Afrika kwa Picha: 30 Desemba 2017-4 Januari 2018

Mkusanyiko wa picha bora kutoka Afrika na kuhusu Waafrika wiki hii:

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha, Jumatano, wahudumu hawa wa treni katika reli ya Addis Ababa-Djibouti walijiweka sawa kupigwa picha baada ya kuwasili kwa treni ya kwanza ya kibiashara katika mji wa Addis Ababa kutoka kituo cha reli cha Nagad nchini Djibouti

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha, Mkesha wa mwaka mpya, watu walikusanyika kwa sherehe za kuukaribisha Mwaka Mpya katika mji wa Victoria Falls nchini Zimbabwe…

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha, Sherehe hizo katika shule ya Victoria Falls Farm zilifikisha kikomo sherehe za siku tatu za kufungwa mwaka katika mji huo maarufu sana kwa utalii…

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha, Nchini Kenya, ilikuwa ni shangwe na nderemo kwa wakazi waliokuwa wamekusanyika nje ya jumba la mikutano la KICC, Nairobi kujionea maonesho ya fataki...

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha, Afrika Kusini, simu zilifanyishwa kazi ya ziada kupiga picha za fataki katika uwanja wa Mary Fitzgerald, Johannesburg kuukaribisha Mwaka Mpya…

Chanzo cha picha, EPA

Maelezo ya picha, Mapema Jumapili katika mji wa Cape Town, wanaume wanaonekana wakicheza nyimbo katika ufukwe wa Scarborough kuuaga mwaka 2017...

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Siku iliyofuata, mamia walifika kwenye fukwe mbalimbali nchini humo kuukaribisha mwaka 2018. Hapa ni ufukwe wa Durban …

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha, Kwa waumini wa kanisa la Nazareth Baptist linalofahamika pia kama Shembe ilikuwa ni siku ya utakaso. Mahujaji walielekea katika mlima wa Nhlongakazi kaskazini mwa Durban kwa ibada.

Chanzo cha picha, EPA

Maelezo ya picha, Jumanne, watu waliokuwa wamejipamba walishiriki kwenye sherehe ya kanivali ambayo asili yake ni utamaduni wakati wa utumwa eneo hilo ambapo watumwa walikuwa wanapewa ruhusa kupumzika siku ya Mwaka Mpya

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Mjini Abuja, Nigeria siku ya Mwaka Mpya, watoto wanaonekana wakicheza kwenye uwanja wa Millennium

Chanzo cha picha, EPA

Maelezo ya picha, Siku hiyo, wakimbizi kutoka Eritrea wanavuta viko vya maji nje ya mgahawa wa muda katika kituo cha kuwazuilia wakimbizi kwa muda karibu na Nitzana, jangwa la Negevn katika mpaka wa Israel na Misri

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Jumapili, Rais Omar al-Bashir anaonekana akiwasili katika ikulu Khartoum kuwahutubia wananchi wakati wa maadhimisho ya miaka 62 tangu kujinyakulia uhuru kwa taifa hilo.

Chanzo cha picha, EPA

Maelezo ya picha, Liberia, wakazi wanatazama matokeo ya duru ya pili ya uchaguzi Jumapili mjini Monrovia. George Weah alishinda.

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha, Na siku hiyo, ng'ombe hawa wanaonekana wakiwa wametulia ufukweni visiwani Zanzibar, Tanzania

Picha kwa hisani ya AFP, EPA, PA, Reuters na Getty Images