Tetesi za soka Ulaya: Arsenal yamtaka Franca

Wesley Franca

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Wesley Franca
Muda wa kusoma: Dakika 2

Arsenal wameongeza juhudi za kusaka beki wa kulia, huku nyota wa Roma mwenye umri wa miaka 22 Wesley Franca akitajwa kuwa chaguo lao kuu. (Teamtalk)

Liverpool wanaongoza mbio za kumsajili kiungo wa Real Madrid Eduardo Camavinga, mbele ya Chelsea, baada ya kufanya mazungumzo mara mbili na wawakilishi wake. (Caught Offside)

Kocha wa Barcelona Hansi Flick amesema hana uhakika kuhusu mustakabali wa Marcus Rashford, ambaye yupo kwa mkopo akitokea Manchester United, huku klabu hiyo ikiwa na chaguo la kumsajili kwa pauni milioni 26. (Manchester Evening News)

Arsenal wako na presha kubwa ya kuuza wachezaji katika dirisha la majira ya joto, huku wachezaji wachache tu wakichukuliwa kuwa hawagusiki. (Telegraph)

Winga wa Barcelona Raphinha amesema hatarajii kuondoka klabuni hapo kabla ya mwisho wa msimu wa 2026-27 licha ya kuvutiwa na klabu za Saudi Arabia. (Sport)

a

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Raphinha

Kiungo wa Newcastle United Bruno Guimaraes ameonyesha atasalia klabuni hapo, bila kushinikiza kulipwa pesa nyingi na kuwa mchezaji anayelipwa pesa nyingi zaidi. (Newcastle Chronicle)

Jaribio la Fulham kumsajili mshambuliaji wa PSV Eindhoven Ricardo Pepi limesitishwa licha ya kufanyiwa vipimo vya afya. (Fabrizio Romano)

Hakuna mchezaji wa Chelsea aliyeomba kuondoka licha ya changamoto za matokeo msimu huu. (Mail+)

Manchester City hawana mpango wa kumuuza Erling Haaland licha ya kutakiwa na vilabu vya Barcelona na Real Madrid. (Football Insider)

Juventus wanachunguza uwezekano wa kumsajili beki Antonio Rudiger, ambaye mkataba wake na Real Madrid unaelekea kuisha majira ya joto. (Tuttosport)

Atletico Madrid wametoa ofa ya pauni milioni 30 pamoja na nyongeza ya pauni milioni 4 kwa ajili ya kumsajili kiungo wa Atalanta Ederson. (Football Italia)