Jordan imezindua makavazi ya kwanza ya kijeshi chini ya bahari

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha, Gari al kivita aina ya kifaru iliyozamishwa futi 92 chini ya bahari

Jordan imezindua makavazi yake ya kwanza ya kijeshi chini ya bahari katika pwani ya Aqaba.

Katika hafla ya uzinduzi huo siku ya Jumatano, ufalme huo ulizamisha magari kadhaa ya kivita pamoja na helikopta kijeshi chi ya bahari.

Magari hayo yameegeshwa kana kwamba yako vitani yamewekwa katika miamba ya matumbawe yaliopo chini ya bahari nyekundu.

Mamlaka zinasema onyesho hilo ni mbinu mpya ya utalii kwa wageni wanaozuru taifa hilo.

Miamba ya matumbawe katika sehemu ya Kaskazini mwa Bahari nyekundu ni kivutio kikubwa kwa wapiga mbizi na watalii wengine.

Halmashauri ya eneo maalum la kiuchumi la Aqaba (ASEZA) imeongeza kuwa itajumuisha aina tofauti ya michezo katika "mazingira hayo ya maonesho".

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Helikopta ya kijeshi, iliyotolewa na kikosi cha jeshi la hewa la Jordan, ilikuwa moja ya vyon=mbo vya kijeshi vilivyozamishwa chini ya bahari

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Halmashauri ya eneo maalum la kiuchumi ya Aqaba imeiambia Jordan Times kuwa ma vifaa hatari vilitolewa ndani ya magari hayo kabla yazamishwe

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Watakaoweza kuzuriu makavazi hayo ni wapiga mbizi wanaotumia vifaa maalum na wataliii wanaotumia maboti maalum yalio na sakafu ya kio

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Wapiga mbizi wakitoka ndani ya maji baada ya kuzamisha magari ya kijeshi chini ya bahari nyekundu katika pwani ya Aqaba

Picha zotye zina haki miliki.