Afrika kwa picha wiki : kati ya tarehe 23-29 Agosti 2019

Baaadhi ya picha bora zilizochukuliwa kutoka maeneo mbali mbali ya bara la Afrika na kwingineko , wiki hii:

Chanzo cha picha, EPA

Maelezo ya picha, Msichana huyo alipiga sarakasi ya nyuma nchini Afrika Kusini katika moja ya maeneo ya michezo katika mji wa Alexandria Johannesburg alipokuwa shule Jumanne

Chanzo cha picha, EPA

Maelezo ya picha, Mwanasarakasi Phaphama Nxumalo akionekana siku hiyo hiyo akionyesha wenzake umahiri wake wa kujirusha hewani

Chanzo cha picha, EPA

Maelezo ya picha, Huko huko Johannesburg, mwanamieleka akiwa mbele ya mashabiki wake Jumamosi..

Chanzo cha picha, EPA

Maelezo ya picha, Shabiki wa mieleka wa Afrika kusini hapa wakiwa katika maombi

Chanzo cha picha, EPA

Maelezo ya picha, mwanamitindo mzaliwa wa Somalia na mjasiliamali Iman akiingia katika zulia jekundu katika tamasha la kimataifa la filamu la Venice International Nchini Italia Jumatano

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha, Katika tamasha hilo hilo alikuwepo mwanamitindo wa Afrika Kusini Candice Swanepoel hapa akiwa tayari kupigwa picha

Chanzo cha picha, Redferns/Getty Images

Maelezo ya picha, Nyota wa Afrobeats Mnaigeria D'banj aligonga vichwa vya habari kwa shoo yake katika Brixton Academy mjini London Jumapili . Mapema wiki hiyo , aliiambia BBC kuwa yeye na mkewe wanatarajia kupata ,mtoto mwingine , mwaka mmoja baada ya mtoto wao wa kwanza kufariki

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha, Siku ya Alhamisi mjini Abidjan, Ivory Coast, watu wakishiriki katika sherehe za kitamaduni za "Fatchue"

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha, Tamasha hilo ni kilele cha shughuli ya kitamaduni ya kuwapa majukumu ya uongozi wa kijamii vijana

Chanzo cha picha, SOPA Images/ Getty Images

Maelezo ya picha, mwanamuzi wa Uganda aliyegeuka kuwa mwnasiasa mbunge MP Bobi Wine akibarikiwa na makasisi wa kikatoliki Jumapili katika tukio la kampeni . Kiongozi huyo wa upinzani anapanga kugombea dhidi ya rais wa muda mrefu Yoweri Museveni katika uchaguzi wa mwaka 2021

Chanzo cha picha, EPA

Maelezo ya picha, Katika eneo la kati mwa kenya siku ya Ijuma, walinzi wa wanyamapori walimsindikiza faru mweupe aliyesalia ili kutoa mayai yake ya uzazi . Inatumainiwa kuwa mayai hayo ili kuendeleza kizazi chao.

Picha kutoka Reuters, EPA, Getty Images, AFP, Redferns na SOPA Images