Mahakama Kenya yaagiza Miguna aachiliwe

Chanzo cha picha, AFP/Getty

Maelezo ya picha, Awali Bw Odinga alijaribu kumsaidia Bw Miguna kuondoka uwanja wa ndege bila mafanikio

Jaji wa mahakama kuu Roseline Aburili ameagiza wakili wa upande wa upinzani Miguna Miguna kuachiliwa kutoka kwa uwanja wa ndege wa kimataifa Jomo Kenyatta.

Miguna ameagizwa kutokea mahakamani kesho Jumatano sasa tatu saa za Afrika Mashariki.

Maelezo ya picha, Maamuzi ya mahakama

Bw Miguna Miguna alijaribu kurejea Kenya Jumatatu lakini akazuiwa kuingia baada yake kudaiwa kutowasilisha pasipoti ya Canada ambayo ilitumiwa kumsafirisha kwa nguvu hadi Canada.

Wakili huyo alisisitiza kwamba ni raia wa Kenya na hafai kuzuiwa kurejea.

Chanzo cha picha, Waikwa Wanyoike

Maelezo ya picha, Hali ilivyokuwa katika uwanja wa ndege wa Jomo Kenyatta siku ya Jumanna, Miguna alikesha kwenye uwanja huo.

Bw Miguna, aliyekuwa amewasili uwanja wa ndege wa kimataifa wa Jomo Kenyatta mwendo wa saa nane adhuhuri, alikesha kwenye uwanja huo.

Maafisa walijaribu kumsafirisha kutoka uwanja huo kwa kutumia ndege ya shirika la Emirates ambayo ilikuwa inaelekea Canada kupitia Dubai.