Kwa picha: Watu 2 wanaofanana na Rodrigo Duterte na Kim Jong-un wazua vioja Hong Kong

Chanzo cha picha, EPA

Huenda ukadhania kwamba rais wa Ufilipino Rodrigo Durtete na mwenzake wa Korea Kaskazini Kim Jong Un walikuwa pamoja katika barabara za mji wa Hong Kong, wakipiga picha na kula pamoja chakula cha jioni katika mgahawa mmoja.

Lakini uchunguzi wa kina ulibaini kwamba wawili hao walikuwa watu waliowaiga viongozi hao wawili.

Kutana na jamaa anayejiita Cresencio Extreme anayefanana na Durtete na Howard X anayefanana na Kim Jong un.

Chanzo cha picha, EPA

Maelezo ya picha, Wawili hao waliobeba bunduki bandia walisalimiwa na wafanyikazi na raia walipowasili katika mgahawa huo wa kuku karanga au Fried Chicken Restaurant

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Walihudhuria ibada ya Jumapili katika kanisa la St Joseph's huku Cresencio Extreme (kushoto)akiwa amevalia shati jeupe ambalo hupendwa sana na rais Durtete

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Mtu huyo anayefanana na rais Durtete alizua kihoja na mkanganyiko katika kanisa hilo katikati ya mji wa Hong Kong baada ya kuzungukwa na waumini

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, "Je huyu ni Durtete?'' Wengine hawakukubaliana naye huku raia huyo akionekana kuwa mdogo kwa umri kuwa rais wa Ufilipino pamoja na mwenzake anayemuiga rais wa Korea Kaskazini Kim Jong Un.

Chanzo cha picha, EPA

Maelezo ya picha, Wawili hao walizidi kuwakanganya raia waliopoonekana wakila chakula cha jioni katika mgahawa wa Hong Kong siku ya Jumapili.

Chanzo cha picha, EPA

Maelezo ya picha, Mr Duterte {kushoto) na muigaji wake

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Bwana Kim (kushoto) na muigaji wake kulia