Tetemeko la Ardhi Uturuki: Ulimwengu waungana baada kukumbwa na janga

Wakati Uturuki na Syria zikianza kutathmini uharibifu uliosababishwa na tetemeko la ardhi lenye kipimo cha 7.8 ambalo hadi sasa limesababisha vifo vya watu wasiopungua 4,800, nchi mbalimbali duniani zimejipanga kusaidia juhudi za uokoaji.

Mvua na theluji inaathiri waokoaji, lakini timu maalum kutoka mataifa mengi, ikiwa ni pamoja na Italia, Marekani, Israel na Taiwan - ziko njiani.

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Iraq inatoa msaada kwa Syria. Vikosi vya usalama vilichakata vifaa kutoka kwa shirika la misaada la Red Crescent ili kutuma katika nchi jirani

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Wanajeshi wa Iraq na wafanyakazi wa shirika la Red Crescent wakipakia vifaa hivyo kwenye lori.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Waokoaji kutoka Taiwan wanajipanga kusaidia katika oparesheni ya kutafuta na kuokoa manusura nchini Uturuki.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Kundi maalumu la wazima moto kutoka Jamhuri ya Czech itasaidia kutafuta manusura kwenye vifusi nchini Uturuki.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Kundi la Czech USAR lina mafunzo maalum ya kutafuta watu ambao huenda wamezikwe kwenye vifusi.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Maafisa wa kundi la utafutaji na uokoaji ya Uholanzi walipaswa kusafiri kutoka Eindhoven kutoa usaidizi nchini Uturuki.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Takriban wazima moto 50 na wafanyikazi wa matibabu waliondoka Pisa, Italia, kusaidia katika mpaka wa Syria na Uturuki katika juhudi za uokoaji.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Rome inasema safari zaidi za ndege zitafuata baada ya wazima moto kuwasili, wakileta wafanyikazi wa matibabu na vifaa vya Uturuki.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Waziri Mkuu wa Ugiriki siku ya Jumatatu aliahidi kufanya "kila juhudi" kusaidia jirani yake Uturuki. Walituma vifaa na waokoaji kuelekea Uturuki siku hiyo hiyo yamkasa.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Ugiriki na Uturuki kihistoria zimekumbwa na migogoro mbalimbali ya mipaka na kitamaduni.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Vikosi vya uokoaji vya Bulgaria vilisambazwa katika Lango la Mpaka wa Kapikule kusaidia katika juhudi za kutoa misaada kote Uturuki.

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Kitengo cha kutoa msaada cha jeshi la ulinzi la Israeli lilielekea Uturuki kusaidia juhudi za uokozi baada ya tetemeko la ardhi. Waziri Mkuu wa Israel pia alisema ameidhinisha kutumwa msaada kwa Syria - ambayo serikali yake haitambui Israel.

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Israel ilipokea ombi la kuisaidia Syria kupitia njia za kidiplomasia. Lakini Damascus ilikataa kuomba msaada.

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Rais wa Marekani Joe Biden alisema maafisa wanajitahidi kuondoka haraka iwezekanavyo ili kuanza kusaidia juhudi za utafutaji na uokoaji za Uturuki.

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Marekani ilisema itatuma timu mbili za utafutaji na uokoaji zenye takriban watu 80 kila moja.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Katika ubalozi wa Uturuki mjini Moscow, kumewekwa shada la maua. Pia kuna mshumaa umewashwa na kando yake kumebandikwa karatasi iliyoandikwa ujumbe "Pole kwa Uturuki". Urusi imetoa msaada kwa Uturuki na Syria.

Picha zote zina haki miliki.