Dortmund: Hakuna mazungumzo ya kumuuza Aubameyang

Maelezo ya picha, Mshambuliaji wa Gabon na Dortmund Aubameyang

Mkufunzi wa Borussia Dortmund Peter Stoger anasema kuwa hakuna ombi la kumsajili Pierre-Emerick Aubameyang lililowasilishwa na Arsenal.

Mshambuliaji huyo wa Gabon ambaye ananyatiwa na the Gunners, hakusafiri na wachezaji wenzake kwa mechi ya Ijumaa dhidi ya Hertha berlin ambayo ilikamilika 1-1.

"hakuna mazungumzo yoyote katika meza kuhusu uhamisho wa Aubameyang ,yanayoendelea ni uvumi. alisema Stoger.

"Tunapanga na Pierre-Emerick Aubameyang na kuna vile atakavyorudi katia kikosi cha kwanza cha timu ."

Aubameyang pia alikosa mechi ya Jumapili iliotoka sare ya 0-0 dhidi ya Wolfsburg baada ya kukosa kuhudhuria mkutanoi wa timu.

Maelezo ya video, Pierre-Emerick Aubameyang

Mchezaji huyo mwenye urmi wa miaka 28 ni mshambuliai wa Dortmund mwenye magoli mengi msimu huu akiwa na mabao13 katika mechi 15 .