Kombe la Dunia 2022: Wachezaji 17 waliozaliwa Afrika wanaoyawakilisha mataifa nje Afrika  

Na Dinah Gahamanyi

BBC News Swahili

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Ansu Fati

Huku mashindano ya soka ya  Kombe la Dunia yakiendelea nchini Qatar, maswali yamekuwa yakiibuka, mijadala imekuwa ikiibuka hususan miongoni mwa baadhi ya watumiaji wa  mitandao ya kijamii kuhusu wachezaji waliozaliwa Afrika wanaochezea timu za zisizo za Kiafrika.

Mjadala huu ulipamba moto zaidi Wiki hii  wakati Rais wa Liberia mwanasoka wa zamani wa kimataifa George Weah alipompongeza  mtoto wake wa kiume, Timothy Weah, baada ya klabu yake ya Lille kushinda taji la Ligi Kuu ya Ufaransa.

"Mimi mwenyewe kama mshindi wa taji la Ligue 1, nafahamu fika kwamba unahitaji kujitolea na kufanya kazi kwa bidii kila wiki ili kupata ushindi ,” Rais Wear alisema katika ujumbe uliowekwa katika tovuti yake rasmi ya urais.

“Licha ya kuumia mara kadhaa na kucheza mechi 28 , hiki ni kitu ambacho kimekuwa ndoto ya Tim. Japo baba yake Timothy Wear alizaliwa ni rais wa Liberia, binafsi Tim alizaliwa Brooklyn nchini Marekani na ana uraia wa Marekani.      

Lakini  je ni wachezaji gani waliozaliwa Afrika wanaozichezea timu zisizo za Afrika katika Kombe la Dunia  la mwaka huu? Na wanachezea timu gani?:

 1. Ansu Fati.(Uhuspania)

Alizaliwa mjini Bissau nchini Guinea Bissau.

2. Alphonso Davies.(Canada)

Alizaliwa  Buduburam, Ghana.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Eduardo Camavinga

3. Eduardo Camavinga.(Ufaransa)

Alizaliwa Cabinda nchini Angola  na wazazi wake walikuwa Wacongo   

4. Youssoufa Moukoko. (Ujerumani)

Alizaliwa Younde nchini Cameroon

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Danilo Pereira

5. Danilo Pereira.(Ureno)

Alizaliwa  mjini Bissau, nchini Guinea Bissau

6. Steve Mandanda.(Ufaransa)

Alizaliwa mjini Kinshasa katika Jamuhuri ya Kidemokrasi ya Congo 

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Breel Embolo

7. Breel Embolo.(Uswizi-Switzerland)

Alizaliwa mjini Yaounde nchini Cameroon

8. Mohammed Muntari. (Qatar)

Alizaliwa Kumasi, nchini  Ghana

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Amadou onana

9. Amadou onana.(Ubelgiji)

Alizaliwa mjini  Dakar, nchini  Senegal

10. Ismail Kone.(Canada)

Alizaliwa Abidjan, nchini Ivory Coast.

11. Keanu Baccus.(Australia)

Alizaliwa Durban nchini South Africa.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Musab Kheder

12. Musab Kheder.(Qatar)

Alizaliwa  Khartoum, nchini Sudan.

13. Boualem Khoukhi.(Qatar)

Alizaliwa  Bou Ismail nchini  Algeria.

14. William Carvalho.(Ureno)

Alizaliwa  Luanda, Angola.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Thomas Deng

15. Thomas Deng.(Australia)

Msudan Kusini aliyezaliwa kama mkimbizi katika kambi ya wakimbizi ya  Kakuma, nchini Kenya.

16. Awer Mabil.(Australia)

Msudan Kusini aliyezaliwa kama mkimbizi katika kambi ya wakimbizi ya  Kakuma, nchini Kenya.

17. Garang Kuol.(Australia)

Alizaliwa nchini Misri