Misri yagundua makaburi ya kale yenye miili huko Luxor

Chanzo cha picha, EPA

Maelezo ya picha, Mwili huo wa binadamu unaaminiwa kuwa ule wa afisa kutoka ufalme wa Misri wa miaka 3,500 iliyopita.

Wana akiolojia nchini Misri wameonyesha vitu kadhaa ukiwemo mwili wa binadamu uliohifadhiwa kutoka kwa moja ya makaburi ambayo hayakuwa yamekaguliwa kwenye mji wa kale wa Luxor

Mwili huo wa binadamu unaaminiwa kuwa ule wa afisa kutoka ufalme wa Misri wa miaka 3,500 iliyopita.

Makaburi hayo yako eneo la Draa Abul Naga necropolis, eneo ambalo ni maarufu kwa mahekalu yake na makaburi.

Eneo hilo liko karibu na bonde la wafalme ambapo wengi wa Pharao wa Misri walizikwa.

Wizara inayohusika mambo ya kale nchini Misi ilisema kuwa makaburi hayo yalikuwa yamegunduliwa na mwanaakiolojia wa Ujerumani miaka ya tisini lakini ilibaki imefungwa hadi hivi karibuni.

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha, Michoro ilyopatikana ndani ya kaburi

Chanzo cha picha, EPA

Maelezo ya picha, Vifaa hivi navyo vilipatikana kwenye kaburi