Tetesi za soka Ulaya: Zidane kuinoa Ufaransa, De Zerbi kutua Spurs

Chanzo cha picha, Getty Images
Kocha wa zamani wa Real Madrid, Zinedine Zidane, amekubali kuwa kocha wa timu ya taifa ya Ufaransa baada ya kumalizika kwa fainali za Kombe la Dunia mwaka huu. Zidane, mwenye miaka 53, anatarajiwa kuchukua nafasi ya Didier Deschamps (ESPN).
Kocha wa zamani wa Brighton & Hove Albion na Marseille, Roberto De Zerbi, yuko tayari kuwa kocha mkuu wa kudumu wa Tottenham Hotspur iwapo klabu hiyo itasalia Lgi kuu ya England (Telegraph).
Winga wa Manchester United na England Jadon Sancho, ambaye kwa sasa yuko kwa mkopo Aston Villa, amefanya mazungumzo na Borussia Dortmund kuhusu uwezekano wa kurejea Bundasliga kwa uhamisho wa bure, huku mchezaji huyo mwenye miaka 25 akiwa tayari kupunguza mshahara wake (Sky Sports Deutschland).
Manchester United inamtaka beki wa kushoto Alphonso Davies kutoka Bayern Munich, huku klabu hiyo ya Bundesliga ikiwa tayari kusikiliza ofa kwa ajli ya mchezaji huyo mwenye miaka 25 (CFBayerninsider).

Chanzo cha picha, Getty Images
Uongozi wa Newcastle United bado una imani na kocha Eddie Howe licha ya presha, huku mabadiliko makubwa ya wachezaji yakitarajiwa katika dirisha la usajili la majira ya kiangazi (Mail).
Beki wa kulia wa Chelsea, Josh Acheampong (19), anasakwa na Crystal Palace huku kukiwa na tetesi za kutaka kuondoka Stamford Bridge (Football Insider).
Manchester United bado haijaanza mawasiliano na makocha wanaowania nafasi ya ukocha wa kudumu, huku uongozi wa klabu hiyo ukipanga kutokuharakisha uamuzi wa kumpata kocha mpya (Sky Sports).
Kiungo wa Leeds United na Japan, Ao Tanaka (27), anawindwa na klabu za Ujerumani Schalke 04 na Hannover 96 (Teamtalk).
Manchester United pia inamnyemelea nahodha wa Newcastle United, Bruno Guimarães, ambapo ripoti kutoka Brazil zinaeleza kuwa anaweza kuuzwa kwa pauni milioni 60 (Sports Illustrated).
Mshambuliaji wa Ufaransa Antoine Griezmann (35) anatarajiwa kuondoka Atletico Madrid baada ya miaka 10 na kujiunga na klabu ya MLS, Orlando City (Times).













