Tazama baadhi ya picha bora Afrika 2020

Baadhi ya picha za Afrika zilizotia fora mwaka 2020:

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Januari, kundi la nzige lilivamia sehemu kubwa ya Afrika Mashariki ikiwemo eneo la Samburu nchini Kenya.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Februari 2020, sherehe ya kupaka rangi ilifanyika eneo la Tigray nchini Ethiopia mji wa Mekelle - ambapo hata farasi hakuachwa nyuma. Hata hivyo, baadaye mji huo ulikumbwa na vita.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Mnamo mwezi Machi, virusi vya ugonjwa wa corona vikasambaa kote duniani. Mwanaume huyu Gonzaga Yiga kutoka nchini Uganda alichukua jukumu binafsi kuelimisha umma katika mji mkuu wa Kampala kuhusu hatua za kuchukuliwa kupunguza maambukizi.

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Taarifa za ugonjwa wa corona zilipoendelea kusambaa, ugonjwa huo ukapata umaarufu nchini Kenya kiasi cha kubuniwa msongo uliopewa jina corona katika saluni za mjini Nairobi

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha, Watoto hawa wamechuchumaa katika mduara uliochorwa kwenye kituo cha basi mjini Kigali nchini Rwanda kama njia moja ya kuhakikisha watu hawakaribiani.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Mnamo mwezi Juni, raia nchini Mali waliandamana walidai kung'atuliwa madarakani kwa Rais Ibrahim Boubacar Keïta. Miezi miwili baadaye, akatolewa madarakani kupitia mapinduzi ya kijeshi.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Waislamu kote barani Afrika wakisherehekea sikukuu ya Eid al-Adha mnamo mwezi Julai. Kwa wakulima kama kijana huyu wa Senegal mjini Dakar, inamaanisha kuosha kondoo kabla ya kuwapeleka sokoni kuwauza.

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha, Mchimbaji madini mdogo mdogo Saniniu Kuryan Laizer nchini Tanzania alikuwa milionea kwa siku moja mnamo mwezi Juni kwa kuuza mawe mawili yaTanzanite kwa thamani ya dola milioni 3.4 sawa na (£2.6m), aliuza tena jiwe jingine la thamani ya milioni 2 mnamo mwezi Agosti.

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Sokwe katika mbuga ya taifa ya Virunga Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo akinyonyesha watoto wake wawili mnamo mwezi Septemba.

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Maandamano kwa jina Sars yaliyotokea mjini Lagos na kote nchini Nigeria dhidi ya ukatili unaotekelezwa na polisi mnamo mwezi Oktoba yalisababisha kuvunjwa kwa kikosi maalum cha polisi.

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha, Novemba, makumi ya maelfu ya watu nchini Ethiopia katika eneo la Tigray walitoroka eneo hilo na kuingia Sudan kutafuta usalama.

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha, Na mwisho ni harusi iliyokuwa maarufu mitandaoni Afrika Kusini mnamo mwezi Desemba, baada ya serikali kupiga marufuku uogeleaji katika fukwe za bahari za umma kuzuia wimbi la pili la virusi vya corona.

Picha kwa hisani ya AFP, Getty Images na Reuters