Iran yasema vikwazo vya Marekani ni 'ukiukaji wa masharti ya kusitisha mapigano'

Chanzo cha picha, Reuters
Jeshi la majini la Iran lilisema kwamba kuendelea kwa vikwazo vya Marekani kwenye bandari za Iran ni "ukiukaji wa masharti ya kusitisha mapigano".
Mapema mwezi huu Iran na Marekani zilikubaliana kusitisha mapigano kwa masharti ya wiki mbili, ambapo walikubaliana kwamba Meli zitaruhusiwa kupitia Mlango-Bahari wa Hormuz.
Njia muhimu ya meli imefungwa tena na Iran na jeshi la majini la Iran linasema itaendelea kufungwa hadi kizuizi cha meli na bandari za Iran kitakapoondolewa.
Katika taarifa yake ya hivi karibuni, Jeshi la Iran linasema taarifa zilizotolewa na Trump kwenye Mlango-Bahari wa Hormuz "hazina uhalali wowote".
Haijulikani wazi ikiwa taarifa hiyo inarejelea maoni maalum yaliyotolewa na rais wa Marekani.
Trump aliwaambia waandishi wa habari katika Ofisi ya Oval Jumamosi kwamba viongozi wa Iran wanataka kufunga mlango-bahari, lakini Marekani haitawaruhusu "kututishia".
Unaweza kusoma;



