Kombe la Dunia2018: Ni nini kinachochangia mkwaju bora wa penalti?

Ni nini kinachochangia mkwaju bora wa penalti? Nani mwenye rekodi bora ya kupiga penalti? Je mtu anafaa kuwa na bahati?

Huku michuno hiyo ya kombe la dunia ikiingia katika awamu ya muondoano tunaangazia mikwaju ya penalti katika historia ya kombe la dunia, 26 ikiwa imepigwa tangu kuzinduliwa 1978- Ijapokuwa hakuna penalti zilizohitajika nchini Argentina mwaka huo.

Kupiga penalti bora

Kati ya mikwaju 240 katika kombe la Dunia kabla ya michuano hiyo 2018 nchini Urusi, 170 ilifungwa-ikiwa ni kiwango cha 7 kati ya 10.

kati ya penalti zilizofanikiwa kuingia katika goli, eneo zilizopigwa na kufungwa ni la chini pamoja na upande wa kushoto wa mkono wa kipa kulingana na data kutoka kwa wataalam wa soka Opta.

Mkwaju wa penalti unaopigwa vibaya zaidi ni ule wa chini chini na katikati ya goli ikiwa ni asilimia 58 ya mikwaju hiyo iliofanikiwa kuingia katika wavu.

Kupiga eneo la juu la goli

Iwapo mchezaji ataamua kupiga penalti yake katikati ya goli basi anafaa kulenga juu . hakuna kipa aliyeokoa mkwaju hata mmoja kati ya 15 iliopigwa katika kombe la dunia katikati na juu

Kulenga eneo la juu la goli kwa jumla ni mpango mzuri , kama Harry Kane alivyoonyesha katika mechi ya Uingereza dhidi ya England's group game against Panama, akipiga mikwaju yake katika kona ya juu kushoto ya wavu

Data ya Opta inaonyesha kuwa asilimia 90 ya penalti zote zinozopigwa eneo la juu ya maeneo yote ya kando kando ya goli hufungwa

Lakini mpango huo hukumbwa na hatari ya kukosa lango, kama alivyogundua mshambulaiji wa zamani wa Itali Roberto Baggio katika fainali za kombe la dunia la 1994, alipopiga mpira juu na kuipatia Brazil Ushindi.

Ni mkwaju mmoja kati ya mitano ambayo imeokolewa ikiwa ni 49 kati ya majaribio 240 huku makipa 28 wakihusika katika kuokoa mikwaju hiyo

Mikwaju hiyo imeokolewa kwa asilimia sawa katika pande zote za kushoto na kulia ambapo imeokolewa mara 24 baada ya kipa kuruka upande wa kushoto na mara 25 baada ya kipa kuruka upande wa kulia

Mikwaju 12 imepiga mwamba wa goli ama chuma cha juu cha goli.

Je kuna timu inayoweza kuishnda rekodi ya Ujerumani?

Huku mabingwa watetezi Ujerumani wakitolewa katika awamu ya kimakundi kwa mara ya kwanza tangu 1938, Urusi ndio timu iliofanikiwa zaidi katika mikwaju ya penalti.

Ni Mjerumani mmoja pekee kwa jina Uli Stielike katika mikwaju ya penalti ya kombe la Dunia kati ya West Germany na Ufaransa katika mechi ya nusu fainali ya 1982 aliyekosa penalti katika michuano ya kombe la Dunia .

Tangu wakati huo, Ujerumani imefanikiwa kufunga mikwaju 15 mtawalia na kushinda mikwaju yote minne walioshirikishwa.

Lakini licha ya kuondolewa mapema , Argentina huenda ikawapiku, likiwa taifa lenye rekodi nzuri ya upigaji wa penalti.

Lionel Messi may have missed from the spot against Iceland in the group stages, but his countrymen have a good record in shootouts, notching up four wins from five attempts.

Walishindwa wakati mmoja pekee 2006- cha kushangaza walishindwa na Ujerumani.

Upande mwengine , Uingereza ina rekodi mbaya ya upigaji wa mikwajju ya penalti, kitu ambacho hakimshangazi mtu yeyote ambaye ameifuatilia timu hiyo ya taifa.

Uingereza imepoteza mechi zake zote tatu ambazo ushindi wake uliamuliwa kwa mikwaju ya penalti wakifunga mikwaju saba kati ya 12 katika kombe la Dunia.

Shinikizo inayokuwepo

Upigaji wa mikwaju ya penalti hujulikana kama bahati nasibu, na bahati hutarajiwa kabla ya mpigaji wa kwanza kupiga mpira.

Mfumo uliopo sasa unafanya timu kupiga mikwaju hiyo ikibadilishana huku uamuzi kuhusu yule atakayepiga mpira wa kwanza ukifanywa kupitia shilingi.

Timu A inapiga kwanza halafu Timu B halafu tena Timu A na kuenedelea.

Upande utakaoshinda shilingi inaporushwa juu na kuanguka na kuamua kupiga wa kwanza ana fursa nzuri, huku timu za kwanza zikipata ushindi kwa asilimia 60.

Watafiti kutoka shule ya kiuchumi mjini London wamelaumu shinikizo ya kiakili ya kusalia nyuma kuathiri upigaji. Timu inayochukua nafasi ya pili kupiga penalti za kombe la dunia ina asilimia 69 ya kufunga huku timu inayopiga wa kwanza ikiwa na asilimia 73.