Je kombora la X-22 ambalo Urusi ililitumia kupiga Dnieper ni la aina gani?

Chanzo cha picha, ANTON GERASHCHENKO

Maelezo ya picha, Video ya shambulio katika  Kremenchuk - X22  inaweza kuangamiza mkusanyiko wa maduka mall mara moja

Mnamo tarehe 14 Januari , jeshi la Ukraine liliripoti kwamba Urusi ilipiga jengo refu katika  Dnipro kwa kutumia kombora la aina ya  X-22 lililofyatuliwa kutoka kwenye kifyatuzi cha bomu  Tu-22m3  juu ya Kursk lililopo karibu na mpaka na  Ukraine.

Kombora la aina hii , kulingana na kamanda wa kikosi cha Air Force, katika kipindi cha dakika 30  lilipiga jengo refu  lililopo katika mtaa wa  Naberezhna Peremohy na kuwauwa watu wapatao 20  katika shambulio  hilo. Bado Urusi haijatoa kauli yoyote kuhusina na shambulio hilo   

 "Urefu, na kasi ya kombora na eneo lilipofyatuliwa viliweza kutambuliwa kwa njia ya mtambo wa rada. Bila shaka lilikuwa ni kombora la Kh-22 ,"  ilisema Air Force.

Katika msimu wa majira ya kiangazi kombora la aina hii lilipiga jumba la maduma ya bidhaa mbali mbali (mall) katika eneo la  Kremenchuk na kuwauwa watu makumi kadhaa.   

 Katika taarifa maalumu kamanda wa Air Force  Luteni Jenerali  Mykola Oleschuk alisema kwamba vikosi havina silaha zenye uwezo wa kudungua aina hii ya kombora. 

 Alisisistiza kuwa ni mifumo  ambayo inaweza kudungua ndege pekee, ambayo inaweza kutolewa kwa Ukraine na washirika wake wa kigeni katika siku zijazo (tunazungumzia kuhusu mifumo ya aina hiyo kama vile  Patriot PAC-3 or SAMP-T), ndio yenye uwezo wa kuzuia mashambulio yaliyolengwa na makombora haya ya anga.

Alitoa wito wa kutoaminiwa kwa taarifa ambazo zinapinga taarfa hizi. 

Chanzo cha picha, TYMOSHENKO. OFFICE OF THE PRESIDENT

"Tangu kuanza kwa uvamizi wa jeshi la Urusi nchini Ukraine, zaidi ya makombora ya aina hii  120 yamekuwa yakifyatuliwa  ndani ya eneo la Ukraine. Hakuna hata moja lililodunguliwa kwa njia ya ulinzi wa anga  ," alisisistiza kamanda.

 Kulingana naye,  uzito wa  wa mfuniko wa kombora hili ni  Kh-22 ambao ni sawa na kilogramu 950 , na umbali wa eneo linaloweza kupiga ni kiloita hadi  600. 

Oleschuk  alisema kuwa linapoyatuliwa kutoka maeneo ya mbali, linaweza kukwepa eneo lililolengwa kwa umbali wa mita mamia kadhaa.   

 Wakati huo huo, mwezi Mei 2022, Kamanda wa  Air Force  aliripoti kuangushwa kwa kombora la masafa la  Kh-22.  

Hatahivyo baadaye alitilia shaka hilo na kusema kuwa

"Taaarifa iliyotolea na vyanzo rasmi ni ya kuaminika kwa ujumla, lakini kuna baadahi ya taarifa zisizao za kuaminika zilizochapishwa kuhusu  "kudunguliwa " kwa Kh-22s, hilo ni ukweli ," alikiri.

Ni roketi ya zamani ya Usotieti 

Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

X-22  ni silaha mojawapo kati  ya makombora yaluyobuniwa katika enzi ya Muungano wa Usovieti  ( USSR)  katika miaka ya 1960.

 Makombora haya yalitengenezwa kwa vilipuzi vya  Tu-22 na baadaye yalirekebishwa na kuboreshwa zaidi, kombora hili likiwemo.

Kombora hili lililoboreshwa katika miaka ya 1970, lilikuwa na kasi ya kufurahisha ya mwendo wa kilomita 4,000 kwa saa . Lilikuwa na uwezo mkuwa wa kivita.

 Mwanzoni, kombora hili  ambalo hutengenezwa kwenye ndege lilibuniwa kwa ajili ya mashambulizi dhidi ya vyombo vya majini, na iliangaliwa kama yenye ufanisi sana, iliogopwa katika nchi za Magharibi. Katika filamu   "The Price of Fear"  kuna sehemu maarufu  zinazoonyesha vilipuzi hivi maarifu vikiipiga  ndege ya Marekani ya abiria kwa makombora ya  X-22.

 Katika miaka ya  1970 na  80, lilikuwa ni kombora lenye ufanisi mkubwa la masafa marefu, lenye kasi ya juu zaidi na kifuniko chake kilikuwa ni dhabiti. Hatahibyo, ukweli kwamba asili yake liliundwa kwa ajili ya mashambulio ya majini, inatoa fursa ya kuamini kuwa halina ufanisi wa kufanya mashambulio ya ardhini.

Chanzo cha picha, OFFICE OF THE PROSECUTOR GENERAL

Maelezo ya picha, Kituo cha maduka kilichoharibiwa

Kombora lililobuniwa kwa ajili ya mashambulizi ya majini ni vigumu kuweza kutumiwa kfanya mashambulizi ya nch kavu – huongozwa na mtambo wa rada na eneo linalolengwa linapaswa kuonekana wazi – kwa mfano ,  kipande cha chuma ndani ya bahari.

Eneo linalolengwa ni vigumukuonekana kwenye uso wa dunia.  

 Roketi hizi zina mfumo wa kutafuta eneo linalolengwa, ambao huziongoza katika kulenga mashambulizi yake katika maeneo yaliyolengwa. 

Hususan moja ya marekebisho yake ambapo-  X-22NA -hukuruhusu tu kufyatua kombora kwenye maeneo yaliyolengwa, kwenye ardhi  kulingana na  jinsi yalivyopangwa  " kwenye eno la ramani". Inaweza kupaa kwa kuzingatia eneo, lakini kwa ujumla liliundwa kujiongoza angani. Safari ya anga ya kituo kwa kituo.

Je ni ya kisasa  na  yana ufanisi upi?

Toleo la kwanza la  kombora la  X-22PSI  lililoboreshwa lilikuwa na ufanisi wa kiwango cha chini – labda liliweza tu kuzingira eneo.

Ilikuwa ni kilomita mia moja, uwezo ambao sio mzuri  sana kwa maeneo madogo yanayolengwa.

Baadaye, aina yake iliyoboreshwa, yenye kifuniko kipya ilitengenezwa.

Toleo la baadaye la mashambulio ya ardhini la kombora hili linafahamika kama Kh-22NA. Ni vigumu kusema lina uhanisi wa kiasi gani. 

 Lakini kwa vyovyote vile, wakati wa mashambulio yote ya Kremenchuk na Dnipro, yalijaribu kuongeza ufanisi. Kamanda wa Vikosi vya Ukraine aliripoti kuwa katika mashambulio yote mawili, vilipuzi vya , Tu-22M3 viliondoka kutoka katika uwanja wa ndege wa jimbo la Kaluga na yakapiga juu ya anga la Kursk.

Licha ya kuboreshwa,  makombora ya Kh-22NA bado ni ya zamani, na  kwa ujumla yanakabiliwa na hatari ya kudunguliwa na mifumo ya kukabiliana na mashambulio ya anga.   

 Ukiliyalinganisha na , "Caliber"  kutoka katika  Bahari nyeusi (Black Sea) yanapaa mbali zaidi   na mbali  kutoka kwenye maeneo yanayolengwa.

Kwa ujumla, kwa  Kh-22NA, kadri inavyofyatuliwa kutoka mbali, ndivyo inavyokuwa vigumu kuyapiga kwa usahihi maeneo yanayolengwa.   

Roketi hizi zina matatizo mengine – ni ngumu kuzitunza kutokana na utumiaji wake wa mafuta machafu yenye sumu. Kwa ujumla hizi ni silaha zilizopitwa na wakati, na kwa kawaida zilikuwa zikifyatuliwa  katika masafa marefu wakati wa mazoezi ya mafunzo ya kijeshi.