Kwanini Trump ambaye alitishia kuishambulia Iran ameongeza muda wa kusitisha mapigano?

Chanzo cha picha, Win McNamee/Getty Images

Muda wa kusoma: Dakika 3

Hatua ya rais wa Marekani Donald Trump kuongeza muda wa usitishaji mapigano kati yao na Iran, inaonekana kama "kurudi nyuma" kutoka kwa semi zake za awali.

Saa chache tu kabla ya kutoa tangazo hilo alikuwa ameiambia shirika la habari la CNBC kuwa "natamani tuishambulie Iran na mabomu" na kuongezea kuwa jeshi la Marekani liko tayari kwa mashambulizi.

Trump awali ametishia kushambulia daraja zote, na viwanda vya nishati nchini Iran.

Saa chache kabla makataa ya makubaliano ya kwanza kutamatika, Trump alisitisha vita hivyo kwa muda usiojulikana akisema alikuwa akiitikia ombi la serikali ya Pakistan.

Katika vita hivi Trump amejaribu kuishinikiza serikali ya Iran kujisalimisha kwa kutumia vitisho, ila sasa inaonekana kuwa hayuko tayari kuishambulia Iran tena.

Shinikizo kutoka serikali ya Marekani

Chanzo cha picha, Leigh Vogel/Getty Images for About Face: Veterans Against The War

Tangazo la Trup linatoa matumaini ya mazungumzo ya kupatikana kwa amani kufanyika tena, katika siku zijazo.

Chapisho za Trump katika mitandao ya kijamii inaonyesha kuwa hana uelewa wa mapendekezo ya Iran, na nani anatoa tamko au maamuzi ya mwisho kutoka serikali ya Iran.

Hii inatoa inaleta wazi semi za Trump kuwa wamelemaza utawala wa Iran, na inababaika katika kufanya maamuzi yake ya mwisho.

Ila pia tangazo la Trump linaashiria kuwa hayuko tayari kuanzisha vita vingine vyenye ukubwa wa aina hiyo ten ana Iran.

Mvutano wa ndani kwa ndani nchini Marekani na kupanda kwa bei ya mafuta, huenda kukamzuia Trump kuanzisha vita vingine.

Aidha Trump hajatoa tarehe kamili ya kumalizika kwa usitishaji mapigano.

Kizuizi cha kijeshi cha Marekani bado kinatekelezwa katika bandari za Iran, suala ambalo Iran inaliona kama uhalifu wa kivita, na kizuizi cha kuendelea kufanya mazungumzo.

Je, Trump hana haja tena ya kuendelea na vita dhidi ya Iran?

Chanzo cha picha, Getty Images

Donald Trump ameamua kujipa muda kabla ya kufanya maamuzi.

Kabla ya hili Trump alikuwa akiishurutisha Iran kukubali matakwa yao au waanzishe mashambulizi upya.

Ila Trump ameacha kutoa vitisho vya kuishambulia Iran kwa mara ya pili sasa n ahata kuongeza muda wa usitishaji mapigano,kuashiria kwamba ana nia ya kumaliza vita hivyo.

Masuala tata kuhusu Iran bado hayajatatuliwa

Chanzo cha picha, Majid Saeedi/Getty Images

Trump kuongeza muda wa usitishaji mapigano kumeleta afueni kwa raia wa Marekani na dunia nzima, huku Marekani ikijaribu kutaka kujua ni nani wakufanya naye mazungumzo nchini Iran.

Marekani inataka kufunguliwa kwa mlango bahari wa Hormuz, na kudhibiti madini ya urani ya Iran.

Iran imesema haitaki kumiliki mabomu ya nyuklia kwa sasa labda siku za usoni. Bado kuna masuala tata ambayo pande zote mbili bado hazijatatua.

Matakwa muhimu ya usitishaji mapigano

Chanzo cha picha, U.S. Navy via Getty Images

Matakwa muhimu ya usitishaji mapigano kati ya Marekani na Iran

  • Tarehe 8 mwezi Aprili, makubaliano ya kusitisha mapigano ya wiki mbili yaliafikiwa kati ya Iran na Marekani.
  • Kulingana na Donald Trump, makubaliano hayo yalitegemea sharti kwamba Iran ifungue tena Mlango wa Bahari wa Hormuz, njia muhimu ya usafirishaji wa mafuta na bidhaa nyingine.
  • Iran iliruhusu meli kupita katika mlango huo kwa muda wa wiki mbili chini ya uangalizi wa jeshi lake na kulifunga siku moja baadaye.
  • Makamu wa Rais wa Marekani JD Vance alisafiri kwenda Pakistan kwa mazungumzo ya awali ya amani, lakini alirejea Washington, D.C. baada ya mazungumzo hayo kutibuka.
  • Baada ya kutofikiwa kwa makubaliano, Marekani ilirejesha kizuizi cha baharini dhidi ya Iran na kuongeza shinikizo la kiuchumi, ikiwa ni pamoja na vitisho vya vikwazo kwenye benki za kimataifa.