Afrika kwa picha wiki hii: Tarehe 12 hadi 18 Julai 2019

Baadhi ya picha bora zilizopigwa kutoka maeneo mbali mbali ya Afrika wiki hii:

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha, Jumamosi nchini Misri , vumbi likipangushwa kwenye sanamu iliyovumbuliwa yapata kilomita 40 kutoka mji mkuu Cairo.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, katika siku hiyo hiyo picha hii ya mpiga mbizi ilichukuliwa katika eneo la bahari lenye mawimbi makubwa kwenye tukio michezo ya baharini la Corona Open J-Bay nchini Afrika Kusini

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Waogeleaji wanawake wa Misri waliliwakilisha taifa lao katika mashindano ya dunia ya kuogelea nchini Korea Kusini Jumatano

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha, Katika siku hiyo hiyo katika michezo ya kombe la mataifa ya Afrika, mchezaji Anice Badri wa Tunisia akiudhibiti mpira wakati wa mechi yao dhidi ya Nigeria mjini Cairo

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Nchini Sierra Leone, wanafunzi hawa marafiki wa kike wakitembea chini ya mwavuli mmoja walipokuwa wakielekea nyumbani baada ya masomo Ijumaa

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha, Msanii wa muziki wa vichekesho qaitwae Moulouk el-Tawaef, akiwa katika shoo katika tamasha la mwaka la kimataifa la Tunisia njini Tunis

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha, Mwanamuziki Mfaransa mwenye asili ya Mali Aya Nakamura akiwatumbuiza mashabiki wake katika tamasha la muziki la wazungumzaji wa Kifaransa kusini- magharibi mwa Ufaransa

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha, Jumamosi, waandamanaji waliingia mitaani tena katika mji mkuu wa Sudan Khartoum, ambako baraza la chama tawala na upinzani walisaini mkataba wa kugawana madarakana siku kadhaa baadae

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Mwewe hawa walionekana wakipaa juu ya mji wa london mchana walipokuwa njia ni kuelekea katika bara la Afrika kama wafanyavyo kila ifikapo katikati ya mwezi Julai kila mwaka , kulingana na shirika la ulinzi wa ndege la uingereza

Picha kwa hisani ya , Getty Images na AFP