Tetesi za soka Jumamosi: Man Utd, Man City zamgombea Anderson

Chanzo cha picha, Getty Images

Muda wa kusoma: Dakika 3

Manchester United na Manchester City zote zinataka kukamilisha mpango wa kumsajili kiungo wa Nottingham Forest, Elliot Anderson, 23, haraka msimu huu wa joto kutokana na kwamba Kombe la Dunia linaweza kuongeza bei yake zaidi ya pauni milioni 100. (Sun)

Hatima ya nahodha wa Manchester United Bruno Fernandes, 31, haijulikani ikiwa klabu hiyo itapokea ofa kubwa kwa kiungo huyo wa Ureno kutoka kwa timu kama Paris St-Germain na Bayern Munich msimu huu wa joto. (Caught Offside)

Hata hivyo, Manchester United imeazimia kumbakisha Fernandes, licha ya kuwa na kifungu cha kutolewa cha pauni milioni 57 katika mkataba wake. (Express)

Chanzo cha picha, Getty Images

Liverpool imejiandaa kurekebisha kikosi chao kisichofanya vizuri, huku viongozi wa Anfield wakiwa tayari kuidhinisha marekebisho makubwa ya msimu wa joto. (Star)

Liverpool inaweza kukabiliwa na ushindani kutoka kwa wapinzani wao wa Ligi Kuu Manchester United na Newcastle ikiwa wanataka kumsajili kiungo wa kati wa Juventus mwenye umri wa miaka 25 wa Ufaransa Khephren Thuram msimu huu wa joto. (Mirror)

Mlinzi wa kimataifa wa Ujerumani chini ya umri wa miaka 21, Karim Coulibaly, anajiandaa kuondoka Werder Bremen msimu huu wa joto, huku Newcastle United ikitajwa kuwa moja ya klabu tano zinazomfuatilia mchezaji huyo wa miaka 18. (Bild)

Chanzo cha picha, Getty Images

Beki wa kati wa Argentina na Bournemouth, Marcos Senesi, 28, anataka Barcelona ifanye uhamisho wake msimu huu wa joto, lakini Liverpool, Chelsea, Aston Villa, Everton, Tottenham, Newcastle na Sunderland pia wanavutiwa. (Teamtalk)

Kiungo wa kati wa Ecuador Moises Caicedo, 24, anasema amejitolea kwa Chelsea lakini hajakataa uhamisho wa Real Madrid baadaye katika taaluma yake. (AS)

Mlinda lango wa Brighton na Uholanzi, Bart Verbruggen, 23, anaweza kuwa chaguo la msimu wa joto kwa Bayern Munich, huku Tottenham na Newcastle pia zikiwa katika harakati za kumtafuta. (Teamtalk)

Beki wa Colombia Jhon Lucumi, 27, ana uwezekano mkubwa wa kuondoka Bologna msimu huu wa joto, na Sunderland bado ina shauku ya uhamisho baada ya kushindwa kumpata miezi kadhaa iliyopita. (ForzaRoma via Sport Witness)