Mwanajeshi wa Marekani aliyeshiriki operesheni ya Maduro akamatwa baada ya kushinda kamari

Chanzo cha picha, Getty Images
Serikali ya Marekani inamshikilia wanajeshi mmoja aliyeshiriki katika operesheni ya kumkamata aliyekuwa rais wa Venezuela, Nicolás Maduro, kwa tuhuma za kutumia taarifa za siri kufanya biashara katika kamari za kidijitali maarufu kama Polymarket.
Mamlaka nchini Marekani imemfungulia mashitaka Gannon Ken Van Dyke, mwanajeshi wa kikosi maalum, kwa kutumia taarifa za siri kufanya biashara kwenye masoko yanayohusiana na mpango wa kumwondoa Maduro madarakani.
Serikali imesema kitendo hicho kinahesabika kama biashara kwa kutumia taarifa za siri chini ya sheria za shirikisho ni kosa la jinai.
Van Dyke, aliyekuwa akifanya kazi katika kambi ya Fort Bragg, North Carolina, anadaiwa kupata zaidi ya dola 409,000 kutokana na mchezo huo.
Unaweza kusoma pia:





