John F Kennedy: Wakati rais wa Marekani alipokutana na Mwalimu Nyerere na wapiganiaji uhuru wengine wa Afrika

Chanzo cha picha, JFK Presidential Library

Maelezo ya picha, Rais John F Kennedy alikutana na Rais wa kwanza wa Ghana Kwame Nkrumah katika Ikulu ya White House mwezi Machi 1961

Katika msururu wa barua za wandishi wa Afrika ,mwandishi wa Sierra Leone-Gambia Ade Daramy amezama na kuibuka na picha za rais wa Marekani John F Kennedy ambaye alikuwa mstari wa mbele kuanzisha uhusiano wa taifa lake na Afrika .

Kabla ya Kennedy kuwa rais mwaka wa 1961 nchi yake haikuwa imechukua hatua ya kuelewa mageuzi makubwa yaliokuwa yakifanyika Afrika

Kufikia wakati alipouawa mwaka wa 1963 tasiwra hiyo ilikuwa imebadilika sana.

Katika muda wake mfupi afisini Kennedy alikuwa amepokea kila kiongozi aliyekuwa akipigania uhuru wan chi yake katika Ikulu ya White House nahata viongozi ambao kwa wakati huo walikuwa wakiongoza nchi zao .

Chanzo cha picha, JFK Presidential Library

Maelezo ya picha, Rais wa Senegal Léopold Sédar Senghor, alikuwa kiungo muhimu katika vuguvugu la kupinga ukoloni katika mataifa ya Afrika yanayozungumza kifaransa, na alizuru Washington Novemba 1961

Mwaka mmoja kabla ya kuwa rais mataifa 17 ya Afrika yalikuwa yamepata uhuru na kwa sabau alifahamu mambo yalikuwa yakibadiliska Kennedy alikuwa ameanzisha uhusiano nao na kuanza kuyaunga mkono mataifa ya Afrika .

Chanzo cha picha, JFK Presidential Library

Maelezo ya picha, Kiongozi mwingine wa Afrika Julius Nyerere, ambaye wakati huo alikuwa Waziri Mkuu wa Tanganyika, alizuru White House Juali 1961, miezi mitano baada ya kupata uhuru kutoka kwa Uingereza

Sera hiyo ya uhusiano wa kidiplomasia ilidumu kwa muda mrefu isipokuwa wakati wa utawala wa rais Donald Trump ambaye hakuwa na uhusiano wa karibu sana na Afrika na hata lugha yake alipozungumzia nchi za Afrika ilisaliti msimamo wake kuhusu alivyoataka Marekani kuhusiana na nchi za Afrika.

Mtangaluzi wa Dwight D Eisenhower pia hakuwa na sifa nzuri kuhusu uhusiano wake na nchi za Afrika.

Aliamuambia rais wa Togo Sylvanus Olympio, kwamba sababu ya Marekani kuwa na balozi mmoja kuzishughulikia Togo na Cameroun ni kwa sababu hakutaka mabalozi wake 'kuishi katika mahema'

Chanzo cha picha, JFK Presidential Library

Maelezo ya picha, Rais wa President Sylvanus Olympio alipopokelewa katika uwanja wa ndege na Kennedy mwezi Machi 1962

Wakati wa kampeini za uchaguzi wa mwaka wa 1960 Kennedy alikosoa utawala wa Eisenhower kwa kutelekeza maazimio ya watu wa Afrika na kwamba Marekani ilifaa kuwa upande unaopinga ukoloni.

Chanzo cha picha, JFK Presidential Library

Maelezo ya picha, Emperor Haile Selassie wa Ethiopia, mmoja wa wanzilishi wa Muungano wa Afrika mwezi Mei 1963, alikaribishwa Washington na mama taifa Jacqueline Kennedy na rais wa Marekani Oktoba mwaka huo

Alipochukua uongozi Kennedy aliwaalika viongozi wa Afrika White House pamoja na Jackie Kennedy, alimsalimia kila mmoja wao akiwemo Emperor wa Ethiopia Haile Selassie na Mfalme Hassan IV wa Morocco - walipowasili nchini humo.

Chanzo cha picha, JFK Presidential Library

Maelezo ya picha, Haile Selassie aliendeshwa kwa gari katika barabara za bunge la Marekani

Pia kuwa na gwaride la heshima ,dhifa za chakula na ziara za kwenda kumbi kubwa za tamasha za muziki katika sehemu zenye historia .

Chanzo cha picha, JFK Presidential Library

Maelezo ya picha, Rais wa kwanza wa Ivory Coast' Félix Houphouët-Boigny, na mke wake Marie-Thérèse Houphouët-Boigny, walipoalikwa kwa karamu ya chakula cha jioni katika ziara yao ya kwanza 1962

Ziara hizo ziliangaziwa katika vyombo vya habari na wananchi walihimizwa kujitokeza na kushangilia.

Chanzo cha picha, JFK Presidential Library

Maelezo ya picha, Kiongozi wa Ethiopia Haile Selassie alikaribishwa Marekani kwa kuandaliwa gwaride la heshima

Kulikuwa na njama ya kisiasa katika yote hayo. Muungano wa Kisovieti pia ulikuwa ukiendeleza juhudi kama hizo katika nchi za Kiafrika kwa kujitenga na Wakoloni wa zamani wa nchini hizo.

Alipoingia madarakani, Kennedy aligundua haraka umuhimu wa kuwa karibu na mataifa yanayoibuka Barani Afrika.

Chanzo cha picha, JFK Presidential Library

Maelezo ya picha, Rais John F. Kennedy akitoa hotuba yake baada ya kuwasili kwa Rais wa Guinea, Ahmed Sékou Touré.

Kennedy hata hivyo alionekana kujitolea kabisa kuiendeleza Afrika na watu wake.

Chanzo cha picha, JFK Presidential Library

Maelezo ya picha, Wari Mkuu wa kwanza wa Nigeriar, Abubakar Tafawa Balewa, alifanya mazungumzo na Kennedy katika Ikulu ya White House mwezi Julai, 1961

Wakati alipouawa bara la Afrika liliathiriwa sana na mauaji yake na hasa ikizingatiwa kwamba mrithi wake Johnson, hakuwa na msimamo wa kuendeleza uhusiano huo kati ya Marekani na Afrika.

Chanzo cha picha, JFK Presidential Library

Maelezo ya picha, Rais John F. Kennedy alipokutana na William V.S. Tubman, Rais wa Liberia

Kuuawa kwa shujaa wa ukombozi wa Congo Patrice Lumumba huku shirika la CIA likishukiwa kuhusika ni kumbusho kwamba vita baridi vya wakati huo vilivyohusisha muungano wa Soviet vilikuwa pia vikiendelezwa barani Afrika.

Chanzo cha picha, JFK Presidential Library

Maelezo ya picha, Rais wa kwanza wa Congo-Brazzaville Fulbert Youlou alizuru Washington mwezi Juni 1961

Miaka 60 baadaye Joe Biden ameanza tena kuchonga upya uhusiano wa kidiplomasia kati ya Marekani na Afrika. Kupitia taarifa mapema mwezi huu alisema Marekani iko tayari kuwa 'Mshirika wa Afrika kwa kuisaidia na kunufika kwa pande zote mbili'

Maneno ya Biden yalikariri kujitolea kwa Kennedy kuboresha uhusiano huo - na sasa kinachongojewa ni iwapo vitendo vitaambatana na tamko hilo.

Picha za Robert Knudsen, Cecil Stoughton, Abbie Rowe, Picha za White House, ziliwasilishwa na Maktaba ya Rais John F Kennedy na makavazi ya, Boston