Trump aitaka Urusi kuwacha kuivuruga Ukrain

Chanzo cha picha, EVN

Maelezo ya picha, Trump (kushoto) na rais wa Poland Andrzej Duda

Rais wa Marekani Donald Trump ametoa wito kwa Urusi kuacha kuivuruga Ukrain na nchi zingine, na kuacha kuungia mkono tawala dhalimu kami zile za Styria na Iran.

Akiongea akiwa mji mkuu wa Poland Warsaw, Trump aliitaka Urusi kujiunga na mataifa yenye kuwajibika.

Urusi imepinga matamshi hayo ya Trump.

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Bwana Trump akiwasili Hamburg kwa mkutano wa G20

Rais huyo wa Marekani amesafiri kuenda mjini Hamburg kuhudhuria mkutano wa G20 ambapo atakutana na rais wa Urusi kwa mara ya kwanza.

Mjini Warsaw alihutubia umati mkubwa uliokuwa ukimshangilia

Aliisifu Poland kama nchi iliyo tayari kulinda uhuru wa magharibi.

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Watu wanaosikiliza hotuba ya trump Poland

Bwana Trump aliitaka Urusi kuungana na nchi zinaowajibika katika vita dhidi ya adui mmoja.

Msemaji wa serikali ya Urusi Dmitry Peskov alisema kuwa Urusi haijakubali kuwa inavuruga eneo hilo.

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha, Waziri mkuu wa Uingereza Theresa May na rais wa Marekani Donald Trump wakikejeliwa Hamburg on Thursday

Trump ametofautiana na baadhi ya nchi za ulaya kuhusu mabadiliko ya hali ya hewa na biashara,

Mashirika ya kutoa misaada yatarajiwa kufanya maandamano mjini Hamburg kuwakata viongozi kujitahidi zaidi kumaliza kutokuwepo usawa.

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Waandamani wawasili kwa traini mjini Hamburg

Chanzo cha picha, EPA

Maelezo ya picha, Melania Trump (kushoto) akiwa na mama wa taifa nchini Poland Agata Kornauser-Duda