Ni kwanini baadhi ya dawa hazipaswi kutumiwa na vinywaji vyenye kahawa

Chanzo cha picha, Getty Images

Kwa wengi wetu, kuanza siku bila kikombe cha kahawa ni jambo lisiloweza kufikirika.  

Lakini, katika baadhi ya nyakati, wakati tunapomeza au kutumia dawa fulani asubuhi, ni bora kusubiri kwa muda mrefu kabla ya kunywa kinywaji  hiki.

Baadhi ya dawa zinaweza kumezwa katika nyakati tofauti za siku, lakini pia inashauriwa  kutozimeza pamoja na vinywaji vyenye kahawa.  

 Kuna takriban dawa 60 ambayo yanaweza kuwa na mwingiliano na kahawa  ," Antonio Javier Carcas Sansuán, anasema mtaalamu wa madawa  na profesa  katika chuo kikuu cha  Madrid, aktika mazungumzo na  BBC Mundo, ingawa mwingiliano kati ya mengi kati ya madawa haya  haya ni wa kadri.

Tunapotumia dawa, inasafiri katika mwili wetu wote, inapokuwa tumboni au katika utumbo , hupita ndani yad amu na halafu husambaa kote mwilini. 

 "Dawa hizi zinapaswa kupita katika eneo ambapo itatekeleza kitendo cha uponyaji  wa ugonjwa zinazoutibu, ni lengo la kimatibabu ," Elena Puerta Ruiz de Azúa, profesa katika kitengo cha tiba ya dawa katika Chuo kikuu cha  Navarra, aliiambia  BBC Mundo.

 Fikiria  eneo lililolengwa  kama kituo cha mkakati wa kutibu ugonjwa, protini katika miili yetu – ambayo hupokea dawa huiimarisha au kuizuia – ambapo itapunguza ufanisi.

Na kwa dawa kufanya kazi yake, inahitaji kufyonzwa na kusambazwa  kwa ufanisi.  

Halafu dawa hiyo inafaa kuzunguka kwa njia yake pekee, itengwe na mwili pamoja na viungo muhimu vya mwili katika mchakato huu ni ini, ambalo linakazi ya kusafisha mwili wetu. Lakini vipi iwapo kahawa na vinywaji vingine vyenye kafeini  itaongezwa kwenye safari hii? Inategemea dawa na lengo lake

Chanzo cha picha, Getty Images

Iwapo tunazungumzia dawa yenye lengo la kumfanya mtu asinzie , ukiichanganya na kahawa au vinywaji vyenye kiungo cha kafeini , kama vile Coca cola itakuwa na madhara kwasababu italeta athari mbaya kwa dawa kwa kutenda kinyume na matarajio ya  kile ambacho dawa ilitarajiwa kukifanya.

 Madawa kadhaa ya aina hii ni kutoka familia ya benzodiazepines, ambayo hutumiwa katika matibabu, kwa mfano kutibu ukosefu wa usingizi  na wasiwasi   

"Kafeini itafika kwenye ubongo wakati huo huo sawa na dawa hii ," anasema Puerta.

"Halafu upande mmoja utapokea kichocheo cha kafeini na upande wa pili utapokea dawa ambayo nguvu yake ya tiba imepungua: athari ambayo ni kinyume ."

Chanzo cha picha, Getty Images

"Kwa baadhi ya madawa, labda ongezeko hili  la utegili huenda lisiwe la maana kwasababu wana ukingo mpana salama, lakini kwa wengine ambao ndio wengi huhitaji kiwango kamili cha dawa, na kutopata dawa kamili kunaweza kusababisha hatari," wanaonya wataalamu

 "Ni dawa ambayo haijalishi kata imekolea kidogo au zaidi. Inaweza kuwa hatari iwapo makali yake yataongezeka .

Kufyonzwa mwilini 

Inashauriwa kwamba baadhi ya dawa, kama vile ile inayotumiwa kutibu kiwewe, kabla ya mlo wowote

Chanzo cha picha, Getty Images

Ni muhimu kwamba  uwepo wa chakula  tumboni na kwenye utumbo unaweza pia kuzuia ufyonzwaji wa  aina fulani za dawa.

 "Hata kama utameza dozi kama ilivyoshauriwa , iwapo sehemu yake haitaingia mwilini , haitakuwa na athari yoyote kwa tiba  ."

 Hatahivyo, kwa dawa, chakula ni kitu muhimu : baadhi yad awa zinazozuia majeraha zinaweza kuwa na uharibifu mkubwa kwa ute wa tumbo.

 Kwa sababu hii "wakati mwigine kile tunachokishauri ni kumezadawa na chakula ili kuia athari za majeraha tumboni."

Chanzo cha picha, Getty Images

Tetracycline , ambayo ni aina ya  antibiotic, haiendani na maziwa kwani yanaizuia kufyonzwa mwilini , anafafanua  Puerta.

 Iwapo utameza dawa ya antibiotic  ya aina hiipamoja na maziwa  , "ni sawa na kuitupa tu."

Na ni kwamba jamii hii ya  antibiotics, inapoingizwa katika bidhaa za maziwa, hutengeneza  mchanganyiko usioyeyuka  wenye   calcium, unaoitwa  chelates, ambao hautafyonzwa katika utumbo, kwa hiyo haitakuwa na athari yoyote ya tiba, kulingana na malengo yake.

Soma maelezo 

Kama madawa yanaathiri mfumo wa kati wa neva, kama vile  antidepressants,  zinamezwa, ni muhimu kufuata maagizo ya daktari, kwani kadini yenyewe huchochea sana mfumo huo.  

Chanzo cha picha, Getty Images

Kulinangana na  Puerta, ni muhimu kwamba dawa zitumiwe kama ilivyoelezwa na wataalamu wa afya. 

 "Sahau kutegemea dawa za nyumbani. Kama  umeelezwa kwamba  paketi moja ya dawa iwekwe kwenye maji iyeyuke ndio unywe, fanya hivyo, usiiweke kwenye juisi au soda wala kimiminika kingine chochote kile , kwasababu itabadili viungo vyake."

 Zaidi ya hayo, anafafanua kuwa kuna dawa nyingi ambazo hazikinzani na kahawa.     

 "Umeona kila kisa " na njia bora zaidi ni kuhakikisha unamuuliza daktari au mtaalamu wa dawa katika maduka ya dawa.

Kwa ujumla ni muhimu kunywa kahawa kwa kadri,’’ anasema Carcas.