodunguliwa. Rubani wa kwanza aliokolewa mapema. Operesheni ya uokoaji ilijumuisha ndege kadhaa kama ila ya aina ya A-10 Warthog ambayo ilishambuliwa kwenye anga katika eneo la Ghuba kabla ya rubani wake kujiondoa na kuokolewa.

Ndege moja aina ya helikopta - iliyombeba rubani wa ndege ya kivita ya F-15E Jet iliyodunguliwa – ililengwa katika shambulizi la silaha ndogo kama roketi, ambapo wanajeshi waliokuwa ndani wakati wa kushambuliwa walijeruhiwa , lakini ndege hiyo ilifanikiwa kusafiri na kutua salama, kwa mujibu wa vyombo vya habari kutoka Marekani.

Kitengo maalum cha jeshi la mapinduzi {IRGC} kimesema kwamba jamii ya wafugaji ambayo inaishi katika eneo la milima nchini Iran, ilifyatulia risasi ndege mbili za kivita za Marekani aina ya Black Hawk Helikopta.

Kitengo cha kuthibitisha taarifa cha BBC Verify, kimethibitisha kuwa picha ya video iliyochapishwa Ijumaa ikionyesha kinachoonekana kama watu watatu waliokuwa na silaha wakifyatulia risasi au makombora upande ambapo helikopta hizo za BlackHawk zilikuwa zinapaa angani.

Usimamizi mkuu katika jeshi la Iran umesema kwamba mfumo mpya wa ulinzi wa ang awa Iran umewawezesha kudingua ndege za kivita za Marekani. Haya ni kw amujibu wa shirika la habari linalomilikiw ana serikali la IRNWA.

Mikowa ya Kohgiluyeh na Boyer-Ahmad ipo katika eneo la milima mingi la kusini mwa Iran, ambapo ni makazi ya watu zaidi ya laki saba ikiwemo jamii ya Wafugaji.

Wafugaji hao wa kuhamahama, wanaoishi katika eneo hilo, wanafahamika sana kwa kumiliki bunduki ambazo huzitumia kuwalinda mifugo wao na kambi zao za muda dhidi ya wezi hasa wakiwa katika maeneo ya nyada za juu, milimani.

Mkoa wa Khuzestan una umaarufu wa mali kubwa ya mafuta na ndipo viwanda vingi vilipo. Ni makazi kwa watu zaidi ya milioni 4.7, n ani watu wa tabaka mbali mbali, wakiwemo Waarabu, Waajemi, WaLor na makundi mengine ya kijamii.

Tunafahamu nini kujusu misheni ya ndege ya kivita iliyodunguliwa?

Chanzo cha picha, US Air Force via Getty Images

Maelezo ya picha, Picha ya maktaba ya ndege mbili za kivita za F-15E

Ndege ya kivita ya F-15E imeundwa kwa ajili ya kutekeleza mashambulizi ya angani kwelekezwa ardhini na vile vile mashambulizi ya angani ambayo yanahususha makabiliano na ndege nyinginezo za kijeshi.

Katika majukumu ya kutekeleza mashambulizi ya angani kuwlekezwa ardhini, rubani wa ndege hii anaweza kurusha makombora kwa eneo mahsusi inayolengwa kwa kutumia teknolojia ya miamba ya lazer inayomuonyesha eneo husika kulingana na data iliyoweka kwa mfumo wake. Mabomu yake pia yanasimamiwa na mfumo wa GPS unaozielekeza hadi kwenye eneo maalum ambalo ndege hiyo imetakiwa kushambulia.

Ndege hiyo inasimamiwa na maafisa wawili: Wa kwanza ni Rubani na afisa wa pili mtaalamu wa mahsmabulizi ya silaha – anayefahamika kama WIZZO katika jeshi . Jukumu la afisa huyu ni kuchagua maeneo ya kulengwa na kuhakikisha kwamba silaha zilizopangiwa kulenga maeneo yaliyo ardhini yanafanya hivyo kulingana na program ilivyopanga.

Wanajeshih awa wawili hugawanya majukumu, hasa katika maizngira ambapo hali ya kivita ni ngumu na wanatakiwa kurusha makombora au kujibu mashambulizi kwa haraka na hasa anapojaribu kukwepa tishio rubani.

Hatufahamu ni nini hasa kilichodunguwa ndege hiyo ya Marekani, lakini kama ilifanikiwa kuangushwa na WaIrani, sababu kuu ya uwezo hu oni mfumo wa ulinzi wa makombora yanayotoka aradhini kuelekzwa angani -SAM.

Taarifa ya ziada na Ghoncheh Habibiazad, BBC Idhaa ya Kiajemi

Imetafsiriwa na Leillah Mohammed na kuhaririwa na Ambia Hirsi