Mkurugenzi Mkuu wa zamani wa Google athibitishwa kuwa mkurugenzi mkuu mpya wa BBC
Chanzo cha picha, EPA
Aliyekuwa
mtendaji mkuu wa Google Matt Brittin amethibitishwa kuwa mkurugenzi mkuu mpya
wa BBC.
Rais huyo wa
zamani wa kampuni ya Google barani Ulaya, Mashariki ya Kati na Afrika atachukua
nafasi ya Tim Davie, ambaye alisema alikuwa akijiuzulu mwezi Novemba kufuatia kesi
iliyohusu jinsi hotuba ya Rais wa Marekani Donald Trump ilivyohaririwa.
Mwenyekiti
wa BBC Samir Shah alisema Brittin, ambaye aliondoka Google mwaka wa 2025 baada
ya miaka 18, "analeta uzoefu wa kipekee BBC wa kuongoza shirika la ngazi
ya juu na tata sana kupitia mabadiliko".
Brittin,
mwenye umri wa miaka 57, alisema "nina hamu sana kuanza kazi hii",
akielezea kama "wakati halisi wa hatari, lakini pia fursa yenyewe".
Trump asema Iran 'inaogopa' kukubali kuwa kuna majadiliano huku Tehran ikikanusha ripoti hizo
Chanzo cha picha, Reuters
Waziri wa
Mambo ya Nje wa Iran Abbas Araghchi amesema katika mahojiano ya televisheni ya
taifa ya Iran kwamba kwa "siku kadhaa" Marekani "imeanza kutuma
ujumbe mbalimbali kupitia wapatanishi tofauti".
Lakini amesema
ukweli kwamba jumbe hizi "ziliwasilishwa kupitia nchi rafiki", na
kwamba Iran ilikuwa ikijibu kwa kusema "misimamo yao na kutoa
maonyo", "sio mazungumzo wala majadiliano, wala chochote cha aina
hiyo".
Araghchi pia
amesema kwamba sera ya Iran kwa sasa ni kuendelea "kujitetea", na
"hawana nia ya kujadiliana kwa sasa".
Anaongeza
kwamba, "Hii ni vita vya Israeli na watu wa eneo hilo na watu wa Marekani
wanalipa gharama yake."
Kilichofanyika
hivi karibuni kuhusu mazungumzo kati ya Marekani na Iran?
Kilichotokea
kufikia sasa:
Waziri wa Habari wa Ikulu ya Marekani
Karoline Leavitt amesema siku ya Jumatano, Rais Trump amekuwa akishiriki
katika "mazungumzo yenye tija" na Iran kwa siku tatu
zilizopita.
Pia alisema hatua hiyo ilikuwa
"imefanyika kwa haraka" na utawala wa Iran ulikuwa unatafuta
"njia ya kutokea"
Ujumbe huo ni tofauti kabisa na
sauti ya Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Abbas Araghchi, ambaye baadaye
alisema kwamba Iran " haina nia ya kufanya majadiliano kwa
sasa "
Alisema ujumbe
"umewasilishwa kupitia nchi rafiki", lakini mabadilishano haya
"si mazungumzo wala majadiliano, wala kitu chochote cha aina
hiyo"
Bila kukata tamaa, Trump
anasisitiza kwamba Iran "inajadiliana", akisema " wanaogopa
kusema hivyo kwa sababu wanafikiri watauawa na watu wao
wenyewe". Aliongeza: "Pia wanaogopa watauawa na sisi"
Pia kumekuwa na ripoti
zinazokinzana kuhusu mapendekezo ya kukomesha vita. Siku ya Jumatano,
kulikuwa na ripoti kwamba Iran ilikuwa imepokea mpango wa vipengele 15 kutoka
Marekani kwa ajili ya kufikia makubaliano ya kusitisha mapigano.
Kwa upande wake, "afisa
mwandamizi wa usalama wa kisiasa" wa Iran alinukuliwa na mtangazaji
wa serikali Press TV akisema walikuwa na masharti matano ya kukomesha
vita, ikiwa ni pamoja na malipo ya "fidia ya vita" na kumaliza
vita katika nyanja zote.
Wakati huo huo, mapigano
yanaendelea - moshi ulionekana ukitoka kwenye kituo cha umeme cha
Israeli baada ya kuripotiwa kwa shambulio la kombora la Iran, huku mifumo
ya ulinzi wa anga ya Iran ikisikika mjini Tehran.
Hujambo. Karibu katika habari zetu za moja kwa moja kuhusu vita vya Iran huku kukiwa na ripoti zinazokinzana kuhusu mazungumzo kati ya Marekani na Iran. Tarehe ni 26/03/2026.